You need to login to view profiles OR to update your profile

Create a new account

Sign up for news and free books by email!
New announcements
Discussions
Proverbs
Mchumia juani, hulia kivulini
Join
or login
to VOTE
Votes
59
View this proverb in English
Work in the sun, eat in the shade
na Magreth Lazaro Mafie 🇹🇿
🏆 Shindano la Insha ya Methali 
🥉 Mshindi wa Tatu
Ni mara ngapi umesikia Mchumia juani hulia kivulini? Hii ni methali ya kiswahili (kibantu) yenye maana ya kuwatia moyo watu katika shughuli mbalimbali wanazozifanya Kila siku wawe na Imani kuwa ipo siku watayafurahia matunda ya kazi yao. 

Methali hii huwapa watu nguvu, bidii, moyo, ujasiri, tumaini na weledi katika kufanya kazi. Mfanyakazi huamini kuwa baada ya kazi ngumu zenye surubu basi huleta mavuno mazuri yenye kumfanya astareheke kivulini akila matunda ya kazi yake. Shairi lifuatalo linaonesha kwa namna gani mchumia juani huwa katika majukumu ya Kila siku.

Siogopi jua wala mvua, nikiitengeneza kesho yangu
Siogopi maumivu Wala majeraha, maana yote ni ya muda
Jua kali na kazi ndiyo desturi yangu, ili kheri kuja maishani
Machinga,mkulima, makuli na mvuvi wao na jua, Ili kuitafuta kesho
Mchumia juani, hulia kivulini bado nakitafuta kivuli.
Ni mchana jua la utosi, kichwani nina mavuno, jasho linatiririka
Jua limezama Sasa kasia ufukweni, hoi kitandani, nyavu zi baharini
Nyumbani mtaa wa nne, nahodha wa familia surubu nivute  kheri
Jua Sasa la chomoza, Kiguu na njia kulitafuta tonge
Mchumia juani, hulia kivulini bado nakitafuta kivuli.

Bwana mmoja alikuwa mkulima. Maisha yake yote alitumia katika kilimo. Hivyo kupendeza kwake kulikuwa mara chache. Watu kijijini kwake walimuita mkulima stadi. Alijenga nyumba kwa kuuza sehemu ya mazao yake, alisomesha wanae kwa kilimo.

Bwana huyu alikuwa mtu mwenye bidii alijifunza siku zote kanuni za mkulima bora, hivyo kadri muda unavyokwenda mashamba yake alivuna mazao mengi. Watu wengi walistaajabu sana kuona mabadiliko makubwa ndani ya familia yake. Aliwekeza vitu vingi kijijini kwake, mashamba, nyumba, maduka na mifugo mingi vilitoka shambani.

Watu wengi walikuja kujichukulia hekima kwa mkulima stadi. Siku zote aliwaambia "Mchumia juani, hulia kivulini. Jembe limeniheshimisha kijijini Mimi na familia yangu. Maisha yangu sasa yanakwenda barabara kwa hakika niko kivulini nafurahia matunda ya kazi yangu ya juani. Mimi leo kijana wa mkulima huyo stadi najivunia malezi, uwajibikaji wake kwa sababu kazi za juani leo zimetufanya tupumzike na kula kivulini. Kwa hakika maana ya mchumia juani inaonekana kwa vitendo. Bidii yako ndilo jua lako na kivuli ndiyo matunda ya bidii yako.

Hadithi hii inashibishwa na hadithi ilee ya "Mabala the Farmer" yaani Mabala Mkulima iliyoandikwa na Richard S. Mabala(1989). 

Mabala alikuwa mfanyakazi bandarini Kisha akapunguzwa hivyo akachagua kurudi kijijini Morogoro. Mabala alikuwa mzembe,mlevi na mbishi. Mabala alikwenda shambani na galoni ya pombe alikunywa na kulala, alipoamka alimwongelesha mkewe lakni hakujibiwa zaidi ya  sauti ya jembe tik-tok, tik-tok .

