You are now browsing in Swahili. Switch to English
In Swahili: "Sasa unavinjari kwa Kiswahili. Rudi kwa Kiingereza"
Lazime uingie akaunti ili kubadilisha wasifu wako au kuona wasifu wa wengine

Fungua akaunti mpya

Taarifa
Majadiliano
Methali

Asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu

Ili kupiga KURA kwa Methali ya Mwezi
Kura
0
Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by

Swali: Je, umejifunza zaidi kutoka kwa wazazi wako ama kupitia uzoefu wako ulimwenguni?


Methali hii hutumika wakati mtu amekosa na kupata madhara, haswa kama ameonywa... kama vile dereva wa lori katika picha hii (kutoka Oxfordshire, Uingereza). Bila kujali kama ulifunzwa na wazazi, hatimaye lazima ukabiliane na ukweli wa maisha halisi. Ona pia: Mtoto akilia wembe, mpe

Kuna shairi lililotungwa na Akilimali Snow-White juu ya methali hii:

ASOFUNZWA NA WAZAZI, HUFUNZWA NA ULIMWENGU
na Akilimali Snow-White

Zama walinipumbaza, wazee kwa kunilea,
Nikashindwa kujifunza, myendo mipya ya dunia,
Leo najipendekeza, kwa walimwengu sikia,
Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.

Kazi zote singeweza, bila kuwanyenyekea,
Kutii kuwembeleza, kisha kuwatumikia,
Hata nikawapendeza, wakanifunza kwa nia,
Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.

Sasa kusema naweza, Kizungu bila udhia,
Kama vile Kingereza, na lugha zingine pia,
Kwa juhudi najifunza, hata zimenielea,
Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.

Naweza kuzungumza, pasipo kutia doa,
Na paovu kuongoza, doa nikaliondoa,
Mwishowe pakapendeza, lingano moja hatua,
Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.

Sina nilipopasaza, pasina kupachungua,
Pande zote hachunguza, marifa nikachukuwa,
Hata najua kuuza, bidhaa na kununua,
Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.

Kiasi nilo jifunza, si haba kwa kubabia,
Nitokapo napendeza, kazi njema natumia,
Ni vigumu kuibeza, jinsi inanielea,
Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.

Haifai kupuuza, kwa kitu usicho jua,
Jaribu kupeleleza, na kisha ukichungua,
Nia unap,o ikaza, hushindwi kitu kujua,
Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.

Kazi nilizojifunza, babangu hakuzijua,
Hakujua Kingereza, kuuza na kununua,
Bali kujipendekeza, ndipo mwana nikajua,
Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.

Nawatilia nyongeza, mlio nisaidia,
Nyote mlionifunza, Rabi awape afia,
Mungu heri tawajaza, mema kuwarudishia,
Asofunzwa na wazazi, hufunzwa na walimwengu.

- Diwani ya Akilimali

Fikeni E. M. K. Senkoro (1988) aliandika juu ya shairi hili:
[M]tu hawezi kupata uzoefu wa mambo yote yahusuyo maisha kutoka kwa wazazi wake: lazima awe tayari kufunzwa na ulimwengu, yaani kujifunza kutoka kwa wengine zaidi ya baba na mama yake. 

Nimejitahidi kutafsiri shairi hili kwa Kiingereza, na nitashukuru sana sana kupata feedback zenu, ndugu wajuaji wa Kiswahili na Kiingereza. (Someni hapa.)

Mnafikiriaje? Shairi hili lina maana gani kwako? 
Marejeleo
Picha ni kweli, inaonyesha ajali iliyotokea Uingereza, mkoa wa Oxfordshire, (Pich kutoka mitandao ya kijamii) - Soma pia Makala hii ya BBC

Shairi lilitoka Diwani ya Akilimali

Nukuu ya mwisho inatoka kitabu cha "Ushairi - Nadharia na Tahakiki" na F.E.M.K. Senkoro, Sura ya 7 (Dar Es Salaam University Press, 1988, ISBN 9976 60 0224)  
Loading...
Loading...
Ingia akaunti yako ili kuona na kutoa maoni
Maana yake, afadhali kuridhika na ulicho nacho, badala ya kuiweka hatarini kwa ajili ya kupata kitu kubwa zaidi.

