We sponsored the creation of 3 pickleball courts in Arusha, Tanzania
Donate Play pickleball Learn more
We also sponsor monthly tennis tournaments Learn more
You need to login to view profiles OR to update your profile

Have an account? Login

Log in
Forgot your password?
Didn't receive your confirmation email?

Create a new account

Proverb Essay Contest
Vote Now - $20 for First Place!
The three essays that get the most s will win a cash prize. Anyone with a Maktaba.org account can vote by clicking next to an essay.
You can vote for multiple essays. Learn more: Contest Rules
View in Swahili
Some of the recent essays
Join
or login
to VOTE
Votes
9

na Mélanie N. 
Mama, mama, mama! 
     Nuru ya mtu ni mama. Ukimkosa mama imezima nuru. Aheshimiwe mama, katika dunia hakuna kitu cha kumwakilisha. 
     Angeweza kutoa mimba yako akabaki kuwa kijana.Ila alivumilia mpaka miezi tisa ya kujifungua akakuweka ulimwenguni. Husaidia Mungu kumuumba mtu. Hakujali maumivu ya kujifungua, umbo lake, sura yake, umri wake, vyote vyake mwilini mwake vilibadirika ili upate uhai. Mama hufanya chini-juu ili upate afya njema. Alifanya kila liwezekanalo ili upate elimu ya kutosha. Huacha kile ambacho kingemfurahisha ili uwe mtu. Hushinda shambani ili upate cha kutia mdomoni. Mheshimu mama aliyekutunza hadi hapo ulipofika. 
     Kwa hiyo unatoa wapi ujasili wa kumtukana mama yako unamdharau mama yako ili umheshimu nani? Eti ungetangulia mbele yake ungemzaa. Kweli? Usijiidanganye. Atukae mama yake hujikosesha baraka. Kuwa makini vijana wa leo, msijitafutie mikosi na hasara visivyo na msingi ambavyo havitomalizika. Hata kama unamzidi elimu, mama anabaki kuwa mama. Hapo ulipo ndie kasababisha upafike. Kwa hiyo fanya uwezavyo ili umtoe hapo alipo. 
     Ulibarikiwa mama, umewazidi wote mama. Hakuna cha kukulipa mama isipokuwa tu kukutakia maisha mema tena marefu.
...
Join
or login
to VOTE
Votes
7

na Alfred N. 
Hapo zamani za kale katika Kijiji cha NYAMAGOMA ,kulitokea binti moja anayeitwa SUDI Aneti ambaye katika maisha yao ya kila siku alikuwa akitamaani maisha ya raha tu. Alikuwa na  Tabia ya kuwachuna wanaume kwa kuwaomba pesa nyingi.Alipoona hayo hayatoshi aliamua kujiunga na ushirikina na kuenda kwa waganga wa kienyeji kwa lengo la kuzitafuta pesa nyingi kwa muda mfupi. Ni ukweli pesa aliipata tena ya kutosha Ila ikawa ni ya masharti .wazazi wake walijaribu kumshauri aachane na ushirikina huo bali aanzishe miradi yake huku akianzia kwa vinavyolingana na uwezo wake hakuwasikiliza.Alieendelea kuyaishi maisha hayo,huku matatizo yakawa yanamkuta kila wakati,ilifika kiasi mizimu ikamuomba uhai wa mama yake kama kafara naye akakataa kata kwa ubadaye Mali zote zilipoptea akafikia hatua ya kujuta akiukumbuka ushauli alioupewa na wazazi wake.angelikubali kulidhika na mali zinazokuja taratibu yasingelimkuta hayo yote kwa ukweli CHURURU SI NDONDONDO

Chururu /mchiriziko/myiririko
Kitenzi: kuchurura nyiririka

Ndondondo:malipo yanayokuja kila baada ya mwezi au mwaka kutokana na makubaliano ya watu wawili( mfanyakazi na bosi wake)

Malejeleo : kamusi kuu  
...
Join
or login
to VOTE
Votes
11

na Lolly F. 
🅽🅾 🅿🅰🅸🅽😔 🅽🅾 🅶🅰🅸🅽✊
No pain no gain is a proverb mostly used by many of us since we all believe in working hard and hustling alot so as we can all live a good life.
This proverb was first used by one of the famous poet in 1648 named 𝗥𝗼𝗯𝗲𝗿𝘁 𝗛𝗲𝗿𝗿𝗶𝗰𝗸 in the little poem named "no pain no gain". Some of the quoted verses of the poem include the verse that stated "man's fortunes are according to his pains".

