You are now browsing in Swahili. Switch to English
In Swahili: "Sasa unavinjari kwa Kiswahili. Rudi kwa Kiingereza"
Lazime uingie akaunti ili kubadilisha wasifu wako au kuona wasifu wa wengine

Umeshafungua akaunti? Ingia

Ingia
Umesahau nenosiri lako?
Sijapata barua pepe ya kuthibitisha

Fungua akaunti mpya

Jiandikishe upate habari na vitabu bure!
Mafunzo ya Kutafakari Usomaji
Mchapishaji 21st Century Basic Education Program (TZ21)
Mwaka 2014
sw
Pakua
1.7 MB
Wapendwa Walimu Mafunzo haya ya kutafakari usomaji kwa walimu wa darasa la 1 na 2 katika shule za msingi ni juhudi nyingine tena za Programu ya TZ21 kuboresha ufundishaji wa usomaji na matumizi ya rasilimali za usomaji zilizopo shuleni. Mafunzo haya yanalenga kuimarisha uwezo wa walimu katika kuchunguza na kutumia kwa upana rasilimali/zana za usomaji zilizotengenezwa na TZ21 pamoja na zile zinazobuniwa na walimu na wanafunzi wenyewe ili kuwa na matokeo bora zaidi katika kufundisha usomaji. Malengo, mazao na matokeo ya mafunzo haya ni kama ilivyobainishwa hapa chini: Malengo: Walimu wataweza: - Kutafakari maendeleo na changamoto za programu ya usomaji. - Kuchunguza maudhui ya kielektroniki na kuamua matumizi yenye matokeo bora zaidi wakati wa kufundisha. - Kujifunza zaidi kazi/shughuli zenye matokeo bora zaidi ya usomaji kwa kutumia rasilimali/zana zilizofaraguliwa katika kufundishia. - Kuchunguza zana na rasilimali kwa matumizi bora yanayolengwa. - Kuchunguza uchaguzi wa matini yanayoendana na ngazi ya usomaji. - Kufanya mazoezi na kutumia stadi walizopata kujiandaa kwa ufundishaji. Mazao: walimu wataweza: - Kutumia vizuri maudhui ya kielekroniki wakati wakifundisha. - Kuchagua zana na rasilimali za usomaji zinazofaa kwa ajili ya kufundishia. - Kuchagua matini zinazoendana na ngazi ya usomaji wa wanafunzi wao. Zana za Uandaaji wa Rasilimali/Vifaa vya Usomaji
...
Mafunzo haya ya kutafakari usomaji kwa waalimu wa darasa 1 na 2 ni matokeo ya msaada wa watu wa Amerika kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada ya Kimataifa ya Mendeleo la Amerika (USAID) kwa Programu ya Elimu ya Msingi ya TZ21. Msaada huu wa watu wa Amerika unalenga kujenga uwezo wa watoto wa Tanzania kielimu.
...
Shukrani kwa 21st Century Basic Education Program (TZ21)
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all