KAMUSI YA KISWAHILI-KICHINA ni kamusi mpya ya kipekee mahususi kwa watu wanaojifunza na kutumia lugha ya Kiswahili na Kichina. Kamusi hii imepangwa katika mpangilio mzuri unaomuwezesha mtumiaji wa Kiswahili na Kichina kuitumia vizuri na kwa urahisi. Sehemu ya Kwanza; Kiswahili- Kichina, Sehemu ya Pili; Kichina- Kiswahili na Sehemu ya Tatu; Misamiati ya Kiswahili- Kichina – Matamshi. Sehemu zote tatu zina maneno na misamiati yenye vipengele vilivyopangiliwa vizuri kumwezesha msomaji kutumia kamusi hii vizuri hatua kwa hatua .
Kamusi hii ya Kiswahili – Kichina ni muhimu sana katika maendeleo ya lugha ya Kiswahili na Biashara. Ni sehemu ya uthibitisho kwamba lugha yetu ya Kiswahili ni lugha pevu na endelevu na yenye uwezo wa kujenga na kuelezea misamiati mbalimbali kwa lugha mbalimbali katika kufanikisha lengo la mawasiliano kwa kuunganisha watu katika nyanja mbalimbali. Hivyo Kamusi hii itakuwa na faida kubwa kwa wanafunzi , wasomi, wafanyabiashara na watafiti wa Tanzania na China.
Ni kamusi ya aina yake, Pata nakala yako sasa.
...