In one of the streets in makamba village lived a poor man with his wife and two daughters. The man had a lung cancer that made him weak for couple of days and since the family had no money to pay for the hospital bills then the man was forced to stay at home without getting any treatment despite the fact that his wife worked hard but the little money she got was used for food. The two daughters had two different personalities since the older one was too proud and lazy but the Young one was kind and hard-working so the father decided to give them a test and he told them"my daughter's as u see my health is not good and despite the fact that your mother is working hard the money she gets isn't enough for treatment so I want all of you to find a good way of getting money" and so the daughters agreed and everyone went to do so. The lazy daughter spent all day sleeping but the hardworking daughter went and hustled and got alot of money and helped her family since she believed that "no pain no gain" and everyone was proud of her.

I too believe in the proverb since I have always worked hard at school and I can now see the fruits of my hardworking skills.

Similar proverb that goes along with no pain no gain is "No sweat,No sweet" and the proverb that goes contra to that is "Beauty is pain".

𝗖𝗼𝗻𝗰𝗹𝘂𝘀𝗶𝘃𝗲𝗹𝘆 ,Do we all believe that in order to achieve worthwhile goals we need to suffer or work hard?

𝗦𝗼𝘂𝗿𝗰𝗲𝘀: poemhunter.com No Pains, No Gains Poem by Robert Herrick
...
Join
or login
to VOTE
Votes
6

na Angelica A. 
Methali ya "mpanda ngazi hushuka" ina maana kwamba watu wanaopanda ngazi za mafanikio au mamlaka wanaweza kushuka haraka kutoka kwenye nafasi yao ya juu. Inatukumbusha kwamba hali ya mafanikio au umaarufu haijithibitishi kuwa ya kudumu au salama. Mambo yafuatayo yanathibitisha ukweli kuhusu methali hii;

 Hali ya Majivuno; Methali hii inaweza kutumika kuonyesha hatari ya kujivunia sana mafanikio au kuwa na kiburi. Inatuambia kwamba hali ya juu inaweza kubadilika ghafla, na mtu anaweza kupoteza kile alichokuwa nacho ikiwa hatakuwa makini au asipoweza kudumisha kiwango chake cha juu cha kazi au tabia nzuri.

 Kupandishwa cheo; Methali hii pia inaweza kutumika kuwahimiza watu wawe waangalifu na waangalie mbali zaidi, wasijiridhishe na mafanikio yaliyopatikana hadi wakati huo, na badala yake wajitahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kudumisha maadili yao ili kuepuka kuanguka. Methali hii inatufundisha baada ya kupandishwa cheo tusijisahau katika uwajibikaji wetu wa kila siku kwani kuna uwezekano pia wa kushushwa cheo au kupoteza cheo hicho tulichopata.

 Hali ya kuwa na Kiburi;  Katika maisha, methali hii  imekuwa ikitumiwa kwa muda mrefu sasa. "Mpanda ngazi hushuka." Methali hii inatufundisha somo muhimu kuhusu hatari ya kiburi na jinsi inavyoweza kusababisha kushuka kwa haraka kutoka kwenye nafasi ya juu. Hakika, methali hii ina umuhimu wake katika jamii yetu ya leo inatuhimiza tuwe watii kazini na kuwaheshimu wafanyakazi wenzetu. Katika jamii yetu ya leo, tunaona mifano mingi ya watu ambao wamepanda ngazi za mafanikio lakini wameanguka kutokana na kiburi chao. Kwa mfano, kuna watu maarufu na wenye mamlaka ambao wamejikuta katika matatizo makubwa baada ya kujisahau na kudharau wengine. Wamevurugwa na kiburi chao na wamesahau kuwa mafanikio yao yanategemea juhudi za wengine na msaada wa jamii yao. Kiburi kinaweza kusababisha mzunguko wa chuki na uhasama. Watu wenye kiburi hawataki kushirikiana na wengine au kusikiliza maoni na ushauri wanaopewa. Wanajiona kuwa juu ya wengine na hawana haja ya kujifunza au kuboresha. Kwa sababu hiyo, wao hujikuta wakitengwa na kupoteza ushirikiano na msaada wa watu wanaowazunguka.

Kupata Kazi; Watu wengi wanatafuta kazi kwa bidii ili wapate na baada ya kupata wanajisahau na kutowajibika wakiwa katika maeneo yao ya kazi na kusahau watu walio wasaidia wakati wanapotafuta kazi hali hiyo hupelekea wapoteze kazi walizo nazo na kufukuzwa kazini kama methali isemavyo "Mpanda ngazi hushuka" hivyo methali hii inahimiza watu wanapopata kazi wawe na heshima kwa jamii na wale wote walio wasaidia kupata kazi hiyo kwani wanapo kwenda kinyume na hivyo kunawapelekea kufukuzwa kazi na hali yao ya maisha kushuka  na kuwa katika hali ngumu ya maisha. 

