You are now browsing in English. Switch to Swahili
In Swahili: "Sasa unavinjari kwa Kiingereza. Rudi kwa Kiswahili"
You need to login to view profiles OR to update your profile

Create a new account

New announcements
Discussions
Proverbs

Ahadi ni deni

Join
or login
to VOTE for Proverb of the Month
Votes
0
Updated 5mo ago
by
View this proverb in English
A promise is a debt
Hakika methali hii inaonyesha kanuni muhimu kuhusu mahusiano: Kutoa ahadi hujenga matarajio katika watu wengine. Tunapokosa kutimiza ahadi zetu, tunaharibu mahusiano yetu na jina letu. Ukitoa ahadi, jiulize, "Je, tungeandika mkataba wa maandishi unaosema hivyo, ningekuwa tayari kutia saini?" 

Kifaransa:
Chose promise, chose due.
Lililoahadiwa litadaiwa
Kirusi:
Долг платежом красен, а займы отдачею.
Deni ni nzuri linapolipwa, na mikopo inaporudishwa.
Kilatini:
Pacta sunt servanda
Makubaliano lazima yaheshimiwe. (Kanuni muhimu ya sheria ya kimataifa)
Kichina
口說無憑
Maneno yaliyosemwa hayana uthibitisho.
Kiingereza
Your word is your bond.
Neno lako ni dhamana yako.

Mnaonaje? Ahadi ina nguvu kama mkataba?
Sources
Kirusi: attested to here and in this 1941 USSR propaganda poster
Kichina: 口說無憑 Spoken words are no guarantee.
Kiingereza: Word is bond
Loading...
Loading...
Login to view and post comments
Watu wengi wanaogopa kuuliza maswali kwa sababu wanahofia kuonwa mjinga. Lakini kuuliza maswali ni njia bora ya kujifunza kutoka kwa wengine. 

Pia kuuliza maswali husaidia wenzako. Je umewahi kusita kuuliza swali kwani ulidhani wengine wameshaelewa... lakini baadaye uligundua hawakuelewa pia? 

Kiingereza
There's no such thing as a stupid question
...
Updated 5mo ago
by
This proverb means that there are some things you can't do alone. The tango is dance for two people, so you can't dance the tango alone.

The proverb comes from a 1952 song It Takes Two to Tango:
You can sail in a ship by yourself,
Take a nap or a nip by yourself.
You can get into debt on your own.
There are lots of things that you can do alone.
But it takes two to tango, two to tango...
- It Takes Two to Tango (1952, Al Hoffman, Dick Manning and Pearl Bailey) - Check out the sources to listen to the original recording!

This proverb has many different meanings that you can apply in your daily life and relationships.  There are lots of things in life that require more than one person: It takes two people to cooperate, to make a bargain or to engage in a fight. You may really want to dance with someone, but if they don't want to dance with you, it's better to move on.  Similarly, if you're in a fight, consider how your own behavior might be contributing to continuing the fight. A dance isn't about being perfect, it's about being in time with your partner and enjoying the experience. 

Similar proverbs from Africa:
Egyptian (Arabic):
ايد لوحدها ماتسقفش‎
One hand can't clap

Swahili:
Bila mtu wa pili ugomvi hauanzi
Without a second person a quarrel cannot start

Kidole kimoja hakiuwi chawa
One finger doesn't kill a louse

...
Updated 5mo ago
by
na Rose Mwanri 🇹🇿 
🏆 Shindano la Insha ya Methali 
🥈 Mshindi wa Pili 

Akiba Haiozi

Methali ni usemi wa kimafumbo unaotumika katika jamii. Maneno katika methali huwa na maana ya ziada na methali huwa na pande mbili. Upande wa kwanza hutoa wazo na upande wa pili humalizia wazo. Akiba haiozi ni miongoni mwa methali za kiswahili inayotumika sana katika jamii za kiafrika na kwa watumiaji wa lugha ya kiswahili duniani, ikiwa na lengo la kuwaasa watu juu ya umuhimu wa kujiwekea akiba.

 Dhima ya methali hii ni kutusisitiza sisi wanajamii kujianda vema na maisha ya leo pamoja na kesho huku tukiwa tayari kuzikabili changamoto mbalimbali za maisha.

 Methali hii hutuonyesha ni kawaida mwanadamu kupatwa na dharura mbalimbali katika maisha ya kila siku. Mfano kupatwa na maradhi, ajali, au hata kifo. Pale unapokuwa na akiba uliyojiwekea itakusaidia wakati umepatwa na changamoto ya ghafla ambayo hukuitarajia.

 Faida nyingine ya kuweka akiba ni kuboresha maisha. Cha kwanza nashauri tuwe na utaratibu wa kuweka akiba mara kwa mara ili kuweza kuboresha maisha yetu kwa ujumla. Tunavyozidi kuweka akiba ndivyo ambavyo akiba hiyo inaweza kutusaidia kuboresha makazi yetu na miundombinu kwa ujumla ndani ya jamii zetu. Mfano mzuri ni wazazi ambao akiba wanazoziweka huwasaidia kulipa karo za shule pamoja na kununua vifa mbalimbali vya shulena hata gharama zingine zinazojitokeza kwa wakati huo.

