na Mélanie N.
Mama, mama, mama!
Nuru ya mtu ni mama. Ukimkosa mama imezima nuru. Aheshimiwe mama, katika dunia hakuna kitu cha kumwakilisha.
Angeweza kutoa mimba yako akabaki kuwa kijana.Ila alivumilia mpaka miezi tisa ya kujifungua akakuweka ulimwenguni. Husaidia Mungu kumuumba mtu. Hakujali maumivu ya kujifungua, umbo lake, sura yake, umri wake, vyote vyake mwilini mwake vilibadirika ili upate uhai. Mama hufanya chini-juu ili upate afya njema. Alifanya kila liwezekanalo ili upate elimu ya kutosha. Huacha kile ambacho kingemfurahisha ili uwe mtu. Hushinda shambani ili upate cha kutia mdomoni. Mheshimu mama aliyekutunza hadi hapo ulipofika.
Kwa hiyo unatoa wapi ujasili wa kumtukana mama yako unamdharau mama yako ili umheshimu nani? Eti ungetangulia mbele yake ungemzaa. Kweli? Usijiidanganye. Atukae mama yake hujikosesha baraka. Kuwa makini vijana wa leo, msijitafutie mikosi na hasara visivyo na msingi ambavyo havitomalizika. Hata kama unamzidi elimu, mama anabaki kuwa mama. Hapo ulipo ndie kasababisha upafike. Kwa hiyo fanya uwezavyo ili umtoe hapo alipo.
Ulibarikiwa mama, umewazidi wote mama. Hakuna cha kukulipa mama isipokuwa tu kukutakia maisha mema tena marefu.