You are now browsing in Swahili. Switch to English
In Swahili: "Sasa unavinjari kwa Kiswahili. Rudi kwa Kiingereza"
Lazime uingie akaunti ili kubadilisha wasifu wako au kuona wasifu wa wengine

Umeshafungua akaunti? Ingia

Ingia
Umesahau nenosiri lako?
Sijapata barua pepe ya kuthibitisha

Fungua akaunti mpya

Elimu Yetu Jitihada ya kupata Michango ya Vitabu, 2021 - 2022

Toa michango yako leo!

Changia vitabu kwa maktaba yako

Toa kitabu na saidia kupambana na ujinga na umaskini.
Unaweza kuchangia kitabu chochote, kipya au cha zamani
Waulize majirani, ndugu na marafiki wako. Labda wana vitabu visivyotumika kwao.

Vitabu hubadilisha maisha!

Mtu mmoja anaweza kubadilisha maisha ya watu wengi.

Imarisha maktaba yetu

Michango yako itaimarisha maktaba yetu na sote tutapata nafasi ya kusoma vitabu vingi zaidi.
Tunategemea wafadhali wakarimu kama wewe ili kuendelea kuitumikia jamii yetu.
Tafadhali waambie marafiki zako, familia na majirani kuhusu Elimu Yetu na uliza kama wana lolote la kuchangia. Tunakubali kifedha na michango ya aina yote. Elimu Yetu kwa sasa inahitaji:
Vitabu
Vifaa vya Shule
Vyakula
Vifaa vya Michezo
Kompyuta, kompyuta mpakato na kompyuta za mkononi
Kitu cha thamani zaidi unaweza kuchangia ni muda wako. Elimu Yetu kwa sasa inatafuta watu wa kujitolea kufundisha masomo yote na washauri wa wanafunzi wa rika zote. Huna haja ya kuwa na cheti cha kufundisha au kujua Kiingereza. Kama una ujuzi au kipaji, tafadhali njoo ujiunge na jamii yetu na ushiriki na wengine.

Toa mchango wako leo!

Ili kutoa mchango wako, tafadhali wasiliana na:
Johnson John
Mkutubi wa Elimu Yetu
john@elimuyetu.org
Simu: 0629911602

Tafadhali tutembelee Kijenge Tindigani


Plot 126, Block GG, Kijenge Tindigani, Kimandolu
PO Box 837, Arusha, Tanzania
www.elimuyetu.org
maktaba@elimuyetu.org