 Methali hii ni ya zamani sana. Chanzo cha methali hii ni kitabu cha kale kiitwacho  "Hadithi ya Ahikar." (Kinajulikana pia kama "Methali za Ahiqar.")
Mwanangu, mguu wa kondoo katika mkono wako mwenyewe ni bora kuliko bega zima katika mkono wa mwengine; Afadhali kondoo mdogo aliye karibu na wee kuliko ng'ombe aliye mbali; Afadhali shomoro aliyeshikwa mkononi kuliko ndege elfu warukao angani; vazi ulilo nalo ni afadhali kuliko vazi la zambarau usiloliona.
- Hadithi ya Ahikar (ukurasa wa 110)
Kitabu hiki kinasimulia hadithi ya mshauri wa wafalme wa kale wa Ashuru na Misri. Inadhaniwa kuwa hadithi hii ilitungwa takribani 600 KK, na kuna nakala iliyochapishwa mwaka wa 500 KK. 

Methali karibu na hii kutoka nchi mbalimbali:
French:
Un tiens vaut mieux que deux tu l'auras
'Shika-hii-hapa" moja ina thamana kuliko 'nitakuletea-baadaye' mbili
Japanese
明日の百より今日の五十
Hamsini leo ni bora kuliko mia kesho
Italian
Meglio un uovo oggi che una gallina domani
Bora yai leo kuliko kuku kesho

Mnaonaje -- methali hii ni ushauri mzuri? Ni bora kuridhika na kitu kinachopatikana kwa hakika, ama kutafuta kitu bora zaidi kisicho na hakika?
...
Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by
Huwa tunatendewa kama tunavyowatendea wengine. Kwa kawaida methali hii hutumika kama onyo, au wakati mtu mbaya anapata alichostahili. Lakini pia inaweza kutumika kama tumaini la baraka kwa wale wanaofanya mema. Chimbuko halisi cha methali hiyo haijulikani, lakini ilianza Amerika miaka za 60 hivi. Inaendana na kanuni la Karma katika dini ya Kihindi.

Methali na nukuu zinazohusiana:
Shakespeare
Bado tunayo hukumu hapa (duniani);
Tunafundisha tu umwagaji damu, ambayo, ukifundishwa, hurudi
ili lipiza kisasi na kumtesa mvumbuzi: mkono wa haki
huweka viungo vya kikombe chetu cha sumu
Kwa midomo yetu wenyewe.  ( Makbeth Act I, Scene 7 )
Biblia:
Chochote apandacho mtu, ndicho atakachovuna ( Wagalatia 6:7 )
Kichina: 
善有善報,惡有惡報
Wema hulipwa kwa wema, na ubaya kwa ubaya. 
Kijerumani:
Wie man in den Wald hineinruft, so schallt es heraus
Unacholia msituni, kitasikika tena
...
Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by
Ustawi wa kiuchumi huenea na huwafikia raia wote wa nchi au eneo. Nchi haiwezi kufaidika bila raia wake wote kufaidika kwa namna moja au nyingine, kama vile baharini, maji yakijaa boti zote zitapanda, wimbi linalokuja litainua boti zote ziwe mitumbwi, jahazi, meli au mashua.

Msemo huo hutumiwa kumaanisha makundi yote yalinufaika kutokana na mabadiliko ya hali, hasa utitiri wa rasilimali, hata kama inaonekana kama zinawafikia matajiri wachache pekee. Nimesikia wafanyakazi wakiona wenzao wamepokea bonasi au kamisheni kubwa wanasema, "A rising tide lists all boats," ikimaanisha mauzo yakipanda, mapato ya kampuni yataongezeka na fursa kwa kampuni, na kwa hivyo, kwa wafanyikazi wote pia. Katika kesi hii, ni wazi wimbi halizinui boti zote kwa usawa au kiasi kilekile.

