Publisher 21st Century Basic Education Program (TZ21)
Wapendwa Walimu
Mafunzo haya ya kutafakari usomaji kwa walimu wa darasa la 1 na 2 katika shule za msingi ni juhudi nyingine tena za Programu ya TZ21 kuboresha ufundishaji wa usomaji na matumizi ya rasilimali za usomaji zilizopo shuleni. Mafunzo haya yanalenga kuimarisha uwezo wa walimu katika kuchunguza na kutumia kwa upana rasilimali/zana za usomaji zilizotengenezwa na TZ21 pamoja na zile zinazobuniwa na walimu na wanafunzi wenyewe ili kuwa na matokeo bora zaidi katika kufundisha usomaji. Malengo, mazao na matokeo ya mafunzo haya ni kama ilivyobainishwa hapa chini:
Malengo: Walimu wataweza:
- Kutafakari maendeleo na changamoto za programu ya usomaji.
- Kuchunguza maudhui ya kielektroniki na kuamua matumizi yenye matokeo bora
zaidi wakati wa kufundisha.
- Kujifunza zaidi kazi/shughuli zenye matokeo bora zaidi ya usomaji kwa kutumia
rasilimali/zana zilizofaraguliwa katika kufundishia.
- Kuchunguza zana na rasilimali kwa matumizi bora yanayolengwa.
- Kuchunguza uchaguzi wa matini yanayoendana na ngazi ya usomaji.
- Kufanya mazoezi na kutumia stadi walizopata kujiandaa kwa ufundishaji.
Mazao: walimu wataweza:
- Kutumia vizuri maudhui ya kielekroniki wakati wakifundisha.
- Kuchagua zana na rasilimali za usomaji zinazofaa kwa ajili ya kufundishia.
- Kuchagua matini zinazoendana na ngazi ya usomaji wa wanafunzi wao.
Zana za Uandaaji wa Rasilimali/Vifaa vya Usomaji
...