 Hali nzuri ya kiuchumi;  Watu wenye uwezo mzuri wa kimaisha mara nyingi wanatumia hela na mali walizo nazo kwaajili ya kustarehe na kusahau kufanya vitu vya msingi kama kuwekeza hela walizo nazo kwenye biashara ili kupata faida zaidi na kuwadharau wengine wenye hali ya chini ya kimaisha. Wakati mwingine wanatumia hela walizo nazo kuponda raha kwa kuhonga na kuendekeza starehe  na kuwa na idadi ya wapenzi wengi wakiamini hela walizonazo zitawasaidia kupata watu wanao wahitaji matokeo yake wanaangukia kupata magonjwa ya zinaa. Matokeo yake baada ya kupata magonjwa wanaishia kujitibu magonjwa yasiyopona na kujikuta wanapoteza hela nyingi na kufilisika kila mara  wanabadilisha hospitali, wengine wanaenda kwa waganga wa kienyeji ili wapate dawa  za kuwatibu huku watu waliowathamini wakati wakiwa na afya njema wanawakimbia na kuhitaji msaada kutoka kwa wale waliowadharau wakati wakiwa na hali nzuri ya kiuchumi wakati mwanzoni waliwadharau na kuona hawana maana siyo hadhi yao. Methali hii ya  "Mpanda ngazi hushuka" inatufundisha tusiwadharau watu wengine hata kama tuna hali nzuri ya kiuchumi kwani ipo siku tajiri anaweza kufilisika na yule aliyedharauliwa maisha yake kubadilika na kuwa na hali nzuri kimaisha na kuwasaidia hata wale watu walikuwa wakimdharau kipindi hakiwa hana hali nzuri ya kimaisha.

Methali ya "mpanda ngazi hushuka" inahimiza watu kuwa waangalifu na waangalie mbali zaidi. Tunapaswa kudumisha unyenyekevu na kujifunza kutoka kwa wengine. Kupata mafanikio kunahitaji kazi kubwa, uvumilivu, na kujitolea.
...
Join
or login
to VOTE for Proverb of the Month
Votes
15
Join
or login
to VOTE
Votes
15

"na Ibrahim Nyanda
🏆 Shindano la Insha ya Methali
“Ni kwa nini kijiji chetu hakina maendeleo ukilinganisha na vijiji vingine vinavyotuzunguka? Vijana wengi kutoka vijiji vingine wa umri wetu wamesoma na wengine wana kazi zao za maana huko mjini. Pamoja na kwamba kuna shule kijijini kwetu lakini vijana hatufanyi vizuri shuleni na hata walimu wanapoajiriwa hawakai muda mrefu wanahama. Kuna nini hapa Bombambili?" Haya ni maswali ambayo kijana Akilimali alimwuliza rafiki yake Manase wakiwa machungani wakilisha ng’ombe. 

Mara baada ya swali hili Manase alionekana amezama katika wimbi kubwa la mawazo na mara baada ya kufikiri kwa muda alimgeukia rafiki yake Akilimali na kumtazama kwa kina kiaha akamwuliza, “Unaamini kuhusu ushirikina” Akilimali alijibu kwa kutikisa kichwa kuashiria kukubaliana na swali aliloulizwa na kisha akasema “Naamini kwani mara kadhaa nimekua nikiona watu wakienda kwa waganga na wengine wanapopitia magumu huamini wamerogwa, si unakumbuka juzi bibi Andunje tulivyoambiwa kuwa amekutwa juu ya paa la mzee Masanja uchi wa mnyama akiwanga, sasa mpaka hapo naachaje kuamini mshikaji wangu” 

Manase alimwangalia Akilimali kwa makini kisha akamwambia, "Nataka nikueleze siri moja ambayo huwezi amini……. hivi unajua kama mama yako na dada yako ni wachawi?” Akilimali alibaki ameduwaa mithili ya mjusi aloyebanwa na mlango halafu akiwa amefura kwa hasira akamwambia Manase “Aisee mwanangu usianze kuniletea habari zako za udwanzi hapa, tena koma kabisa kumwambia mama yangu mchawi vinginevyo ntakuja kukufanyia kitu mbaya hutokuja kuamini macho yako, ohoooo!!” 