Mabala alikuwa mbishi, alimwagilia sukari shambani alifikiri ni mbolea, lakni mwisho alibadilika na kuwa mkulima stadi akawa mchumia juani ili familia yake ije kulia kivulini. Je wewe unahisi Mabala ni mchumia juani? Ndani ya familia au kwenye jamii mkulima stadi anakupa picha gani?

Mwisho hadithi hii kutoka katika methali ya mchumia juani hulia kivulini hutuonyesha dira njema katika kila tunachokifanya katika maisha ya kila siku. Huku methali kama Subira yavuta kheri, Mgaa na Upwa hali wali mkavu zote hufanana kimaudhui, zipo katika kuipa jamii nguvu na matumaini kwa kila jambo lifanyikalo katika malengo.
Sources

Juu ya Insha hii

Insha hii ilishinda nafasi ya tatu 🥉 katika Shindano la Methali ya Insha la Maktaba.org 🏆 7/7/2023
Magreth Lazaro Mafie ni mwanafunzi Mtanzania 🇹🇿 

Hakimiliki

Creative Commons Attribution (CC BY 4.0)
na Magreth Lazaro Mafie
Ilichapishwa na Maktaba.org
Mchoro/Image: CC BY Maktaba.org

The original essay included the following image, which is not included in the Creative Commons license.
Mchoro huu na / This image from: Honey Bee Arts - YouTube


Loading...
Loading...
Login to view and post comments
Kila kazi kubwa katika maisha huhitaji kufanyika kwa hatua ndogo, siku baada ya siku. 

Je, unajua methali zingine zinazofanana na hii au zinazotoa dhana hiyohiyo? 

Msemo huu unakumbusha shairi liitwalo "Vitu Vidogo" na Julia Abigail Fletcher Carney: 
Matone madogo ya maji,
Chembe kidogo za mchanga, 
hutengeneza bahari kubwa
Na ardhi ya kupendeza

Vivyo hivyo zile dakika ndogo,
ingawa ni ndogo,
hutengeneza enzi za milele. 
Julia Carney alitunga shairi hili mwaka wa 1845 darasani akiwa mwanafunzi darasani -- na alipewa dakika 10 tu kuliandika!
...
Updated 4mo ago
by
Many people are afraid to ask questions because they don't want to be seen as stupid. But asking questions is the best way to learn from others.

Asking questions also helps others around you. Have you ever hesitated to ask a question because you thought others already understood... but later you realized they didn't either? 

This proverb is similar to the English saying, “There's no such thing as a stupid question.”
...
Updated 4mo ago
by
Kadiri hamu ya kula inavyoongezeka, chakula kina ladha bora.

Methali hiyo ilionekana kwa mara ya kwanza katika kitabu cha Miguel de Cervantes Don Quixote, kilichochapishwa mwaka wa 1615 (katika Sehemu ya II, Sura ya V)

Mara nyingi wazazi husema hivi kwa watoto wao wanapokuwa walaji kwa fujo.
...
Updated 4mo ago
by
Huwa tunatendewa kama tunavyowatendea wengine. Kwa kawaida methali hii hutumika kama onyo, au wakati mtu mbaya anapata alichostahili. Lakini pia inaweza kutumika kama tumaini la baraka kwa wale wanaofanya mema. Chimbuko halisi cha methali hiyo haijulikani, lakini ilianza Amerika miaka za 60 hivi. Inaendana na kanuni la Karma katika dini ya Kihindi.

Methali na nukuu zinazohusiana:
Shakespeare
Bado tunayo hukumu hapa (duniani);
Tunafundisha tu umwagaji damu, ambayo, ukifundishwa, hurudi
ili lipiza kisasi na kumtesa mvumbuzi: mkono wa haki
huweka viungo vya kikombe chetu cha sumu
Kwa midomo yetu wenyewe.  ( Makbeth Act I, Scene 7 )
Biblia:
Chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna ( Wagalatia 6:7 )
Kichina: 
善有善報,惡有惡報
Wema hulipwa kwa wema, na ubaya kwa ubaya. 
Kijerumani:
Wie man in den Wald hineinruft, so schallt es heraus
Unacholia msituni, kitasikika tena
...
Updated 4mo ago
by