Wakosoaji wa methali hii wanaweza kulalamika kwamba methali hii inatumika pia ili kuhalalisha mpango au makubaliano yoyote hata kama yatawanufaisha wachache tu. Lakini kwa kawaida msemo huo husemwa  na viongozi kwa matumaini au kama pongezi.

Methali hiyo mara nyingi huhusishwa na John F. Kennedy rais wa Marekani, ambaye aliiitumia katika hotuba yake, mwaka wa 1963 akijitetea baada ya baada ya kukosolewa juu ya ujenzi wa bwawa ulitumia pesa nyingi sana (matumizi ya fujo). Mwandishi wa hotuba za Kennedy (aliyeitwa Ted Sorensen) alifichua kwamba Rais Kennedy alitumia methali hii baada ya kuisoma katika jarida la "New England Council."

Msemo karibu na huu ni "to grow the pie" yaani "kukuza keki" ambayo inamaanisha, kama keki ni kubwa zaidi, washiriki wote watapata keki zaidi hata kama uwiano/asilimia haibadiliki.

Je, unakubali kwamba ustawi mpana wa kiuchumi huwafikia wote?
...
Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by

Je, una ndoto kubwa?

Ndoto ambayo huwezi kuitimiza peke yako? Labda hata ambayo haiwezi kukamilika katika kizazi kimoja?

Kuna makanisa ya kigothi barani Ulaya ambayo yalichukua zaidi ya miaka 600 -- zaidi ya vizazi 20 -- ili kukamilisha ujenzi!

Ingawa Piramidi kubwa zaidi ya Giza imejengwa kwa kasi (ndani ya kizazi kimoja), ila pia ilichukua makumi ya maelfu ya watu.

Nchini Tanzania, Msikiti Mkuu wa Kilwa Kisiwani ulijengwa katika karne za 11-14, ukajengwa upya baada ya tetemeko la ardhi, na uliendelea kufanyiwa ukarabati hadi karne ya 18. Ulitajwa pia miaka ya 1300 na msafiri Ibn Battuta. (Je ulijua unaweza kuona Kilwa Kisiwani kupitia "ziara ya mtandaoni" yaani 3D Virtual Tour? Ona kiungo chini kwenye "Rasilimali")

Maajabu ya dunia, ya kisasa na ya kale, yalianza kama ndoto kubwa, ndoto ambazo zilichukua vizazi vingi kutimiza. Kila kizazi kiliendeleza kazi ya zamani na pia walitoa mchango wao kwa kubadilisha mipango ya siku zijazo. 

Hivyo bhasi, kama unajaribu kufanya jambo kubwa -- jambo ambalo hakika litabadilisha ulimwengu - usitarajie litafanyika kwa siku moja. Na usijaribu kuijenga peke yako. 

Methali Zinazohusiana:


 Kiswahili:
Ukitaka kwenda haraka, nenda peke yako, ukitaka kwenda mbali, nenda na wenzako

Kifaransa:
Rome ne fu[t] pas faite toute en un jour
Kutoka kitabu cha Li Proverbe au Vilain kilichochapishwa takriban mwaka wa 1190
Kifaransa cha kisasa: Rome ne s'est pas faite en un jour
Maana yake: Roma haikujengwa kwa siku moja

Kichina:
冰凍三尺,非一日之寒
Mita ya barafu sio kwa sababu ya siku moja ya baridi

Kigaelic
Chan ann leis a’ chiad bhuille a thuiteas a’ chraobh
Sio pigo la kwanza linaloangusha mti
...

Picha: Shukran kwa Zamani Project waliounda ziara ya mtandaoni ya Kilwa Kisiwani!

Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by