Manase alimtuliza rafiki ake Akilimali halafu akamwambia, “Ngoja niwarudishe ng’ombe jirani afu nikupe mchapo mzima ulivyo, najua utanielewa we punguza jaziba kwanza” 

Mara baada ya kurudisha mifugo jirani Manase akaanza kumweleza Akilimali, “Rafiki angu nataka nikupe siri hii ambayo nimekaa nayo kwa muda mrefu, chochote unachokiona hapa hata kutokuwepo kwa naendeleo kijijini ni kwa sababu ya ushirikina, kila siku mama yako na dada yako huwa ninawaona wakija nyumbani wamepanda fisi wakimpitia mama kwenda kuwanga…..” Manase alitulia kidogo halafu akaendelea 

“Huwezi kuamini kwani hata mimj nilikua siamini mpaka nilipopakwa dawa na kuwaona, nitakupa hiyo dawa utapaka machoni na utakuja kunipa majibu kesho.” 

Mara baada ya mlo wa usiku Akilimali alikua ameketi akiota moto nje ya nyumba yao ya udongo iliyoezekwa kwa nyasi wakati huo mama yake na dada yake wakiwa ndani na yeye akiwa na baba yake pale nje. Alipaka ile dawa kama alivyoelekezwa na baada ya dakika kumi alimwona dada yake na mama yake wamepanda juu ya fisi mithili ya pikipiki tayari kwa safari ya kwenda kuwanga. 

“Nisamehe sana rafiki angu, ilikua ni hasira tu” aliongea maneno haya Akilimali huku akilengwa na machozi, 

“Mimi nilijua, sasa unavyoona kijijj chetu hakiendelei hata mama yako pia na dada yako wanahusika, inaumiza sana kila mwanakijiji anayetaka kuleta maendeleo anaishia kufa, lazima kuna siku watakuja kuumbuka kama ilivyokua kwa bibi Andunje” 

“Nina uhakika hata baba yako hajui kama mama yako na dada yako ni wachawi na kila siku huwa wanaenda kuwanga na ninyi kuwaachia mauzauza mkijua wapo, nenda kampake baba yako hiyo dawa alafu utanipa majibu” alieleza Manase 

Jioni kwa siri Akilimali alimweleza baba yake kuwa dada yake na mama yake ni wachawi kitu ambacho alipinga vikali. 

“Mama leo baba anatuona, angalia anvyotutumbulia macho” dada yake na Akilimali alimwabia mama yake wakiwa juu ya fisi kama ilivyo ada wakati baba yake na kaka yake wakiwa nje wanaota moto kama ilivyo kawaida yao. 

“Sidhani kama anatuona, hebu geuza fisi tuwe kama tunawaelekea wao” ailisema mana yake na Akilimali.

Akilimali anasema hiyo ndiyo ilikua siku ya mwisho kumwona baba yake kwani baada ya kuona fisi aliyewabeba mke wake na binti yake alitimua mbio kama anashundana mashindano ya mbio za mita mia. Ama kweli usilolijua ni kama usiku wa giza, Akilimali alibaki haamini kama kwa muda wote huo ameishi na mama yake na dada yake bila kujua kuwa ni wachawi. 
...
Sources

Chimbuko:

Methali ya kiswahili kutoka kitabu cha “METHALI ZETU” cha Oxford inayosema “USILOLIJUA NI KAMA USIKU WA GIZA.”  

Juu ya Insha hii

Insha hii ilishika nafasi ya nne katika Shindano la Methali ya Insha la Maktaba.org 🏆 7/7/2023
Ibrahim Methusela Nyanda ni Mtanzania 🇹🇿 

Hakimiliki

Creative Commons Attribution (CC BY 4.0)
na Ibrahim Nyanda
Ilichapishwa na Maktaba.org
Mchoro/Image: CC BY Maktaba.org
Join
or login
to VOTE for Proverb of the Month
Votes
61
Join
or login
to VOTE
Votes
61

na Rose Mwanri 🇹🇿 
🏆 Shindano la Insha ya Methali 
🥈 Mshindi wa Pili 

Akiba Haiozi

Methali ni usemi wa kimafumbo unaotumika katika jamii. Maneno katika methali huwa na maana ya ziada na methali huwa na pande mbili. Upande wa kwanza hutoa wazo na upande wa pili humalizia wazo. Akiba haiozi ni miongoni mwa methali za kiswahili inayotumika sana katika jamii za kiafrika na kwa watumiaji wa lugha ya kiswahili duniani, ikiwa na lengo la kuwaasa watu juu ya umuhimu wa kujiwekea akiba.

