Diwani Ya Akilimali

Faster download

Published Year: 1963

Book Thumbnail

Language: sw

Details: THE EAGLE PRESS Hii ni alama ya East African Literature Bureau, ambayo ni idara moja ya Jumuia ya Kazi za Kushirikiana katika Afrika ya Mashariki. Kazi yake ni kutoa vitabu na kuendesha kazi za maktaba kwa ajili ya wananchi katika Afrika ya Mashariki.

Summary: MTUNGAJI wetu Bwana K. H. A. Akilimali Snow-White ametufanyia hisani kutukusanyia mashairi yake katika sura ya kitabu hiki. Ingawa Bwana Snow-White amefanikiwa sana sana utungaji wa mashairi yu bado kijana mbichi. Hivi mashairi haya mazuri yanaeleza kwa wingi mwendo wa siasa wa vijana, na maonyo na maagizo, pamoja na hekima ya mambo yenyewe kwa namna yanavyofasirika katika maoni ya mtungaji wetu stadl. Baadhi ya mashairi ni jawabu ya mashairi yaliyoandikwa na watungaji wengine, kama ilivyo desturi mashuhuri ya toka asili ya watungaji wa mashairi ya Kiswahili kujibizana. Baadhi ya mashairi haya ni mashangilio au masimango. Baadhi ni maombi au dua. Na mengine ni mashairi yanayohusu mapenzi ndoa na talaka. Mashairi mengine yamo katika sura ya fumbo kwa mfano shairi la 'Jozi' ua 'Ua la moyoni' litafahamika kwa watungaji wengi wa Kiswahili, na hata kwa wasomaji pia kuwa linahusu ndoa na mapenzi.