Maswali Yaliyoulizwa Mara kwa Mara
Dhumuni ya maktaba.org ni nini?
Maktaba.org ilianzishwa ili kuwawezesha watu kusoma vitabu vinavyoboresha maisha yao, vinavyokuza vipaji vyao, na vinavyowasaidia kutimiza malengo yao.
Maktaba iko wapi?
Tunashirkiana na taasisi ya Elimu Yetu ipo mji wa Arusha, Tanzania, eneo la Kijenge. Maktaba iko Tindigani karibu na Ofisi ya Kata Kimandolu.
Tunawakaribisha wageni Kijenge, Arusha!
97 Kijenge Tindigani, Kimandolu
PO Box 837, Arusha, Tanzania
www.elimuyetu.org
admin@maktaba.org
97 Kijenge Tindigani, Kimandolu
PO Box 837, Arusha, Tanzania
www.elimuyetu.org
admin@maktaba.org
Maktaba.org ina matokeo gani?
1) Tunaunganisha wasomi wa jamii yetu na wasomi wa dunia kusoma pamoja na kufunzana.
2) Tunajenga uwezo wa jamii kustahimili, kujitegemea na kukuwa.
3) Tunakuza utamaduni wa usomaji Afrika Mashiriki na Marekani.
Nina ushauri kuiboresha tovuti.
Tunatafuta mawazo bunifu ya kuiboresha maktaba.org! Tafadhali usisite kutuma maoni yako na kupendekeza mabadiliko kwa kuwasiliana na admin@maktaba.org.
Nichangieje
Unaweza kuchangia kwa kujiunga na maktaba.org na kushiriki katika mazungumzo ya jamii. Tafadhali wasiliana na admin@maktaba.org. Tunategemea michango ya jamii yetu na wasomi kama wewe kutuwezesha kuendelea kutoa elimu bila malipo popote ulipo. Tunawashukuru, asanteni sana.
Nianze wapi?
1) Jiunge na jaza wasifu wako.
4) Hifadhi vitabu katika orodha zako za kusoma
5) Viangalie vitabu vinavyosomwa na marafiki wako, na jiungane na wasomi wengine wanaoshiriki mavutio yako.
Vitabu vipi vinapatikana?
Maktaba.org kuna vitabu vya kupakua ("ebooks"), vikiwemo Rasilimali Huria za Elimu ("Open Educational Resources / OER"), na vitabu bora vya Uwanga wa Umma ("Public Domain"), kwa Kiingereza na Kiswahili. Pia katika maktaba yetu iliyopo Arusha eneo la Kijenge Tindigani, kuna vitabu vya nakala ngumu vinavyopatikana kwa kuazima kwa wanachama wa Maktaba.org walioko Arusha, Tanzania. Angalia vitabu vyote kwa eneo
Mnafuata mitaala ya nchi gani?
Maudhui yetu hutumika nchi zote na popote ulipo, na hayakupangwa kufuata mitaala yoyote ya kitaifa. Tumevikusanya vitabu vya Kiswahili na Kiingereza ili kukuza Elimu ya Kujitegemea kwa watu wa marika yote na kila ngazi ya elimu. Soma zaidi kuhusu falsafa yetu
Jinsi ya kuthibitisha akaunti kwa baruapepe
Ili kutumia vipengele vyote vya maktaba.org, lazima uthibithishe email yako kwa kubofya kiungo katika baruapepe tuliyotuma uliposajili awali. Kama haujapata barua yetu, bofya Nitumie tena barua ya kuthibitisha. Kama huwezi kuingia kwenye email yako sasa, tafadhali unda akaunti mpya au wasiliana na utawala wa tovuti kupitia maktaba@elimuyetu.org
Jinsi ya kubadilisha lugha
Kwa kubadilisha lugha ya tovuti kwa akaunti yako, bofya lugha unayotaka, chini ya ukurasa.
Kwa kuona vitabu kulingana na lugha bofya “en” kwa vitabu vya kiingreza or “sw” for books in Kiswahili.
Kwa kuona vitabu kwa lugha katika ukurasa wa vitabu bofya en kwa kuona vitabu vya Kiingereza tu, au sw kwa kuona vitabu vya Kiswahili.
Naweza kushiriki maudhui ya aina gani?
Tunawaunganisha wasomi na tunawahimiza kushirikiana mawazo na maandishi kupitia chambuzi za vitabu, maoni na kubadilishana barua.
Kanuni za Jumuiya
- Shiriki tu maudhui ambayo ni mazuri, kweli na ya thamani.
- Waheshimu wasomi wengine kwenye mijadala ya jamii.
- Usishiriki matangazo, maudhui yenye vitisho/matusi, wala maudhui kinyume na sheria
Mbona maudhui niliyoshiriki hayaonekani?
Labda maudhui yako yaliondolewa kwa sababu yameenda kinyume na Kanuni za Jumuiya zilizoorodheshwa juu. Tunasimamia maudhui ya tovuti ili kulinda usalama wa jamii yetu ya wasomi kwa umri zote. Kwa mfano, tunaweza kuyaficha au kuyafuta maoni ya matusi, matangazo, maudhui ambayo hayawezi kushirikiwa kisheria, na picha zisizofaa watoto. Kama unaamini maudhui yako yaliondolewa kwa kukosa, tafadhli wasiliana na viongozi wa tovuti kupitia maktaba@elimuyetu.org
Je tovuti hii inayakusanya maelezo yangu binafsi?
Ndio, tunayakusanya maelezo yako ili kuboresha huduma tunazotoa, kukuwezesha kuingia akuanti na kuungana na wasomi wenglne, na kukupendekezea vitabu kwako. Hatutumii “cookies” kutoka kompani nyingine.
"We do not allow third-party cookies" maana yake haturuhusu makompani mengine kukufuatilia.
Je maktaba.org itatunza siri maelezo yangu binafsi?
Ndio. Tunatumia maelezo yako tu katika hali chache maalum, kama vile ili kuboresha tovuti hii.
Tunaahidi hatutauza maelezo yako kamwe wala kuyashiriki na watu wengine kwa madhumuni ya kibiashara wala utangazaji.
Nani anaweza kuona wasifu wangu?
Unaweza kuchagua kama wasifu wako utaonyeshwa kwa umma au kwa wahusika ya maktaba.org. Kwa kuona na kubadilisha mapendeleo yako, hariri mapendeleo ya wasifu wako