na Gaston Ch.
Usitukane wakunga na uzazi ungalipo
Related Posts
na Mélanie N. Mama, mama, mama!
Nuru ya mtu ni mama. Ukimkosa mama imezima nuru. Aheshimiwe mama, katika dunia hakuna kitu cha kumwakilisha.
Angeweza kutoa mimba yako akabaki kuwa kijana.Ila alivumilia mpaka miezi tisa ya kujifungua akakuweka ulimwenguni. Husaidia Mungu kumuumba mtu. Hakujali maumivu ya kujifungua, umbo lake, sura yake, umri wake, vyote vyake mwilini mwake vilibadirika ili upate uhai. Mama hufanya chini-juu ili upate afya njema. Alifanya kila liwezekanalo ili upate elimu ya kutosha. Huacha kile ambacho kingemfurahisha ili uwe mtu. Hushinda shambani ili upate cha kutia mdomoni. Mheshimu mama aliyekutunza hadi hapo ulipofika.
Kwa hiyo unatoa wapi ujasili wa kumtukana mama yako unamdharau mama yako ili umheshimu nani? Eti ungetangulia mbele yake ungemzaa. Kweli? Usijiidanganye. Atukae mama yake hujikosesha baraka. Kuwa makini vijana wa leo, msijitafutie mikosi na hasara visivyo na msingi ambavyo havitomalizika. Hata kama unamzidi elimu, mama anabaki...
na Alfred N. Hapo zamani za kale katika Kijiji cha NYAMAGOMA ,kulitokea binti moja anayeitwa SUDI Aneti ambaye katika maisha yao ya kila siku alikuwa akitamaani maisha ya raha tu. Alikuwa na Tabia ya kuwachuna wanaume kwa kuwaomba pesa nyingi.Alipoona hayo hayatoshi aliamua kujiunga na ushirikina na kuenda kwa waganga wa kienyeji kwa lengo la kuzitafuta pesa nyingi kwa muda mfupi. Ni ukweli pesa aliipata tena ya kutosha Ila ikawa ni ya masharti .wazazi wake walijaribu kumshauri aachane na ushirikina huo bali aanzishe miradi yake huku akianzia kwa vinavyolingana na uwezo wake hakuwasikiliza.Alieendelea kuyaishi maisha hayo,huku matatizo yakawa yanamkuta kila wakati,ilifika kiasi mizimu ikamuomba uhai wa mama yake kama kafara naye akakataa kata kwa ubadaye Mali zote zilipoptea akafikia hatua ya kujuta akiukumbuka ushauli alioupewa na wazazi wake.angelikubali kulidhika na mali zinazokuja taratibu yasingelimkuta hayo yote kwa ukweli CHURURU SI NDONDONDO
Chururu...
Read more...na Magreth Lazaro Mafie 🇹🇿🏆 Shindano la Insha ya Methali
🥉 Mshindi wa TatuNi mara ngapi umesikia Mchumia juani hulia kivulini? Hii ni methali ya kiswahili (kibantu) yenye maana ya kuwatia moyo watu katika shughuli mbalimbali wanazozifanya Kila siku wawe na Imani kuwa ipo siku watayafurahia matunda ya kazi yao.
Methali hii huwapa watu nguvu, bidii, moyo, ujasiri, tumaini na weledi katika kufanya kazi. Mfanyakazi huamini kuwa baada ya kazi ngumu zenye surubu basi huleta mavuno mazuri yenye kumfanya astareheke kivulini akila matunda ya kazi yake. Shairi lifuatalo linaonesha kwa namna gani mchumia juani huwa katika majukumu ya Kila siku.
“Siogopi jua wala mvua, nikiitengeneza kesho yangu
Siogopi maumivu Wala majeraha, maana yote ni ya muda
Jua kali na kazi ndiyo desturi yangu, ili kheri kuja maishani
Machinga,mkulima, makuli na mvuvi wao na jua, Ili kuitafuta kesho
Mchumia juani, hulia kivulini bado nakitafuta kivuli.
Ni mchana jua la utosi, kichwani nina mavuno, jasho...
na Rose Mwanri 🇹🇿 🏆 Shindano la Insha ya Methali
🥈 Mshindi wa Pili Akiba Haiozi
Methali ni usemi wa kimafumbo unaotumika katika jamii. Maneno katika methali huwa na maana ya ziada na methali huwa na pande mbili. Upande wa kwanza hutoa wazo na upande wa pili humalizia wazo. Akiba haiozi ni miongoni mwa methali za kiswahili inayotumika sana katika jamii za kiafrika na kwa watumiaji wa lugha ya kiswahili duniani, ikiwa na lengo la kuwaasa watu juu ya umuhimu wa kujiwekea akiba.
Dhima ya methali hii ni kutusisitiza sisi wanajamii kujianda vema na maisha ya leo pamoja na kesho huku tukiwa tayari kuzikabili changamoto mbalimbali za maisha.
