Mchapishaji Raising Voices
Hili chapisho ni kwa ajili ya mtu yeyote mwenye ushawishi kuhusu watoto wanavyopata elimu katika shule zetu. Linajaribu kuwafikia watawala wa shule, waalimu, watungasera na wanaharakati wanaotambua mahitaji ya kuboresha jinsi tunavyotoa elimu. Linalenga
kuwafahamisha na kuwahamasisha wale watu wanaotambua shule kama sehemu yetu ya matumaini, ya uwekezaji wetu wa baadaye na ahadi/wajibu wetu kwa watoto leo. Kwa kifupi, chapisho hili linazungumza na kila mmoja mwenye wajibu katika kubuni shule bora.
Chapisho hili ni mjadala wa mawazo na siyo mwongozo wa utekelezaji. Linawasilisha hoja na michango inayohitaji kufikiriwa sasa wakati tunatengeneza mustakabali. Kama mdau mwenye maslahi na mwenye ushawishi, maamuzi yako yanaweza kuathiri jinsi shule zetu zitakavyoendelea katika miaka ijayo. Kwahiyo hili chapisho linawasilisha mitazamo na taarifa inayoweza kusaidia kufikri na kuchagua.
Matumaini yetu ni kwamba, jinsi unavyosoma hili chapisho, utauliza maswali ya kina zaidi kuhusu jinsi tunavyotoa elimu na itakavyoweza kuwa tofauti na bora. Kwa kuwekeza ushawishi wako, rasilimali na ubunifu katika kutekeleza baadhi ya mawazo yafuatayo unaweza kuathiri
kwa kiasi kikubwa sana maisha ya watoto wengi – pamoja na maisha yatakayoguswa na maamuzi yatakayofanywa na watoto hawa pale watakapokuwa viongozi wetu baadaye.
Chapisho hili huzungumza na kila mmoja mwenye jukumu katika ujenzi wa shule bora.
...