Sign up for news and free books by email!
Usimilisho wa Vielelezo Katika Hadithi za Watoto na Namna Vinavyochangia Katika Uwasilishaji Ujumbe
Written by
Publisher Kenyatta University
Published 2020
sw
Pages 120
Download
1.5 MB
Fasihi ya watoto ni ile ambayo msingi wa kidhamira na kimaudhui huwarejelea watoto. Fasihi ya watoto ni mpya ikilinganishwa na ile ya watu wazima kwa sababu imeanza kuangaliwa kwa upekee wake hasa kuanzia karne ya 18 (Wamitila, 2008). Vielelezo huchangia katika kurembesha umbo na mtindo wa kitabu katika kazi za watoto zilizosimilishwa (Sohaimi, 2011). Mtindo wa lugha, ploti ya hadithi, usawiri wa wahusika na mandhari ya hadithi za watoto hutegemea jinsi ambavyo mwandishi alitumia vielelezo ili kuwasilisha ujumbe. Vielelezo vinaweza kujisimamia na kupitisha ujumbe bila maandishi yoyote; vielelezo huambatanishwa na maandishi na hivyo kunoa ubongo wa mtoto, kuchochea fikra na hata kumfanya mtoto kuwa makini. Isitoshe, vielelezo hufurahisha watoto na kuwafanya kuwa na utashi wa kutaka kusoma zaidi. Hata hivyo, tafiti hizi za awali hazijahusisha moja kwa moja hadithi ya Wasifu wa Mwana Kupona na Alisi Ndani ya Nchi ya Ajabu. Vilevile, mtafiti ananuia kubainisha aina za vielelezo vilivyotumika katika riwaya ya Alisi Ndani ya Nchi ya Ajabu (Hadjavayanis, 2015) na Wasifu wa Mwana Kupona (King‟ei, 2008) na mchango wake katika kuendeleza ujumbe, kuchunguza changamoto zinazotokana na usimilisho wa vielelezo katika Wasifu wa Mwana Kupona (Kingei, 2008) na kuzitolea suluhu na kutathmini changamoto zinazotokana na usimilisho wa vielelezo katika Alisi Ndani ya Nchi ya Ajabu (Hadjavayanis, 2015) na kuzitolea suluhu. Malengo ya Utafiti i) Kubainisha aina za vielelezo vilivyotumika katika riwaya ya Alisi Ndani ya Nchi ya Ajabu (Hadjavayanis, 2015) na Wasifu wa Mwana Kupona (King‟ei, 2008) na mchango wake katika kuendeleza ujumbe. ii) Kuchunguza changamoto zinazotokana na usimilisho wa vielelezo katika Wasifu wa Mwana Kupona (Kingei, 2008) na kuzitolea suluhu. iii) Kutathmini changamoto zinazotokana na usimilisho wa vielelezo katika Alisi Ndani ya Nchi ya Ajabu (Hadjavayanis, 2015) na kuzitolea suluhu. Maswali ya Utafiti i) Ni aina zipi za vielelezo vilivyotumika katika riwaya ya Alisi Ndani ya Nchi ya Ajabu (Hadjavayanis, 2015) na Wasifu wa Mwana Kupona (King‟ei, 2008) na vinachangia aje katika kuendeleza ujumbe? ii) Ni changamoto zipi zinazotokana na usimilisho wa vielelezo katika Wasifu wa Mwana Kupona (Kingei, 2008) na zinaweza kutatuliwa vipi? iii) Ni changamoto zipi zinazotokana na usimilisho wa vielelezo katika Alisi Ndani ya Nchi ya Ajabu (Hadjavayanis, 2015) na zinaweza kutatuliwa vipi? The research aimed at analyzing illustrations in children literature and their contributions in conveying intended message. The researcher analysed adapted texts of Wasifu wa Mwana Kupona (King‟ei, 2008) and Alisi Ndani ya Nchi ya Ajabu (Hadjivayanis, 2015). The researcher focused on; identifying different types of illustrations used in the selected adapted texts and their contributions in conveying messages, analysed challenges in relation to illustrations derived from Wasifu wa Mwana Kupona (Kingei, 2008) and provided possible solutions to the challenges. Consequently, the researcher evaluated challenges in relation to illustrations derived from Alisi Ndani ya Nchi ya Ajabu (Hadjavayanis, 2015) and provided possible solutions to the challenges. The research was guided by adaptation theory by George Bluestone (1957) which was later modified by Goodman (1976), Andrew (1984) and Starrs (2006). Adaptation theory states that a new independent body work is formulated from the initial work. Data that was used in the research was from the library. In the library the researcher read journals, thesis and books related to the research. Moreover, the researcher also read, analysed and wrote down all important works related to the selected texts; Wasifu wa Mwana Kupona (2008) and Alisi Ndani ya Nchi ya Ajabu (2015). Finally, the data collected from this research was analysed by focusing on research objectives and the tenents of the Adaptation theory. The research findings identified the different types of illustrations used in the selected adapted texts. Illustrations identified in the study included; cartoons, map, coloured pictures and drawings. In addition, it was noted that illustrations were used to convey message if used appropriately. Challenges in relation to the usage of illustrations in the selected adapted texts have been discussed based on aspects of children literature that is; the relationship between an illustration and a text, through character potrayal, challenges in relation to setting of a story and colour usage. Furthermore, solutions to the challenges in relation to the usage of illustrations in the selected adapted texts have been explained using the same aspects of children literature mentioned above. This research has contributed to Kiswahili and children literature and more importantly, in children adapted illustrated stories. This is because, the research has laid foundation on issues pertaining illustrations in children literature. Besides, stakeholders in children literature, illustrators of children stories and ministry of education will benefit from research findings in conjuction with selecting a well illustrated child book
...
Utafiti huu unahusiana na vitabu viwili: Alisi Ndani ya Nchi ya Ajabu (Hadjavayanis, 2015) na Wasifu wa Mwana Kupona (King‟ei, 2008) Ukitaka kupakua eVitabu hivi (bure), ona Elisi Katika Nchi ya Ajabu na Utendi Wa Mwana Kupona Vitabu hivi vinapatikana bila malipo (watafsiri wengine). "Kwa wapenzi wote wa Kiswahili na hasa Fasihi ya Watoto hii ni zawadi yenu!" -Mwandishi Masters Thesis - Full Text
...
Thank you to Kenyatta University
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all

No Books Found

Based on the filters you selected, there are currently no books.