 Dhima ya methali hii ni kutusisitiza sisi wanajamii kujianda vema na maisha ya leo pamoja na kesho huku tukiwa tayari kuzikabili changamoto mbalimbali za maisha.

 Methali hii hutuonyesha ni kawaida mwanadamu kupatwa na dharura mbalimbali katika maisha ya kila siku. Mfano kupatwa na maradhi, ajali, au hata kifo. Pale unapokuwa na akiba uliyojiwekea itakusaidia wakati umepatwa na changamoto ya ghafla ambayo hukuitarajia.

 Faida nyingine ya kuweka akiba ni kuboresha maisha. Cha kwanza nashauri tuwe na utaratibu wa kuweka akiba mara kwa mara ili kuweza kuboresha maisha yetu kwa ujumla. Tunavyozidi kuweka akiba ndivyo ambavyo akiba hiyo inaweza kutusaidia kuboresha makazi yetu na miundombinu kwa ujumla ndani ya jamii zetu. Mfano mzuri ni wazazi ambao akiba wanazoziweka huwasaidia kulipa karo za shule pamoja na kununua vifa mbalimbali vya shulena hata gharama zingine zinazojitokeza kwa wakati huo.

 Methali hii pia inatukumbusha kuwa kadri tunavyozidi kuweka akiba ndivyo tunavyokuza hazina yetu. Swa na ile methali inayosema “ Haba na haba hujaza kibaba” ukichambua methali hizi zinaendana maana na utagundua ni ukumbusho mkubwa kwetu kuhusu ujenzi wa hatma njema ya jamii yetu ya sasa na baadae. Kwa kuwa zinatuhimiza kuwekeza kwa kila chumo tulipatalo. Tunakuza hazina kwa kuwa kile tunachoweka akiba kipo kwaajili yetu.

 Chukua nafasi kujiuliza, ni mara ngapi umepatwa na changamoto na akiba ndiyo ikaokoa jahazi, ni mambo mangapi yametokea bila taarifa na akiba ndiyo imetumika kuweka mambo sawa. Naamini sote tunapaswa kuweka akiba bila kujali kipato ni kikubwa au kidogo. Mfano unaweza kuanza kuweka akiba kidogo kidogo kutokana na kile unachokipata na kufikia muda Fulani utakuwa na akiba kubwa.

 Vilevile methali hii inasaidia kukuza maarifa kwa mtu mmoja mmoja na jamii hasa pale ambapo pamekuwepo na tofauti ya uhifadhi wa akiba kutoka kizazi kimoja kwenda kingine. Hapo zamani tunaambiwa watu walikuwa wanahifadhi akiba zao kwa kuchimba chini ya ardhi, kuweka chini ya kitanda au hata sehemu zingine ambazo wao waliamini ni salama. Leo hii watu hawatumii sana njia za kienyeji kuweka akiba zao. Ukija kwenye fedha zipo benki zenye mifumo thabiti na salama katika kuhifadhi fedha. Kwa upande wa akiba ya mazao pia zipo njia salama za kuhifadhi tena hata kwa muda mrefu bila kuharibika. Kwa hakika akiba haiozi.

 Waswahili tunasema “akiba haiozi”, “haba na haba hujaza kibaba” ikimaanisha kwamba akiba yaweza kuonekana ndogo ila kadri inavyoongezeka ndivyo inavyokuwa kubwa. Kinyume chake tunaambiwa “Chovya chovya humaliza buyu la asali”, “Bandu bandu humaliza gogo”. Tukikumbushwa kuwa vile tunavyochukua akiba zetu kidogo kidogo bila sababu ya msingi ndivyo ambavyo iko siku tutahamaki na kuona akiba imeisha bila kuona kitu cha maana kilichofanyika. Tukumbuke “mali bila daftari huisha bila habari”, tuangalie mfano wa shairi hili linalotusisitiza kuhusu kuweka akiba.

Akiba kweli hazina, haijawahi saliti,
Kwetu ni muhimu sana, hutubeba kwa nyakati,
Kipindi kweli hatuna, inasimama kwa dhati,
Sote tuweke akiba, akiba ni mkombozi.

 Kwa hakika ni dhahiri yatupasa kutunza vitu vyetu vizuri na rasilimali tulizonazo kwa kuweka akiba ili tuweze kujinusuru pale ambapo tunapokumbwa na changamoto za kushtukiza kwa ajili ya maisha yetu ya sasa na ya baadae.

