We support Pickleball and Tennis in Arusha, Tanzania
Play tennis Learn more
Book a court Hire a tennis coach
Posts / Proverbs Proverb of the day
SW

Maji yaliyotulia ndiyo yenye kina kirefu

na Nankya Sauda 🇺🇬
Shindano la Insha ya Methali 🏆
Mshindi wa Kwanza 🥇

Maji yaliyotulia ndiyo yenye kina kirefu

Umewahi kuchukua muda na kujiuliza kwa nini wazee huwa wana busara zaidi kuliko vijana? Je, umewahi kuchukua muda wa kutafakari asili yako ulipochipuka? Ikiwa sivyo, [sasa] ni wakati mzuri wa kuanza kutafuta asili yako kwa sababu ni muhimu mtu ajue mizizi yake.
   Baada ya muda, unachukua mzigo wa kufunua asili ya watu mashuhuri wenye akili na haiba zao, utakuja kutambua kwamba wao ni introverts (yaani wakimya, wanaopenda kukaa peke yao/kujitenga) lakini ni mashuhuri. Ni muhimu uchukue muda wako, hata ukiwa bize, ujifunze kuhusu wasomi mashuhuri kama Albert Einstein, mwanasayansi mashuhuri ambaye alisema nukuu inayotuelimisha:
"Maisha tulivu ya upweke yasiobadilikaa huchochea akili na fikra bunifu."

Hii inamaanisha kwamba wakati ukiwa peke yako ni nafasi ya kujitafakari, lakini pia ni nafasi ya kutumia akili yako bunifu. Wanasema wazungumzaji wakubwa ni wanasheria wazuri, na tumeona hayo katika maisha yetu ya kila siku ambapo watu hutoa ahadi tupu, hutoa matamko ya uwongo ili kuwapendeza waliomzunguka bila kuchukua muda wa kufanya kitu kwa nia ya kutekeleza maneno yao. Kwa sababu hiyo, wengi wamepoteza imani na hawa wanaoitwa “wazungumzaji wakubwa.”
   Kwa upande mwingine, wakimya hutushangaza kwa matendo yao. Hatua zao hupangiliwa kila mara, matamanio yao ni wazi na vitendo vyao hufanyika kwa kusudi. Wapenzi wakimya hukuza mahusiano yao ya kimapenzi kwa ubunifu mpya ili kudumisha mahusiano. Waliowaajiri [wakimya] na waliokaa karibu na introverts husema kuwafahamu ni moja ya mafanikio makubwa katika maisha yao, ndo maana hawa wamefanya kazi nadhifu zaidi, wakawa na vipindi vyao vya kutafakari peke yao, na hatimaye walitoa kazi bora na kupata cheo kikubwa.
   Tunaweza kufafanua methali kama misemo inatumika katika nchi au utamaduni fulani. Ni maneno mafupi yenye busara na hutoa ushauri na vile vile kuongeza wazo kuhusiana na maisha ya kila siku. Kwa kweli, ili kufahamu kwa kina mila na desturi za kitamaduni, ni vizuri warejelee methali kwani zinaweza kuwa na maana pana ndani. 
Kihistoria, methali "Still waters run deep" (Maji yalotulia ndo yenye kina kirefu/Usicheze maji yanayosimama) inatoka Kilatini cha kale. Ilipata umaarufu baada ya Shakespeare kuitumia katika tamthilia yake ya Henry VI mwaka 1590. Alisema:
"Maji hutulia pale ambapo mto una kina kirefu."

Tunatambua kwamba, mara nyingi watu hatari zaidi walio na roho mbaya hupanga hatua zao na kuchukua hatua kwa wakati ambao wengine hatarajii. Ndio maana usaliti hutoka kwa watu ambao hatutarajii [kitu kama hicho] kutoka kwao. Kwa hiyo ni muhimu kwa mtu kuchukua si tu yale yanayokutana na macho bali pia kuchukua tahadhari hasa kutoka kwa watu ambao hawalipizi kisasi mara tu baada ya kukasirishwa au kukabiliwa.
   Albert Einstein licha ya tabia yake ya kujittenga, yeye anajulikana sana kwa kubuni nadharia yake ya relativity ambayo ilileta mapinduzi katika uelewa wetu wa nafasi ya nje, wakati, na kanimvutano (gravity).
   Kwa kumalizia, ni muhimu sana kutofikia hitimisho [haraka] kwa sababu sura hudanganya na kuna mengi ya kujua na kugundua kuliko macho yanavyoweza kuona.
Play Tennis or Pickleball in Arusha, Tanzania

Your reservations contribute to supporting:

for kids, teens and adults in Arusha, Tanzania

and the maintenance and upkeep of the courts.

We recently built 3 new lighted pickleball courts in Arusha, Tanzania!

Support fitness, sports and education in East Africa

Help us support great programs in East Africa