Jiandikishe upate habari na vitabu bure!
Mwongozo wa Watumiaji wa Huduma za Mahakama
Mchapishaji Mahakama ya Tanzania
Mwaka 2008
sw
Kurasa 81
Mwongozo huu umeandaliwa kwa kuzingatia sheria na kanuni zinazoongoza utaratibu wa mashauri katika Mahakama ya Tanzania. Aidha, changamoto mbalimbali zinazowakabili watumiaji wa huduma za Mahakama zimetoa msukumo mkubwa wa kuwepo na Mwongozo kama huu utakaowawezesha watumiaji wa huduma za Mahakama kujua taratibu za mashauri kuhusu kufungua na kuendesha mashauri hayo Mahakamani. Mwongozo huu utasaidia
  • a. Kufahamu muundo na mamlaka ya Mahakama;
  • b. Kujua taratibu za mashauri katika ngazi zote za Mahakama;
  • c. Viwango vya ada mbalimbali zinazotozwa na Mahakama;
  • d. Kuelewa masharti yanayohusiana na utoaji dhamana;
  • e. Kujua taratibu za utoaji wa ushahidi, jukumu na kiwango cha kuthibitisha katika mashauri ya madai na jinai katika Mahakama zote; na
  • f. Kujua taratibu za utekelezaji wa hukumu.
Maelezo ya mwongozo huu yametolewa kwa lugha nyepesi ili kuwawezesha watumiaji huduma za Mahakama wasio na uelewa wa sheria, kuelewa na kuifikia Mahakama kirahisi na kupata haki husika
...
Uandaaji wa mwongozo huu umeainisha taratibu mbalimbali zitumikazo katika kusikiliza mashauri ya jinai na madai na umezingatia -
  • 1. Muundo na mamlaka ya Mahakama;
  • 2. Taratibu za ufunguaji Mashauri ya Jinai, Madai, Ndoa, Mirathi, Kazi, Biashara, Ardhi na katika Mahakama za watoto;
  • 3. Taratibu za rufaa na nafuu zinginezo kama marejeo, mapitio na masahihisho;
  • 4. Ada mbalimbali;
  • 5. Taratibu za dhamana;
  • 6. Ushahidi na namna ya kuthibitisha;
  • 7. Upatikanaji wa hukumu;
  • 8. Utekelezaji wa hukumu; na
  • 9. Taratibu za kupokea na kusikiliza malalamiko.
...
Shukrani kwa Tanzania Legal Information Institute
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all

No Books Found

Based on the filters you selected, there are currently no books.