Publisher E & D Vision Pub.
Je, umeshawahi kusafiri kwa kutumia ungo au fagio?Umeshapanda mgongoni mwa nguva au kutalii kwenye tumbo la nyangumi? Hivi ni baadhi ya visa alivyofanya Majaliwa akiwa katika safari yake kuzunguka Tanzania nzima akisaka marimba yake ya nyuzi ishirini. Alianzia Mafia,akaenda Zanzibar,Tanga,Moshi, Arusha,Iringa,Mwanza,Kigoma na miji mingine mingi. Na Kongoti,bingwa wa taifa wa Marimba akimchenga kila mara,huku akingangania marimba ya Majaliwa ili amzuie kushinda na ashinde yeye. Na bila marimba ya nyuzi ishirini,hakuna ushindi.Je,Majaliwa atamkamata Kongoti?Ungana na Majaliwa katika safari hii ya kusisimua,ukutane na Bibi yake anayeweza kuwa katika umbo lolote,jinsi anavyochenga n kuvisumbua vibwengo huko angani usiku wa manane wakiwa na Majaliwa na safari hii ya kusaka marimba yake.
A novel.
...