Elimu ni moja ya sekta muhimu zaidi ya maendeleo. Kijitabu hiki kinaelezea misingi mikuu ya kuongoza kamati za shule na wajumbe wake. Lengo ni kusaidia jitihada za Serikali kuimarisha kamati za shule na kupanua njia ambazo wananchi wanaweza kuchangia kuboresha elimu.
Misingi ya ushiriki katika kamati za shule ni haki za binadamu, ushiriki, uwajibikaji, uwazi na demokrasia. Ni muhimu kwa kila kamati ya shule kuijadili na kuielewa vyema misingi hii ili kuwa na ufanisi zaidi. Naamini kwamba kwa kuzingatia misingi hiyo kamati zitajenga imani kwa wananchi zinaowawakilisha.
Walengwa wakuu wa kijitabu hiki ni kamati za shule za msingi, viongozi wa mitaa na vijiji na shule za msingi. Tunategemea viongozi wa Serikali katika ngazi za mikoa na wilaya kote nchini watafanya jitihada za kuhakikisha kijitabu hiki kinasambazwa na kuwafikia walengwa wote
...