You are now browsing in Swahili. Switch to English
In Swahili: "Sasa unavinjari kwa Kiswahili. Rudi kwa Kiingereza"
Lazime uingie akaunti ili kubadilisha wasifu wako au kuona wasifu wa wengine

Umeshafungua akaunti? Ingia

Ingia
Umesahau nenosiri lako?
Sijapata barua pepe ya kuthibitisha

Fungua akaunti mpya

Taarifa
Majadiliano
Methali
Methali ya Leo
Karibuni sana katika majadiliano yetu ya leo juu ya methali hii:

Mchumia juani, hulia kivulini

Ili kupiga KURA kwa Methali ya Mwezi
Kura
59
ili kupiga kura
Kura
59
Iliharirishwa miezi 4 iliyopita
by
View this proverb in English
Work in the sun, eat in the shade
na Magreth Lazaro Mafie 🇹🇿
🏆 Shindano la Insha ya Methali 
🥉 Mshindi wa Tatu
Ni mara ngapi umesikia Mchumia juani hulia kivulini? Hii ni methali ya kiswahili (kibantu) yenye maana ya kuwatia moyo watu katika shughuli mbalimbali wanazozifanya Kila siku wawe na Imani kuwa ipo siku watayafurahia matunda ya kazi yao. 

Methali hii huwapa watu nguvu, bidii, moyo, ujasiri, tumaini na weledi katika kufanya kazi. Mfanyakazi huamini kuwa baada ya kazi ngumu zenye surubu basi huleta mavuno mazuri yenye kumfanya astareheke kivulini akila matunda ya kazi yake. Shairi lifuatalo linaonesha kwa namna gani mchumia juani huwa katika majukumu ya Kila siku.

Siogopi jua wala mvua, nikiitengeneza kesho yangu
Siogopi maumivu Wala majeraha, maana yote ni ya muda
Jua kali na kazi ndiyo desturi yangu, ili kheri kuja maishani
Machinga,mkulima, makuli na mvuvi wao na jua, Ili kuitafuta kesho
Mchumia juani, hulia kivulini bado nakitafuta kivuli.
Ni mchana jua la utosi, kichwani nina mavuno, jasho linatiririka
Jua limezama Sasa kasia ufukweni, hoi kitandani, nyavu zi baharini
Nyumbani mtaa wa nne, nahodha wa familia surubu nivute  kheri
Jua Sasa la chomoza, Kiguu na njia kulitafuta tonge
Mchumia juani, hulia kivulini bado nakitafuta kivuli.

Bwana mmoja alikuwa mkulima. Maisha yake yote alitumia katika kilimo. Hivyo kupendeza kwake kulikuwa mara chache. Watu kijijini kwake walimuita mkulima stadi. Alijenga nyumba kwa kuuza sehemu ya mazao yake, alisomesha wanae kwa kilimo.

Bwana huyu alikuwa mtu mwenye bidii alijifunza siku zote kanuni za mkulima bora, hivyo kadri muda unavyokwenda mashamba yake alivuna mazao mengi. Watu wengi walistaajabu sana kuona mabadiliko makubwa ndani ya familia yake. Aliwekeza vitu vingi kijijini kwake, mashamba, nyumba, maduka na mifugo mingi vilitoka shambani.

Watu wengi walikuja kujichukulia hekima kwa mkulima stadi. Siku zote aliwaambia "Mchumia juani, hulia kivulini. Jembe limeniheshimisha kijijini Mimi na familia yangu. Maisha yangu sasa yanakwenda barabara kwa hakika niko kivulini nafurahia matunda ya kazi yangu ya juani. Mimi leo kijana wa mkulima huyo stadi najivunia malezi, uwajibikaji wake kwa sababu kazi za juani leo zimetufanya tupumzike na kula kivulini. Kwa hakika maana ya mchumia juani inaonekana kwa vitendo. Bidii yako ndilo jua lako na kivuli ndiyo matunda ya bidii yako.

Hadithi hii inashibishwa na hadithi ilee ya "Mabala the Farmer" yaani Mabala Mkulima iliyoandikwa na Richard S. Mabala(1989). 

Mabala alikuwa mfanyakazi bandarini Kisha akapunguzwa hivyo akachagua kurudi kijijini Morogoro. Mabala alikuwa mzembe,mlevi na mbishi. Mabala alikwenda shambani na galoni ya pombe alikunywa na kulala, alipoamka alimwongelesha mkewe lakni hakujibiwa zaidi ya  sauti ya jembe tik-tok, tik-tok .

Mabala alikuwa mbishi, alimwagilia sukari shambani alifikiri ni mbolea, lakni mwisho alibadilika na kuwa mkulima stadi akawa mchumia juani ili familia yake ije kulia kivulini. Je wewe unahisi Mabala ni mchumia juani? Ndani ya familia au kwenye jamii mkulima stadi anakupa picha gani?

Mwisho hadithi hii kutoka katika methali ya mchumia juani hulia kivulini hutuonyesha dira njema katika kila tunachokifanya katika maisha ya kila siku. Huku methali kama Subira yavuta kheri, Mgaa na Upwa hali wali mkavu zote hufanana kimaudhui, zipo katika kuipa jamii nguvu na matumaini kwa kila jambo lifanyikalo katika malengo.
Marejeleo

Juu ya Insha hii

Insha hii ilishinda nafasi ya tatu 🥉 katika Shindano la Methali ya Insha la Maktaba.org 🏆 7/7/2023
Magreth Lazaro Mafie ni mwanafunzi Mtanzania 🇹🇿 

Hakimiliki

Creative Commons Attribution (CC BY 4.0)
na Magreth Lazaro Mafie
Ilichapishwa na Maktaba.org
Mchoro/Image: CC BY Maktaba.org

The original essay included the following image, which is not included in the Creative Commons license.
Mchoro huu na / This image from: Honey Bee Arts - YouTube