Illustrator Marco Tibasima
Publisher: Twaweza, Raising Voices
sw
Namna ya kutumia kijitabu hiki:
- Orodhesha sifa za mwalimu bora
- Mwambie rafiki yako au mwalimu mwenzio andae orodha kama hiyo na kisha ifananishe na ya kwako.
- Soma kijitabu hiki pamoja na walimu wengine au wanafunzi shuleni. Kisha jadili jinsi mwalimu bora anapaswa kuwa namna gani.
Waalimu: someni sehemu moja wa kijitabu hiki kila wiki wakati wa mkutano waalimu kisha jadilini jinsi ya kutekeleza mapendekezo haya.
- Jadilini changamoto zinazoweza kutokea katika kufanikisha malengo haya. Kisha andaeni mbinu zinazoweza kusaidia kutatua hizo changamoto.
- Wanafunzi: someni sehemu moja ya kijitabu hiki kila wiki pamoja na rafiki zenu. Kisha jaribuni kubainisha walimu wazuri katika shule yenu.
...