We support the Reading community in Arusha, Tanzania
Read more Learn more
Posts / Proverbs Proverb of the day
SW

Kama hujui kufunga kamba, funga vingi

Hapo zamani za kale kulikuwa na kijana aliyetafuta kipaji chake. Siku moja, alishauriwa na babu yake “Kila mtu ana kipaji, utafute chako.” Kwa hivyo, alianza safari ya kukitafuta.

Barabarani aliwakuta vijana wenzake wakicheza mpira wa miguu. Walimkaribisha na akaanza kucheza nao. “Labda hiki ndicho kipaji changu!” alijisemea moyoni.  Hata hivyo, mpira ulipomkaribia, aliogopa. "Sijui kupiga mpira!" akaasema. Wengine wakamkimbiza wakimchekea.

Mtaani, alikutana na mmachinga. “Labda hiki ndicho kipaji changu.” alifikiria. Mmachinga alimkubali, akamwagiza “Msalimie huyu mteja.” Lakini mteja alipomkaribia, kijana aliogopa, “Sijui jinsi ya kumsalimia mteja!” alisema kijana. Mmachinga alikasirika, na kijana akafukuzwa tena.

Akiendelea kutemebea alifikiria “Najuta kutoka leo, sina kipaji chochote.” Alipofika ufukweni, alikutana na mvuvi. Mvuvi alimkaribisha na akaingia mashuani. Mvuvi akampa kamba na kusema “Funga hii.” “Sijui kufunga kamba!” kijana alimjibu mara moja. Mvuvi akamjibu “Kama hujui kufunga kamba, funga nyingi.”

Baada ya siku hiyo, kijana alijifunza mengi kutoka kwa mvuvi, na alifunga maelfu ya kamba. Hatimaye, alikuwa mvuvi stadi aliyeheshimiwa na jamii.

Kipaji chako hakipo tu katika asili yako, bali kinaundwa na juhudi unazozitoa. Ukubali kufundishwa na wengine, na usiogope kujaribu vipya. Fundo la kwanza utakalofunga, hulifungwi vizuri sana. Lakini kadri unavyoendelea kufunga kamba nyingi, ndivyo utakavyojifunza mbinu na mikakati bora.

Yule anayesema "siwezi" hujizuia nafasi za kujifunza. Kama hujui jinsi ya kufanya kitu fulani, ujifunze kwa vitendo na mazoezi. Kama hujui kupiga mpira, piga mipira mingi. Kama hujui kusalimia wateja, wasalimie wengi. Kama hujui kufunga kamba, funga nyingi.
Play Tennis or Pickleball in Arusha, Tanzania

Your reservations contribute to supporting:

for kids, teens and adults in Arusha, Tanzania

and the maintenance and upkeep of the courts.

We recently built 3 new lighted pickleball courts in Arusha, Tanzania!

Support fitness, sports and education in East Africa

Help us support great programs in East Africa