You need to login to view profiles OR to update your profile

Create a new account

Sign up for news and free books by email!
New announcements
Discussions
Proverbs
Mchumia juani, hulia kivulini
Join
or login
to VOTE
Votes
59
View this proverb in English
Work in the sun, eat in the shade
na Magreth Lazaro Mafie 🇹🇿
🏆 Shindano la Insha ya Methali 
🥉 Mshindi wa Tatu
Ni mara ngapi umesikia Mchumia juani hulia kivulini? Hii ni methali ya kiswahili (kibantu) yenye maana ya kuwatia moyo watu katika shughuli mbalimbali wanazozifanya Kila siku wawe na Imani kuwa ipo siku watayafurahia matunda ya kazi yao. 

Methali hii huwapa watu nguvu, bidii, moyo, ujasiri, tumaini na weledi katika kufanya kazi. Mfanyakazi huamini kuwa baada ya kazi ngumu zenye surubu basi huleta mavuno mazuri yenye kumfanya astareheke kivulini akila matunda ya kazi yake. Shairi lifuatalo linaonesha kwa namna gani mchumia juani huwa katika majukumu ya Kila siku.

Siogopi jua wala mvua, nikiitengeneza kesho yangu
Siogopi maumivu Wala majeraha, maana yote ni ya muda
Jua kali na kazi ndiyo desturi yangu, ili kheri kuja maishani
Machinga,mkulima, makuli na mvuvi wao na jua, Ili kuitafuta kesho
Mchumia juani, hulia kivulini bado nakitafuta kivuli.
Ni mchana jua la utosi, kichwani nina mavuno, jasho linatiririka
Jua limezama Sasa kasia ufukweni, hoi kitandani, nyavu zi baharini
Nyumbani mtaa wa nne, nahodha wa familia surubu nivute  kheri
Jua Sasa la chomoza, Kiguu na njia kulitafuta tonge
Mchumia juani, hulia kivulini bado nakitafuta kivuli.

Bwana mmoja alikuwa mkulima. Maisha yake yote alitumia katika kilimo. Hivyo kupendeza kwake kulikuwa mara chache. Watu kijijini kwake walimuita mkulima stadi. Alijenga nyumba kwa kuuza sehemu ya mazao yake, alisomesha wanae kwa kilimo.

Bwana huyu alikuwa mtu mwenye bidii alijifunza siku zote kanuni za mkulima bora, hivyo kadri muda unavyokwenda mashamba yake alivuna mazao mengi. Watu wengi walistaajabu sana kuona mabadiliko makubwa ndani ya familia yake. Aliwekeza vitu vingi kijijini kwake, mashamba, nyumba, maduka na mifugo mingi vilitoka shambani.

Watu wengi walikuja kujichukulia hekima kwa mkulima stadi. Siku zote aliwaambia "Mchumia juani, hulia kivulini. Jembe limeniheshimisha kijijini Mimi na familia yangu. Maisha yangu sasa yanakwenda barabara kwa hakika niko kivulini nafurahia matunda ya kazi yangu ya juani. Mimi leo kijana wa mkulima huyo stadi najivunia malezi, uwajibikaji wake kwa sababu kazi za juani leo zimetufanya tupumzike na kula kivulini. Kwa hakika maana ya mchumia juani inaonekana kwa vitendo. Bidii yako ndilo jua lako na kivuli ndiyo matunda ya bidii yako.

Hadithi hii inashibishwa na hadithi ilee ya "Mabala the Farmer" yaani Mabala Mkulima iliyoandikwa na Richard S. Mabala(1989). 

Mabala alikuwa mfanyakazi bandarini Kisha akapunguzwa hivyo akachagua kurudi kijijini Morogoro. Mabala alikuwa mzembe,mlevi na mbishi. Mabala alikwenda shambani na galoni ya pombe alikunywa na kulala, alipoamka alimwongelesha mkewe lakni hakujibiwa zaidi ya  sauti ya jembe tik-tok, tik-tok .

Mabala alikuwa mbishi, alimwagilia sukari shambani alifikiri ni mbolea, lakni mwisho alibadilika na kuwa mkulima stadi akawa mchumia juani ili familia yake ije kulia kivulini. Je wewe unahisi Mabala ni mchumia juani? Ndani ya familia au kwenye jamii mkulima stadi anakupa picha gani?

Mwisho hadithi hii kutoka katika methali ya mchumia juani hulia kivulini hutuonyesha dira njema katika kila tunachokifanya katika maisha ya kila siku. Huku methali kama Subira yavuta kheri, Mgaa na Upwa hali wali mkavu zote hufanana kimaudhui, zipo katika kuipa jamii nguvu na matumaini kwa kila jambo lifanyikalo katika malengo.
Sources

Juu ya Insha hii

Insha hii ilishinda nafasi ya tatu 🥉 katika Shindano la Methali ya Insha la Maktaba.org 🏆 7/7/2023
Magreth Lazaro Mafie ni mwanafunzi Mtanzania 🇹🇿 

Hakimiliki

Creative Commons Attribution (CC BY 4.0)
na Magreth Lazaro Mafie
Ilichapishwa na Maktaba.org
Mchoro/Image: CC BY Maktaba.org

The original essay included the following image, which is not included in the Creative Commons license.
Mchoro huu na / This image from: Honey Bee Arts - YouTube


Loading...
Loading...
Login to view and post comments
Tofautisha na linganisha matunda na pipi. Matunda yameiva, yana ladha halisi, yamejaa virutubisho na vitamini -- kweli yanajiuza yenyewe.

