Ustawi wa kiuchumi huenea na huwafikia raia wote wa nchi au eneo. Nchi haiwezi kufaidika bila raia wake wote kufaidika kwa namna moja au nyingine, kama vile baharini, maji yakijaa boti zote zitapanda, wimbi linalokuja litainua boti zote ziwe mitumbwi, jahazi, meli au mashua.
Msemo huo hutumiwa kumaanisha makundi yote yalinufaika kutokana na mabadiliko ya hali, hasa utitiri wa rasilimali, hata kama inaonekana kama zinawafikia matajiri wachache pekee. Nimesikia wafanyakazi wakiona wenzao wamepokea bonasi au kamisheni kubwa wanasema, "A rising tide lists all boats," ikimaanisha mauzo yakipanda, mapato ya kampuni yataongezeka na fursa kwa kampuni, na kwa hivyo, kwa wafanyikazi wote pia. Katika kesi hii, ni wazi wimbi halizinui boti zote kwa usawa au kiasi kilekile.
Wakosoaji wa methali hii wanaweza kulalamika kwamba methali hii inatumika pia ili kuhalalisha mpango au makubaliano yoyote hata kama yatawanufaisha wachache tu. Lakini kwa kawaida msemo huo husemwa na viongozi kwa matumaini au kama pongezi.
Methali hiyo mara nyingi huhusishwa na John F. Kennedy rais wa Marekani, ambaye aliiitumia katika hotuba yake, mwaka wa 1963 akijitetea baada ya baada ya kukosolewa juu ya ujenzi wa bwawa ulitumia pesa nyingi sana (matumizi ya fujo). Mwandishi wa hotuba za Kennedy (aliyeitwa Ted Sorensen) alifichua kwamba Rais Kennedy alitumia methali hii baada ya kuisoma katika jarida la "New England Council."
Msemo karibu na huu ni "to grow the pie" yaani "kukuza keki" ambayo inamaanisha, kama keki ni kubwa zaidi, washiriki wote watapata keki zaidi hata kama uwiano/asilimia haibadiliki.
Je, unakubali kwamba ustawi mpana wa kiuchumi huwafikia wote?