We support Pickleball and Tennis in Arusha, Tanzania
Play tennis Learn more
Book a court Hire a tennis coach
Posts / Proverbs Proverb of the day
SW

Bora kuchelewa kuliko kukosa kabisa

Fikiria kama umechelewa Mahojiano ya Ajira. Ungefanyaje? Next time unapofikiri "Nimeshachelewa" jiambie "Bora kuchelewa kuliko kukosa kabisa." Kwa mfano makala hii ya Methali ya Siku ilichelewa, lakini sasa unaisoma - Asante!
Siku moja, mfanyabiashara mashuhuri alitafuta msaidizi. Alipokea maombi na CV za watu wengi sana, lakini wawili tu walikidhi vigezo: Amina na Baraka. Ili kuamua kati yao, aliwaita wote wawili, na akawaalika waje kwaajili ya mahojiano ya ajira, kesho yake asubuhi. "Saa tatu kamili -- vaa mavazi ya kazi, na usichelewe!" Akawaonya.

Kesho yake Ali aliwahi kuamka, akavaa suti yake nzuri, na alipanda basi kijijini kwake saa 2. "Bora kinga kuliko tiba" alifikiria. Njiani kuelekea mjini, basi ilianza kutoa moshi. Abira wote walishuka na waliachwa porini. Hapo hapo mvua ilianza kunyesha. Kila basi lililompita, Ali akaomba nafasi, lakini, kutokana na hali ya hewa, mabasi yote yalikuwa yameshajaa. Kwa hivyo ikabidi atembee kwa miguu. Ilipotimia saa tatu, bado Ali alikuwa mbali na mji, na mvua ikawa kali zaidi na zaidi. "Lazima niendelee" akajiambia, "Bora kuchelewa kuliko kukosa kabisa."

Wakati huohuo mjini, Baraka aliamka ghorofani kwake, na akashtuka ghafla akiona jua lilikuwa limeshafika mbali angani. "Aisee! Niliweka alarm! Simu yangu ina shida gani sasa?" Alitazama saa ukutani: Saa tatu kamili. "Bora niache tu. Hata nikiondoka saivi, bado nitachelewa kufika. Si alisema usichelewe? Hatamwajiri aliyechelewa." Kwa hivyo Baraka, akiwa na huzuni, akalala tena.

Saa nne na nusu, hatimaye, Ali alifika ofisini kwa mfanyabiashara na kugonga mlango, suti yake ikichuruzika maji na matope sakafuni. Mfanyabiashara akajibu. "Si nilikwambia vaa mavazi yanayofaa na usichelewe? Sasa umechelewa zaidi ya saa limoja na mavazi yako yamechafuka. Niambie nitawezaje kukuajiri baada ya hapo?" Kisha Ali akaeleza yote yaliyomtokea. Mfanyabishara akamjibu "Nimejifunza mengi kuhusu wewe kutoka kwa hadithi yako Ali. Ukiwa na kusudi kichwani, utafanya kazi kwa bidii, na pale unapokutana na vikwazo hukati tamaa, hata kama umechelewa. Nakwambia, wewe ndiye wa kwanza kufika leo. Mwingine alikosa kabisa. Nitakuajiri wewe."

Mafanikio makubwa huanza na makosa mengi, lakini baada ya muda, uvumilivu na ustahilimilu huleta matunda. Kukosa ni uanadamu, lakini Mungu ni mvumilivu sana kwetu. Anatupa nafasi nyingi za kujifunza na kujaribu tena, ilimradi tusikate tamaa.

Wengine wanasema methali ya "Better late than never never" inatoka kwa kitabu cha The Canterbury Tales, kilichoandikwa na Chaucer miaka ya 1390.
Better than never is late
“Bora kuliko kamwe ni kuchelewa
-The Canterbury Tales, The Canon's Yeoman's Tale
Wengine wanasema chimbuko la kweli ni kitabu cha Historia ya Roma, kilichoandikwa na Livy takriban mwaka wa 20 KK.
Lilatini: potiusque sero quam numquam
Bora kuchelewa kuliko kukosa kabisa
- History of Rome, Book 4

Methali ya Kiingereza inayoendana ni:
It's never too late
Hakuna kuchelewa
 Methali ya Kiingereza inayopinga:
Don't close the gate after the horse has bolted.
Usifunge mlango baada ya farasi kukimbia

Methali ya Kihindi: 
जब जाति तब सवेरे
Wakati wowote unapoamka, ndo asubuhi yako

Play Tennis or Pickleball in Arusha, Tanzania

Your reservations contribute to supporting:

for kids, teens and adults in Arusha, Tanzania

and the maintenance and upkeep of the courts.

We recently built 3 new lighted pickleball courts in Arusha, Tanzania!

Are you traveling to Tanzania?

Learn Useful Phrases in English & Swahili

Master essential everyday phrases in both languages