Kwa upande mwingine, mfuko wa pipi unalia “nisikilize!”, kwa rangi kali, na kauli mbiu zinazolipuka *BOOM*! Lakini chini au nyuma ya kinachong'aa, tunajua kwa kkweli pipi ni sukari tupu tu yenye rangi na ladha bandia ya matunda.

Kama nyani, binadamu hupenda matunda kwa sababu yanatupatia nishati pamoja na lishe na virutubisho. Pipi hutoa nishati bila lishe halisi (Kalori tupu). Pipi huiga tunda. Usidanganywe!

Kizuri hakihitaji kutangazwa, maana ubora hujieleza yenyewe. Kama wachumi wasemavyo, “demand” inazidi “supply”. Matangazo yanaweza kutuahidi furaha, uzuri, upendo, mali au heshima. Lakini jiulize, je, inawezekana kwa kweli? Coca-Cola sio dawa ya upendo.

Methali hii inatukumbusha thamani ya ubora wa kweli kuliko muonekeano maridadi. Methali hii hutumika wakati msemaji ana mashaka juu ya mtu anayejisifu au kujivunia kupita kiasi.

Tuwe kama kikapu cha matunda: mwazi na mwema. Sifa hizi zitawavuta wengine kwako — angalau wao wanaoelewa kwamba “Chema chajiuza, kibaya chajitembeza!”

Methali zinazohusiana:
Vingaravyo vyote si dhahabu

Don’t judge ya book by it’s cover
Usihukumu kitabu kwa kava yake (muonekeno)

Appearances are deceptive
Maonekano hudanganya
 
高嶺の花
Hana yori dango
Chakula [ni bora] kuliko maua
...
Updated 4mo ago
by
Large tasks in life need to tackled in small steps, day by day. This proverb comes from Swahili:
Haba na haba hujaza kibaba
Little by little fills up the jar

Can you think of other similar proverbs that encourage the same way of thinking? 

This saying reminds be of a poem called "Little Things" by Julia Abigail Fletcher Carney:
Little drops of water,
Little grains of sand,
Make the mighty ocean
And the pleasant land.
     
Thus the little minutes,
Humble though they be,
Make the mighty ages
Of eternity. 
Julia Carney composed this poem in 1845 as a student in class -- and she was given only 10 minutes to write it!
...
Updated 4mo ago
by
Kuna vitu ambavyo huwezi kufanya peke yako. Tango ni mchezo (densi) ya watu wawili, kwa hivyo huwezi kucheza tango peke yako.

Methali hii inatoka wimbo ulioimbwa 1952, It Takes Two to Tango:
Unaweza kusafiri kwa meli peke yako,
kulala au kupumzika peke yako.
Unaweza kuingia kwenye deni peke yako.
Kuna mambo mengi ambayo unaweza kufanya peke yako.
Lakini ni lazima muwe wawili ili kucheza tango, muwe wawili ili kucheza tango...
- It Takes Two to Tango (1952, Al Hoffman, Dick Manning na Pearl Bailey) Ona vyanzo/sources ili kusikiliza wimbo huu!

Methali hii ina maana nyingi tofauti ambazo unaweza kutekeleza katika mahusiano na maisha yako ya kila siku. Mambo mengi huhitaji watu zaidi ya mmoja: Wawili wanatakiwa ili kushirikiana, kufanya biashara ama kupigana. Ukitaka kucheza na mtu ambaye hataki kucheza na wewe, bora kumtafuta mchezaji mwengine.. Vivyo hivyo, ukiwa kwenye mgogoro au magomvi, itabidi ufikirie jinsi tabia yako inavyoweza kuchangia katika kuendeleza shida. katika dance, lengo si kuwa mkamilifu, bali ni kuendana na mwenzako na kufurahia pamoja.
Methali zinazofanana kutoka Afrika: 
Kimisri (Kiarabu): 
ايد لوحدها ماتسقفش‎
Mkono mmoja hauwezi kupiga makofi
Kiswahili:
Bila mtu wa pili ugomvi hauanzi
Kidole kimoja hakiuwi chawa
...
Updated 4mo ago
by
The winner of a competition or conflict receives the majority or entirety of the rewards, and possibly additional benefits beyond what was being fought over. 

In war, the spoils could refer to land, gained power or other sought after resources. In other pursuits the spoils typically refer to accolades, money or opportunities.

The proverb is typically used to explain unequal outcomes or to remind others that the stakes of many conflicts are winner take all, zero sum, or at the very least, disproportionately favorable to the few winners.

Check out the sources section for a description of the context and information about the US politician who was credited with the phrase (in the 1830s).
...
Updated 4mo ago
by