We support Pickleball and Tennis in Arusha, Tanzania
Play tennis Learn more
Book a court Hire a tennis coach in Arusha
Makala / Methali Methali ya Leo
SW

Kiburi hutangulia anguko

Mchoro na Caspar David Friedrich, mwaka wa 1817, "Wanderer above the Sea of Fog / Der Wanderer über dem Nebelmeer / Msafiri Juu ya Bahari ya Ukungu"
Methali ya leo, (Kiburi hutangulia anguko au kiburi huja kabla ya kuanguka) maana yake ni watu wenya kiburi sana wanaweza kufeli haraka. Mafanikio huleta kiburi, na kiburi hutupeleka kupuuza mambo muhimu. Pia ukijiamini sana, ni rahisi kukosa. Kiburi (au ego/ubinafsi) inaweza kutufanya tusione ukomo wa uwezo wetu wala uhalisia wa hali yetu.

Lakini kwa upande mwengine, katika dunia ya kisasa, watu wengi wanathamini zaidi fadhili za kujiamini na kujivunia. Ju kuna utofauti gani kati ya kujiamini (kitu kizuri) na kiburi (kitu kibaya). Toeni maoni, nawaomba!

Methali hii huhusishwa nna hadithi ya Ikarus, kutoka Ugiriki wa kale. (Someni kitabu chetu kipya chenye michoro, "Usiruke Karibu Sana na Jua").  Ikarus alipewa mabawa na baba yake, Daedalus. Mabawa hayo yalitengenezwa na manyoya na nta.  Daedalus akamwambia mwanake asiruke karibu sana na jua, lakini Ikarus alipuuza ushauri wa baba yake, akiruka juu sana, kwa kiburi. Jua liliyeyusha nta, na Ikarus akaanguka baharini na kuzama.

Titanic (Meli) ilijengwa kuanzia 1909. Kabla ya safari ya kwanza,  Phillip Franklin, mkuu wa kampuni aliandika:
There is no danger that Titanic will sink. The boat is unsinkable.
Hakuna hatari ya Titanic kuzama. Meli hii haizamiki.
Kwa sababu ya kiburi chao, hawakuwa na mashua (lifeboats) za kutosha kwa abiria wote, kwa ajili ya dharura. Mwaka wa 1912, Titanic ilizama, pamoja na watu zaidi ya 1500 waliofariki.

Katika fasihi, mashujaa wengi wa trajedy wanashushwa na majivuno na kiburi. Kwa mfano, katika kitabu cha Mflame Lear (na Shakespeare), kiburi cha mfalme kilimfanya awe katika hatari ya kubembelezwa, na uamuzi wake mbaya ukamgharimu kile alicho nacho. Kiburi cha Juliasi Kaizari kilimpeleka kusisitiza kwenda bungeni akipuuza maonyo mengi kwamba angeuawa. Vilevile, Oedipus (Mfalme Edipode) alijivunia sana, na hakusikiliza wengine waliomshauri, asitafute ukweli kuhusu wazazi wake.

Methali ya leo inatoka katika kitabu cha Mithali katika Biblia.
Kiburi hutangulia kabla ya uharibifu
na moyo wa kujivuna kabla ya maangamizi. 

Korani pia ina aya nyingi juu ya kiburi, kwa mfano:
ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ مُخْتَالًا فَخُورًا 
Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri
Surah An-Nisa - 36

Hapa kuna baadhi ya mithali kutoka nchi mbalimbali juu ya kanuni hiyo hiyo.
Kifaransa:
Qui fait le malin tombe dans le ravin
Mwerevu huanguka kwenye bonde
Kirusi:
Сатана гордился, с неба свалился; фараон гордился, в море утопился; а мы гордимся - куда годимся?
Shetani alikuwa na kiburi, akaanguka kutoka mbinguni; Firauni alikuwa na kiburi, akazama baharini; na tunajivunia - tunafaa wapi?
Kiingereza:
The bigger they come, the harder they fall.
Kadiri wanavyokuwa wakubwa, ndivyo wanavyozidi kuanguka.
Play Tennis or Pickleball in Arusha, Tanzania

Your reservations contribute to supporting:

for kids, teens and adults in Arusha, Tanzania

and the maintenance and upkeep of the courts.

We recently built 3 new lighted pickleball courts in Arusha, Tanzania!

Support fitness, sports and education in East Africa

Help us support great programs in East Africa