 Methali hii pia inatukumbusha kuwa kadri tunavyozidi kuweka akiba ndivyo tunavyokuza hazina yetu. Swa na ile methali inayosema “ Haba na haba hujaza kibaba” ukichambua methali hizi zinaendana maana na utagundua ni ukumbusho mkubwa kwetu kuhusu ujenzi wa hatma njema ya jamii yetu ya sasa na baadae. Kwa kuwa zinatuhimiza kuwekeza kwa kila chumo tulipatalo. Tunakuza hazina kwa kuwa kile tunachoweka akiba kipo kwaajili yetu.

 Chukua nafasi kujiuliza, ni mara ngapi umepatwa na changamoto na akiba ndiyo ikaokoa jahazi, ni mambo mangapi yametokea bila taarifa na akiba ndiyo imetumika kuweka mambo sawa. Naamini sote tunapaswa kuweka akiba bila kujali kipato ni kikubwa au kidogo. Mfano unaweza kuanza kuweka akiba kidogo kidogo kutokana na kile unachokipata na kufikia muda Fulani utakuwa na akiba kubwa.

 Vilevile methali hii inasaidia kukuza maarifa kwa mtu mmoja mmoja na jamii hasa pale ambapo pamekuwepo na tofauti ya uhifadhi wa akiba kutoka kizazi kimoja kwenda kingine. Hapo zamani tunaambiwa watu walikuwa wanahifadhi akiba zao kwa kuchimba chini ya ardhi, kuweka chini ya kitanda au hata sehemu zingine ambazo wao waliamini ni salama. Leo hii watu hawatumii sana njia za kienyeji kuweka akiba zao. Ukija kwenye fedha zipo benki zenye mifumo thabiti na salama katika kuhifadhi fedha. Kwa upande wa akiba ya mazao pia zipo njia salama za kuhifadhi tena hata kwa muda mrefu bila kuharibika. Kwa hakika akiba haiozi.

 Waswahili tunasema “akiba haiozi”, “haba na haba hujaza kibaba” ikimaanisha kwamba akiba yaweza kuonekana ndogo ila kadri inavyoongezeka ndivyo inavyokuwa kubwa. Kinyume chake tunaambiwa “Chovya chovya humaliza buyu la asali”, “Bandu bandu humaliza gogo”. Tukikumbushwa kuwa vile tunavyochukua akiba zetu kidogo kidogo bila sababu ya msingi ndivyo ambavyo iko siku tutahamaki na kuona akiba imeisha bila kuona kitu cha maana kilichofanyika. Tukumbuke “mali bila daftari huisha bila habari”, tuangalie mfano wa shairi hili linalotusisitiza kuhusu kuweka akiba.

Akiba kweli hazina, haijawahi saliti,
Kwetu ni muhimu sana, hutubeba kwa nyakati,
Kipindi kweli hatuna, inasimama kwa dhati,
Sote tuweke akiba, akiba ni mkombozi.

 Kwa hakika ni dhahiri yatupasa kutunza vitu vyetu vizuri na rasilimali tulizonazo kwa kuweka akiba ili tuweze kujinusuru pale ambapo tunapokumbwa na changamoto za kushtukiza kwa ajili ya maisha yetu ya sasa na ya baadae.

...
Maana yake, afadhali kuridhika na ulicho nacho, badala ya kuiweka hatarini kwa ajili ya kupata kitu kubwa zaidi.

 Methali hii ni ya zamani sana. Chanzo cha methali hii ni kitabu cha kale kiitwacho  "Hadithi ya Ahikar." (Kinajulikana pia kama "Methali za Ahiqar.")
Mwanangu, mguu wa kondoo katika mkono wako mwenyewe ni bora kuliko bega zima katika mkono wa mwengine; Afadhali kondoo mdogo aliye karibu na wee kuliko ng'ombe aliye mbali; Afadhali shomoro aliyeshikwa mkononi kuliko ndege elfu warukao angani; vazi ulilo nalo ni afadhali kuliko vazi la zambarau usiloliona.
- Hadithi ya Ahikar (ukurasa wa 110)
Kitabu hiki kinasimulia hadithi ya mshauri wa wafalme wa kale wa Ashuru na Misri. Inadhaniwa kuwa hadithi hii ilitungwa takribani 600 KK, na kuna nakala iliyochapishwa mwaka wa 500 KK. 

Methali karibu na hii kutoka nchi mbalimbali:
French:
Un tiens vaut mieux que deux tu l'auras
'Shika-hii-hapa" moja ina thamana kuliko 'nitakuletea-baadaye' mbili
Japanese
明日の百より今日の五十
Hamsini leo ni bora kuliko mia kesho
Italian
Meglio un uovo oggi che una gallina domani
Bora yai leo kuliko kuku kesho

Mnaonaje -- methali hii ni ushauri mzuri? Ni bora kuridhika na kitu kinachopatikana kwa hakika, ama kutafuta kitu bora zaidi kisicho na hakika?
...
Updated 5mo ago
by