Simulizi za Buibui ni mfululizo wa vitabu vya maarifa kwa watoto wa ngazi za chini. Mfululizo huu unahusu viumbe wadogo katika Maisha ya kila siku ya mtoto. Viumbe hawa wanaishi katika mazingira ya nyumbani yanayomzunguka mtoto.
Madhumuni yake ni kujenga tabia za kisayansi kwa watoto tangu mapema. Vitabu vinalenga kuamsha na kuchochea udadisi. Pia, vinalenga tabia na ari ya uchunguzi katika mazingira.
...