You are now browsing in English. Switch to Swahili
In Swahili: "Sasa unavinjari kwa Kiingereza. Rudi kwa Kiswahili"
You need to login to view profiles OR to update your profile

Create a new account

New announcements
Discussions
Proverbs

Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu

Join
or login
to VOTE for Proverb of the Month
Votes
0
Updated 4mo ago
by

Swali: Je, umejifunza zaidi kutoka kwa wazazi wako ama kupitia uzoefu wako ulimwenguni?


Methali hii hutumika wakati mtu amekosa na kupata madhara, haswa kama ameonywa... kama vile dereva wa lori katika picha hii (kutoka Oxfordshire, Uingereza). Bila kujali kama ulifunzwa na wazazi, hatimaye lazima ukabiliane na ukweli wa maisha halisi. Ona pia: Mtoto akilia wembe, mpe

Kuna shairi lililotungwa na Akilimali Snow-White juu ya methali hii:

ASOFUNZWA NA WAZAZI, HUFUNZWA NA ULIMWENGU
na Akilimali Snow-White

Zama walinipumbaza, wazee kwa kunilea,
Nikashindwa kujifunza, myendo mipya ya dunia,
Leo najipendekeza, kwa walimwengu sikia,
Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.

Kazi zote singeweza, bila kuwanyenyekea,
Kutii kuwembeleza, kisha kuwatumikia,
Hata nikawapendeza, wakanifunza kwa nia,
Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.

Sasa kusema naweza, Kizungu bila udhia,
Kama vile Kingereza, na lugha zingine pia,
Kwa juhudi najifunza, hata zimenielea,
Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.

Naweza kuzungumza, pasipo kutia doa,
Na paovu kuongoza, doa nikaliondoa,
Mwishowe pakapendeza, lingano moja hatua,
Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.

Sina nilipopasaza, pasina kupachungua,
Pande zote hachunguza, marifa nikachukuwa,
Hata najua kuuza, bidhaa na kununua,
Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.

Kiasi nilo jifunza, si haba kwa kubabia,
Nitokapo napendeza, kazi njema natumia,
Ni vigumu kuibeza, jinsi inanielea,
Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.

Haifai kupuuza, kwa kitu usicho jua,
Jaribu kupeleleza, na kisha ukichungua,
Nia unap,o ikaza, hushindwi kitu kujua,
Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.

Kazi nilizojifunza, babangu hakuzijua,
Hakujua Kingereza, kuuza na kununua,
Bali kujipendekeza, ndipo mwana nikajua,
Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.

Nawatilia nyongeza, mlio nisaidia,
Nyote mlionifunza, Rabi awape afia,
Mungu heri tawajaza, mema kuwarudishia,
Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.

- Diwani ya Akilimali

Fikeni E. M. K. Senkoro (1988) aliandika juu ya shairi hili:
[M]tu hawezi kupata uzoefu wa mambo yote yahusuyo maisha kutoka kwa wazazi wake: lazima awe tayari kufunzwa na ulimwengu, yaani kujifunza kutoka kwa wengine zaidi ya baba na mama yake. 

Nimejitahidi kutafsiri shairi hili kwa Kiingereza, na nitashukuru sana sana kupata feedback zenu, ndugu wajuaji wa Kiswahili na Kiingereza. (Someni hapa.)

Mnafikiriaje? Shairi hili lina maana gani kwako? 
Sources
Picha ni kweli, inaonyesha ajali iliyotokea Uingereza, mkoa wa Oxfordshire, (Pich kutoka mitandao ya kijamii) - Soma pia Makala hii ya BBC

Shairi lilitoka Diwani ya Akilimali

Nukuu ya mwisho inatoka kitabu cha "Ushairi - Nadharia na Tahakiki" na F.E.M.K. Senkoro, Sura ya 7 (Dar Es Salaam University Press, 1988, ISBN 9976 60 0224)  
Loading...
Loading...
Login to view and post comments
Maana yake, afadhali kuridhika na ulicho nacho, badala ya kuiweka hatarini kwa ajili ya kupata kitu kubwa zaidi.

