We support the Pickleball community in Arusha, Tanzania
Play pickleball Learn more
Book a court Learn pickleball for FREE Hire a Pickleball coach
Posts / Proverbs Proverb of the day
SW

Kalamu hushinda jambia

CC BY Unaruhusiwa kunakili & kusambaza mchoro huu na makala hii bila idhini, ukitaja tu chanzo (www.maktaba.org)

Ufafanuzi


Methali hii ya Kiingereza inatafsirika pia kama "Kalamu ina nguvu kuliko upanga au jambia" au " Kalamu ni kali kuliko upanga." Katika methali hii, jambia au upanga unaashiria nguvu na ukatili, na maana ya kalamu ni maneno. Ingawa upanga unaweza kushinda kwa nguvu, kalamu inaweza kuwashawishi, kuwahamasisha, na kuwaelimisha watu. Sio kila mtu ana silaha za kuwalazimisha watu wengine kufanya kile anachotaka, lakini kila mtu ana uwezo wa kubadilisha ulimwengu kupitia kile anachofikiria, kusema na kuandika kwa maneno. 

Silaha za siku hizi ni kalamu na karatasi.
 - Methali ya Kiswahili

Methali hii ni kweli kwa sababu mara nyingi maneno huchochea na kudhibiti jinsi watu wanavyotumia nguvu na silaha zao. Kwa mfano, kupitia sheria, maneno ya viongozi, mahakimu na majaji yana uwezo wa kuwafunga watu gerezani au hata kuwaua. Kutoa hotuba ya moto kwa umati wa watu wenye hasira kunaweza kuleta ghasia kali na madhara mengine (ona Juliasi Kaizari).

"Ukinipa picha, nitakupa vita."
- William Randolph Hearst
(Mwandishi wa habari na mchapishaji wa magazeti, Marekani)

Lakini pia, methali hiyo inatukumbusha nguvu ya upinzani usio na vurugu kwenye kuleta mabadiliko ya kudumu, kanuni iliyotetewa na kuonyeshwa na watu kama Mahatma Gandhi, Martin Luther King, na Nelson Mandela.  Angalia pia: Insha ya "Civil Disobedience"  na Henry David Thoreau, pamoja na Tamthilia mashuhuri ya "Antigone" na Sophocles.

Chimbuko


Nukuu hii ya "kalamu ina nguvu kuliko upanga" ilipata umaarufu kupitia tamthilia ya "Richelieu: au The Conspiracy"  na Edward Bulwer-Lytton (mwaka wa 1839, ukurasa wa 47). Lakini hakika wazo lilikuwepo kabla.

Wengine wanasema chimbuko halisi la methali hii ni Hadithi ya Ahikar. Kitabu hiki kiliandikwa takriban miaka 600 kabla ya kristu, na ni chimbuko la methali zingine kama "Ndege mkononi ana thamani ya wawili mtini"). Katika toleo letu, mfasiri hakuweza kusoma maandishi kutokana na hali ya karatasi, na maneno yalikatika. (Ukurasa 171/274
Dhibiti kinywa chako kwa uangalifu ...[ILIKATA]... na ufanye moyo wako kuwa mzito(?), kwa maana neno linalosemwa ni kama ndege, naye alitamkaye ni kama mtu asiye na  ...[ILIKATA]... ufundi wa maneno una nguvu zaidi kuliko ufundi wa  ...[ILIKATA]...
- Hadithi ya Ahikar, Ukurasa wa 171/274
Je, hili ndilo chimbuko halisi la methali hii, miaka zaidi ya 2,500 iliyopita? Muwe majaji...

Chanzo karibu na methali hii pia kinaonekana katika Agano la Kale:
Kwa maana neno la Mungu ni hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili.
Waebrania 4:12, Biblia

Na vilevile katika Shakespeare: 
Wengi wanaovaa panga huogopa kalamu.
-William Shakespeare
Tamthilia ya Hamlet, Sehemu ya 2, Onyesho la II (ukurasa wa 59)

 Je, unakubali kalamu hushinda jambia? Toa maoni yako hapo chini!
Play Tennis or Pickleball in Arusha, Tanzania

Your reservations contribute to supporting:

for kids, teens and adults in Arusha, Tanzania

and the maintenance and upkeep of the courts.

We recently built 3 new lighted pickleball courts in Arusha, Tanzania!

Support fitness, sports and education in East Africa

Help us support great programs in East Africa