You need to login to view profiles OR to update your profile

Have an account? Login

Log in
Forgot your password?
Didn't receive your confirmation email?

Create a new account

Sign up for news and free books by email!
Mafunzo ya Kuboresha Ujuzi na Stadi za Kazi kwa Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa Tanzania Bara
Publisher Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
Published 2012
sw
Pages 251
Download 3.0 MB
Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa imeandaa Programu ya Mafunzo ya Maafisa Watendaji wa Kata, Vijiji na Mitaa. Kitabu cha kufundishia kimefanyiwa mapitio ili kuweza kuhusisha mambo yote mapya ya muhimu yaliyojitokeza wakati wa kuendesha Mafunzo. Tayari mafunzo kwa Watendaji wa Kata yamefanyika kote nchini; na sehemu kubwa ya Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa. Yote haya yanafanyika kwa ajili ya kuboresha utoaji wa huduma bora kwa Wananchi. Shabaha au lengo kuu la mafunzo haya ni kuwawezesha Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa kuelewa na kuzingatia misingi na utaratibu wa utekelezaji wa majukumu yao kulingana na malengo ya Serikali. Aidha, madhumuni mahsusi ya mafunzo haya ni kuwawezesha Maafisa hao: • Kuelewa Sheria, Muundo na mfumo wa Uendeshaji wa Serikali za Mitaa; • Kuelewa dhana ya Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa; • Kuelewa Muundo wa Utumishi wa Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa; • Kuelewa Kazi , Wajibu na Haki za Maafisa Watendaji wa Vijiji na Mitaa; • Kuelewa Wajibu wa Afisa Mtendaji wa Kijiji na Mtaa kama Mlinzi wa Amani; • Kuelewa mbinu za Menejimenti na Uongozi, Sheria za Kazi na Usuluhishi wa Migogoro; 10 • Kuelewa Kanuni na Taratibu za Uendeshaji wa Ofisi na Mikutano, Utunzaji wa Kumbukumbu, na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano; • Kuelewa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kuondoa Umaskini, Ujasiliamali na Uanzishwaji wa Vikundi; • Kuelewa Utaratibu wa Uandaaji wa Mipango Shirikishi Jamii katika ngazi ya Kijiji na Mtaa; • Kuelewa Mbinu za Uandikaji na Usimamizi wa Miradi; • Kuelewa Misingi ya Usimamizi wa Fedha na Taratibu za Manunuzi; • Kuelewa umuhimu wa kuzingatia Sheria na Kanuni za Maadili ya Watumishi wa Umma katika utekelezaji a majukumu yao; • Kuelewa masuala mtambuka yanayohusu Utawala Bora na Demokrasia, Uchambuzi wa Kijinsia na Makundi yenye Mahitaji Maalumu na Usimamizi wa Majanga (Ukimwi na Hifadhi Endelevu ya Mazingira)
...
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all