 Methali hii ni ya zamani sana. Chanzo cha methali hii ni kitabu cha kale kiitwacho  "Hadithi ya Ahikar." (Kinajulikana pia kama "Methali za Ahiqar.")
Mwanangu, mguu wa kondoo katika mkono wako mwenyewe ni bora kuliko bega zima katika mkono wa mwengine; Afadhali kondoo mdogo aliye karibu na wee kuliko ng'ombe aliye mbali; Afadhali shomoro aliyeshikwa mkononi kuliko ndege elfu warukao angani; vazi ulilo nalo ni afadhali kuliko vazi la zambarau usiloliona.
- Hadithi ya Ahikar (ukurasa wa 110)
Kitabu hiki kinasimulia hadithi ya mshauri wa wafalme wa kale wa Ashuru na Misri. Inadhaniwa kuwa hadithi hii ilitungwa takribani 600 KK, na kuna nakala iliyochapishwa mwaka wa 500 KK. 

Methali karibu na hii kutoka nchi mbalimbali:
French:
Un tiens vaut mieux que deux tu l'auras
'Shika-hii-hapa" moja ina thamana kuliko 'nitakuletea-baadaye' mbili
Japanese
明日の百より今日の五十
Hamsini leo ni bora kuliko mia kesho
Italian
Meglio un uovo oggi che una gallina domani
Bora yai leo kuliko kuku kesho

Mnaonaje -- methali hii ni ushauri mzuri? Ni bora kuridhika na kitu kinachopatikana kwa hakika, ama kutafuta kitu bora zaidi kisicho na hakika?
...
Updated 4mo ago
by
Kila kazi kubwa katika maisha huhitaji kufanyika kwa hatua ndogo, siku baada ya siku. 

Je, unajua methali zingine zinazofanana na hii au zinazotoa dhana hiyohiyo? 

Msemo huu unakumbusha shairi liitwalo "Vitu Vidogo" na Julia Abigail Fletcher Carney: 
Matone madogo ya maji,
Chembe kidogo za mchanga, 
hutengeneza bahari kubwa
Na ardhi ya kupendeza

Vivyo hivyo zile dakika ndogo,
ingawa ni ndogo,
hutengeneza enzi za milele. 
Julia Carney alitunga shairi hili mwaka wa 1845 darasani akiwa mwanafunzi darasani -- na alipewa dakika 10 tu kuliandika!
...
Updated 4mo ago
by
Kwa kiingereza tunasema "One man's trash is another man's treasure," maana yake, kilichotupwa na mtu mmoja, kinaweza kutumikia mwingine na kuwa na thamani kwake.

Msemo huu hutumika ili kueleza jinsi mapendeleo ya watu hutofautiana, ama kuonyesha matumaini kwamba wanadamu ni wabunifu katika masuala ya kupanga upya au kuchakata vitu vilivyotupwa na wengine.

Kwa mfano, mjasiriamali Gibson Kiwago, mwanzilishi wa WAGA Tanzania, anachakata betri za laptop ili kuleta umeme kwa nyumba na maduka. Jifunze zaidi kuhusu E-Waste (Orodha ya Kusoma)!

Dhana kwamba thamani ya kitu hutegemea mtazamo wako ipo tangu zamani. Chimbuko cha msemo huu ni methali ya Kiingereza iliyotumika karne ya 17:
One man's meat is another man's poison
Nyama na mtu mmoja ni sumu ya mtu mwengine

Je umewahi kuona thamani katika kitu kilichotupwa na mwengine?
...
Updated 4mo ago
by
This proverb means that there are some things you can't do alone. The tango is dance for two people, so you can't dance the tango alone.

The proverb comes from a 1952 song It Takes Two to Tango:
You can sail in a ship by yourself,
Take a nap or a nip by yourself.
You can get into debt on your own.
There are lots of things that you can do alone.
But it takes two to tango, two to tango...
- It Takes Two to Tango (1952, Al Hoffman, Dick Manning and Pearl Bailey) - Check out the sources to listen to the original recording!

This proverb has many different meanings that you can apply in your daily life and relationships.  There are lots of things in life that require more than one person: It takes two people to cooperate, to make a bargain or to engage in a fight. You may really want to dance with someone, but if they don't want to dance with you, it's better to move on.  Similarly, if you're in a fight, consider how your own behavior might be contributing to continuing the fight. A dance isn't about being perfect, it's about being in time with your partner and enjoying the experience. 

Similar proverbs from Africa:
Egyptian (Arabic):
ايد لوحدها ماتسقفش‎
One hand can't clap

Swahili:
Bila mtu wa pili ugomvi hauanzi
Without a second person a quarrel cannot start

Kidole kimoja hakiuwi chawa
One finger doesn't kill a louse

...
Updated 4mo ago
by