You are now browsing in Swahili. Switch to English
In Swahili: "Sasa unavinjari kwa Kiswahili. Rudi kwa Kiingereza"
Lazime uingie akaunti ili kubadilisha wasifu wako au kuona wasifu wa wengine

Umeshafungua akaunti? Ingia

Ingia
Umesahau nenosiri lako?
Sijapata barua pepe ya kuthibitisha

Fungua akaunti mpya

View this book in English Decolonizing Data: One Language at a Time
Jiandikishe upate habari na vitabu bure!
Kuondoa Ukoloni kwenye Data: Lugha Moja Moja
Mwaka 2023
sw
Kurasa 29
Pakua 1.1 MB

Katika wakati ambao wasiwasi juu ya kupatikana kwa teknolojia za kidijitaliunaongezeka, wazo kwamba tunashuhudia enzi ya ukoloni wa kidijitali na wa data linazidi kupata mvuto. Katika miaka ya hivi karibuni, wasomi na wanaharakati wamezidi kutegemea dhana ya ukoloni ili kuelewa athari ya teknolojia inayoegemea data, kujadili madhara yake, na kufikiria juu ya njia mbadala za kuwakomboa na kuwawezesha watu.

Kiini cha sehemu hii ya utafiti, muundo, na utetezi ni suala la lugha. Mnamo Machi 2022, Maabara ya Digital Civil Society katika Chuo Kikuu cha Stanford na mtandao wa Tierra Común walifanya mazungumzo ya mtandaoni na wanenaji na kuleta mitazamo na maarifa mbalimbali kwenye mada hiyo. Kazi yao inatualika tuweze kufikiria upya nafasi ya lugha katika ukuzaji wa teknolojia lakini vile vile katika uandaaji wa umma wa teknolojia hizi. Kwa pamoja, wanenaji hawa walichunguza kwa kina kwa nini mapengo ya lugha katika teknolojia za kidijitali ni muhimu sana kuangaziwa pamoja na jinsi yalivyojikita katika urithi wa ukoloni. Walijadiliana njia nyingi bunifu ambazo jamii zimekuwa zikikabiliana na changamoto hizi zinazohusiana na lugha. Wanenaji hao vile vile walizungumzia na kutafakari juu ya maana ya kiutendaji ya mitazamo isiyokuwa na ukoloni katika lugha na data.

Stakabadhi hii ni matokeo ya mazungumzo haya. Badala ya kutoa video ya mkutano huo, tumeandaa toleo lililohaririwa la unukuzi huo. Lengo letu ni kuanzisha mtagusano mzuri katika jinsi tunavyotoa habari na kuwaalika watu watumie muda wao kutafakari mazungumzo haya kwa makini zaidi. Hutasikia lafudhi nyingi mara moja katika majadiliano yetu, lakini utakutana na maneno katika lugha mbalimbali. Isitoshe, tunatoa tafsiri ya Kihispania na Kiswahili ya unukuzi huu. Uchaguzi wa lugha hizi mbili unadhirisha msisitizo wa Marekani Kusini na Afrika katika tajriba na miradi iliyojadiliwa na wanenaji hao.

Tunakushukuru kwa kutenga muda wako kupitia stakabadhi hii na ni matumaini yetu kwamba itakusaidia kupata taswira tofauti ya jinsi ulimwengu wa kidijitali unavyoweza kuwa.

...
CC-BY-SA
...
Kimetafsiriwa na
Alfred Mtawali
Shukrani kwa The Digital Civil Society Lab (DCSL), Stanford University
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all