Methali hii hutuonyesha ni kawaida mwanadamu kupatwa na dharura mbalimbali katika maisha ya kila siku. Mfano kupatwa na maradhi, ajali, au hata kifo. Pale unapokuwa na akiba uliyojiwekea itakusaidia wakati umepatwa na changamoto ya ghafla ambayo hukuitarajia.
Faida nyingine ya kuweka akiba ni kuboresha maisha. Cha kwanza nashauri tuwe na utaratibu...
by Nankya Sauda 🇺🇬🏆 Proverb Essay Contest
🥇 First Place Winner
Still waters run deep
Ever taken time to wonder why the elderly will always live to be wiser than the young? Have you ever taken time to meditate on where your origin sprouts from? If not, it is high time you started looking for your origin because it is important for one to know their roots.
Over time, you take the burden to unveil the nature of famous geniuses and their personalities, you will come to realize that they are celebrated introverts. It is important that one takes off some time their busy schedule and read about some of the top celebrated geniuses like Albert Einstein , the famous scientist from whom we derive one of the most educative quotes;
““The monotony and solitude of a quiet life stimulates the creative mind.””
This highlights that time spent alone does not only provide one with space for self-reflection but also gives space to someone to use their mind creatively. Great talkers are great are...
Read more..."na Ibrahim Nyanda
🏆 Shindano la Insha ya Methali“Ni kwa nini kijiji chetu hakina maendeleo ukilinganisha na vijiji vingine vinavyotuzunguka? Vijana wengi kutoka vijiji vingine wa umri wetu wamesoma na wengine wana kazi zao za maana huko mjini. Pamoja na kwamba kuna shule kijijini kwetu lakini vijana hatufanyi vizuri shuleni na hata walimu wanapoajiriwa hawakai muda mrefu wanahama. Kuna nini hapa Bombambili?" Haya ni maswali ambayo kijana Akilimali alimwuliza rafiki yake Manase wakiwa machungani wakilisha ng’ombe.
Mara baada ya swali hili Manase alionekana amezama katika wimbi kubwa la mawazo na mara baada ya kufikiri kwa muda alimgeukia rafiki yake Akilimali na kumtazama kwa kina kiaha akamwuliza, “Unaamini kuhusu ushirikina” Akilimali alijibu kwa kutikisa kichwa kuashiria kukubaliana na swali aliloulizwa na kisha akasema “Naamini kwani mara kadhaa nimekua nikiona watu wakienda kwa waganga na wengine wanapopitia magumu huamini wamerogwa, si unakumbuka juzi bibi Andunje...
Read more...na Angelica A. Methali ya "mpanda ngazi hushuka" ina maana kwamba watu wanaopanda ngazi za mafanikio au mamlaka wanaweza kushuka haraka kutoka kwenye nafasi yao ya juu. Inatukumbusha kwamba hali ya mafanikio au umaarufu haijithibitishi kuwa ya kudumu au salama. Mambo yafuatayo yanathibitisha ukweli kuhusu methali hii;
Hali ya Majivuno; Methali hii inaweza kutumika kuonyesha hatari ya kujivunia sana mafanikio au kuwa na kiburi. Inatuambia kwamba hali ya juu inaweza kubadilika ghafla, na mtu anaweza kupoteza kile alichokuwa nacho ikiwa hatakuwa makini au asipoweza kudumisha kiwango chake cha juu cha kazi au tabia nzuri.
Kupandishwa cheo; Methali hii pia inaweza kutumika kuwahimiza watu wawe waangalifu na waangalie mbali zaidi, wasijiridhishe na mafanikio yaliyopatikana hadi wakati huo, na badala yake wajitahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii na kudumisha maadili yao ili kuepuka kuanguka. Methali hii inatufundisha baada ya kupandishwa cheo tusijisahau katika uwajibikaji wetu wa...
na Lolly F. 🅽🅾 🅿🅰🅸🅽😔 🅽🅾 🅶🅰🅸🅽✊
No pain no gain is a proverb mostly used by many of us since we all believe in working hard and hustling alot so as we can all live a good life.
This proverb was first used by one of the famous poet in 1648 named 𝗥𝗼𝗯𝗲𝗿𝘁 𝗛𝗲𝗿𝗿𝗶𝗰𝗸 in the little poem named "no pain no gain". Some of the quoted verses of the poem include the verse that stated "man's fortunes are according to his pains".
In one of the streets in makamba village lived a poor man with his wife and two daughters. The man had a lung cancer that made him weak for couple of days and since the family had no money to pay for the hospital bills then the man was forced to stay at home without getting any treatment despite the fact that his wife worked hard but the little money she got was used for food. The two daughters had two different personalities since the older one was too proud and lazy but the Young one was kind and hard-working so the father decided to give them a test and he told them"my...
Read more...