...
Sources

Juu ya Insha hii

Insha hii ilishinda nafasi ya pili 🥈 katika Shindano la Methali ya Insha la Maktaba.org 🏆 7/7/2023
Rose Mwanri ni mwalimu Mtanzania 🇹🇿 

Hakimiliki

Creative Commons Attribution (CC BY 4.0)
na Rose Mwanri
Ilichapishwa na Maktaba.org
Mchoro/Image: CC BY Maktaba.org

Related on Maktaba.org 


Join
or login
to VOTE for Proverb of the Month
Votes
62
Join
or login
to VOTE
Votes
62

na Magreth Lazaro Mafie 🇹🇿
🏆 Shindano la Insha ya Methali 
🥉 Mshindi wa Tatu
Ni mara ngapi umesikia Mchumia juani hulia kivulini? Hii ni methali ya kiswahili (kibantu) yenye maana ya kuwatia moyo watu katika shughuli mbalimbali wanazozifanya Kila siku wawe na Imani kuwa ipo siku watayafurahia matunda ya kazi yao. 

Methali hii huwapa watu nguvu, bidii, moyo, ujasiri, tumaini na weledi katika kufanya kazi. Mfanyakazi huamini kuwa baada ya kazi ngumu zenye surubu basi huleta mavuno mazuri yenye kumfanya astareheke kivulini akila matunda ya kazi yake. Shairi lifuatalo linaonesha kwa namna gani mchumia juani huwa katika majukumu ya Kila siku.

Siogopi jua wala mvua, nikiitengeneza kesho yangu
Siogopi maumivu Wala majeraha, maana yote ni ya muda
Jua kali na kazi ndiyo desturi yangu, ili kheri kuja maishani
Machinga,mkulima, makuli na mvuvi wao na jua, Ili kuitafuta kesho
Mchumia juani, hulia kivulini bado nakitafuta kivuli.
Ni mchana jua la utosi, kichwani nina mavuno, jasho linatiririka
Jua limezama Sasa kasia ufukweni, hoi kitandani, nyavu zi baharini
Nyumbani mtaa wa nne, nahodha wa familia surubu nivute  kheri
Jua Sasa la chomoza, Kiguu na njia kulitafuta tonge
Mchumia juani, hulia kivulini bado nakitafuta kivuli.

Bwana mmoja alikuwa mkulima. Maisha yake yote alitumia katika kilimo. Hivyo kupendeza kwake kulikuwa mara chache. Watu kijijini kwake walimuita mkulima stadi. Alijenga nyumba kwa kuuza sehemu ya mazao yake, alisomesha wanae kwa kilimo.

Bwana huyu alikuwa mtu mwenye bidii alijifunza siku zote kanuni za mkulima bora, hivyo kadri muda unavyokwenda mashamba yake alivuna mazao mengi. Watu wengi walistaajabu sana kuona mabadiliko makubwa ndani ya familia yake. Aliwekeza vitu vingi kijijini kwake, mashamba, nyumba, maduka na mifugo mingi vilitoka shambani.

Watu wengi walikuja kujichukulia hekima kwa mkulima stadi. Siku zote aliwaambia "Mchumia juani, hulia kivulini. Jembe limeniheshimisha kijijini Mimi na familia yangu. Maisha yangu sasa yanakwenda barabara kwa hakika niko kivulini nafurahia matunda ya kazi yangu ya juani. Mimi leo kijana wa mkulima huyo stadi najivunia malezi, uwajibikaji wake kwa sababu kazi za juani leo zimetufanya tupumzike na kula kivulini. Kwa hakika maana ya mchumia juani inaonekana kwa vitendo. Bidii yako ndilo jua lako na kivuli ndiyo matunda ya bidii yako.

Hadithi hii inashibishwa na hadithi ilee ya "Mabala the Farmer" yaani Mabala Mkulima iliyoandikwa na Richard S. Mabala(1989). 

Mabala alikuwa mfanyakazi bandarini Kisha akapunguzwa hivyo akachagua kurudi kijijini Morogoro. Mabala alikuwa mzembe,mlevi na mbishi. Mabala alikwenda shambani na galoni ya pombe alikunywa na kulala, alipoamka alimwongelesha mkewe lakni hakujibiwa zaidi ya  sauti ya jembe tik-tok, tik-tok .

Mabala alikuwa mbishi, alimwagilia sukari shambani alifikiri ni mbolea, lakni mwisho alibadilika na kuwa mkulima stadi akawa mchumia juani ili familia yake ije kulia kivulini. Je wewe unahisi Mabala ni mchumia juani? Ndani ya familia au kwenye jamii mkulima stadi anakupa picha gani?

Mwisho hadithi hii kutoka katika methali ya mchumia juani hulia kivulini hutuonyesha dira njema katika kila tunachokifanya katika maisha ya kila siku. Huku methali kama Subira yavuta kheri, Mgaa na Upwa hali wali mkavu zote hufanana kimaudhui, zipo katika kuipa jamii nguvu na matumaini kwa kila jambo lifanyikalo katika malengo.
...
Sources

Juu ya Insha hii

Insha hii ilishinda nafasi ya tatu 🥉 katika Shindano la Methali ya Insha la Maktaba.org 🏆 7/7/2023
Magreth Lazaro Mafie ni mwanafunzi Mtanzania 🇹🇿 

Hakimiliki

Creative Commons Attribution (CC BY 4.0)
na Magreth Lazaro Mafie
Ilichapishwa na Maktaba.org
Mchoro/Image: CC BY Maktaba.org

The original essay included the following image, which is not included in the Creative Commons license.
Mchoro huu na / This image from: Honey Bee Arts - YouTube


Join
or login
to VOTE for Proverb of the Month
Votes
86
Join
or login
to VOTE
Votes
86

by Nankya Sauda 🇺🇬
🏆 Proverb Essay Contest 
🥇 First Place Winner

Still waters run deep

Ever taken time to wonder why the elderly will always live to be wiser than the young? Have you ever taken time to meditate on where your origin sprouts from? If not, it is high time you started looking for your origin because it is important for one to know their roots. 
 Over time, you take the burden to unveil the nature of famous geniuses and their personalities, you will come to realize that they are celebrated introverts.  It is important that one takes off some time their busy schedule and read about some of the top celebrated geniuses like Albert Einstein , the famous scientist from whom we derive one of the most educative quotes;
The monotony and solitude of a quiet life stimulates the creative mind.”

This highlights that time spent alone does not only provide one with space for self-reflection but also gives space to someone to use their mind creatively. Great talkers are great are great lawyers they say, and we have seen this happening during our daily routine where people make empty promises, make false declarations to please those around them but may never take time off to do something in a bid to realize their words. Because of that, many have ended up losing trust in these so called great talkers.
     On the other hand however, silent people have always blown our minds with their actions. Their moves are always calculated, their ambitions clear and their actions intentional. Romantic lovers in a relationship are always spicing up their relationships with new inventions to keep their love blooming. Those that have employed or stayed around introverts can justify that staying around these people has been one of the greatest achievements in their lives, for these have always worked  smarter, had critical thinking sessions in their alone time and eventually produced the best results and the biggest promotions.
     Literally, we can loosely define proverbs as traditional sayings that are particular to a particular country. They are short and wise sayings that usually offer advice as well as boost an idea in relation to the day to day life.  In fact, for one to have a clear and elaborate understanding of cultural norms and practices, it is wise that they always make a reference to proverbs since they can have an elaborate meaning beneath them.
     Historically, the proverb “STILL WATER RUNS DEEP” draws its origin from the ancient times in Latin. It became popular after Shakespeare used it in his play Henry vi in 1590. He said;
“Smooth runs the water where the brook is deep”

We realize that, in some instances the most dangerous people with the wickedest hearts have always calculated their moves and taken action at a time everyone least expects them to. That is why betrayals come from people we least expect them from. It is therefore crucial for someone to not only take what the eyes meet but also take caution especially from people who do not retaliate immediately after they have been provoked or confronted.
     Albert Einstein despite his introverted character, he his famously known for devising his theory of relativity which revolutionized our understanding of space, time, gravity and the universe.
     Conclusively, it is very important  not to draw conclusions just because looks are deceptive and there is always more to know and discover than the eyes can see.
...
Sources

About this Essay

This essay won first place 🥇 in Maktaba.org's Proverb Essay Contest 🏆 July 2023
NANKYA SAUDA is from Uganda 🇺🇬 age 21 

Copyright 

Creative Commons Attribution (CC BY 4.0)
Essay by Nankya Sauda
Published by Maktaba.org
Image: CC BY Maktaba.org
Image created from "Weeping Willows by Akerselven" by Thorolf Holmboe, Public Domain 1907 

Related Books available free on Maktaba.org 

Henry VI: Part II na William Shakespeare
Relativity: The Special and General Theory na Albert Einstein 
Join
or login
to VOTE
Votes
6

na Gaston Ch.  
Methali hii inatokana na mila na desturi za Kiafrika ambapo wakunga wana jukumu kubwa katika mchakato wa kujifungua. Wakunga wanajulikana kwa uwezo wao wa kusaidia wanawake wajawazito wakati wa uzazi na mama na mtoto wanapohitaji msaada wa kiafya na kihisia. Chimbuko lake linaweza kupatikana katika tamaduni mbalimbali za Kiafrika.

Methali hii hutumika kuelezea umuhimu wa kuwa na heshima na kutokuwatukana watu wanaoleta mabadiliko au wanaoshikilia nafasi muhimu katika jamii. Wakunga ni mfano mzuri wa watu hawa. Wanawake wajawazito wana shida na mahitaji ya pekee, na wanahitaji wakunga wanaowaheshimu na kuwathamini. Methali hii inatumika kuonyesha kuwa ni muhimu kuheshimu na kuthamini kazi na jukumu la mtu yeyote katika jamii.

Aliyekuwa kijiji cha Mbinguni kulikuwa na mama mjamzito aitwaye Amina. Wakati wa kujifungua, alijikuta akijitenga na kukataa msaada wa wakunga katika kijiji chao. Aliwaona wakunga kama watu wasio na thamani na alikuwa akipenda kufanya mambo pekee yake. Siku ya kujifungua ilifika na Amina akapatwa na matatizo wakati wa uzazi. Aliumia sana na hakuwa na mtu wa kumsaidia. Baada ya masaa mengi ya mateso, mtoto wake aliokolewa tu na kijana aliyekuwa mwathirika wa kutukana wakunga. Amina aligundua kuwa angekuwa amepata msaada mkubwa na uzazi ungelikuwa rahisi iwapo angewathamini na kuwashukuru wakunga wenye ujuzi katika kijiji chake. Tangu siku hiyo, Amina alieneza ujumbe projeni na akawa balozi wa kuheshimu wakunga katika kijiji chake na maeneo mengine.

Nilipata uzoefu mkubwa wa methali hii wakati wa ujauzito wangu wa kwanza. Nilihisi kujiamini na niliamua kuwa nina uwezo wa kujifungua bila msaada wa wakunga. Nilidhani nilikuwa na maarifa ya kutosha kutokana na kusoma na kutazama video za kujifungua. Hata hivyo, wakati wa kujifungua, nilikumbana na shida na maumivu makali. Nilikuwa nimedharau umuhimu wa wakunga na hivyo nilijikuta nikiteseka peke yangu. Baada ya masaa mengi ya mateso, niliweza kujifungua salama tu baada ya msaada wa wakunga waliofika dakika za mwisho. Uzoefu huu ulinifundisha umuhimu wa kuheshimu na kuthamini msaada wa wakunga wakati wa uzazi.

Ili kutekeleza methali hii katika maisha yetu ya kila siku, tunapaswa kuheshimu na kuthamini wengine, hasa wale walio na majukumu muhimu katika jamii. Tunapaswa kuwa na ufahamu wa mchango wao na kuheshimu ujuzi wao. Katika maisha yetu ya kila siku, tunapaswa kuwa na tahadhari katika kutoa maoni yasiyo ya heshima na kuepuka kuwatukana wale wanaoleta mabadiliko au wanaoshikilia jukumu muhimu.

Katika jamii za Kiafrika, wakunga wana jukumu muhimu katika mchakato wa kujifungua. Hawa ni wataalamu ambao hujitolea kumsaidia mwanamke mjamzito wakati wa kujifungua. Wanao maarifa ya kina juu ya uzazi na wanaweza kutoa ushauri na msaada wa kimwili na kihisia wakati wa uzazi. Ni muhimu kuheshimu na kuthamini ujuzi wa wakunga katika jamii zetu.

Methali zinazohusiana: "Usimcheke ng'ombe kabla ya shingo kuvunjika" (Kiswahili): Ina maana kwamba haipaswi kumdharau mtu au kusherehekea mapema kabla ya kutimiza malengo yao.

- "Man proposes, God disposes" (Kiingereza): Ina maana kwamba mipango ya binadamu inaweza kubadilishwa na nguvu za juu au hali zisizotarajiwa.

Methali zinazopingana: "Afande ni mtaji wa mwizi" (Kiswahili): Ina maana kwamba mtu anayefanya kazi na mwizi anapata faida kutokana na vitendo vya uhalifu.

- "Usijifanye mjuzi, kizuri cha mwenzio sikikiri" (Kiswahili): Ina maana kwamba haipaswi kujidai kujua kila kitu na kukataa kujifunza kutoka kwa wengine.

Majadiliano: Je, umewahi kupata uzoefu wa kuwadharau au kuwatukana watu ambao walikuwa na jukumu muhimu katika maisha yako? Je, ulitambua umuhimu wao baadaye? Ni nini kilichokufanya ubadilishe mtazamo wako kuelekea wao?

...