Jiandikishe upate habari na vitabu bure!
Kiongozi cha Mwalimu kwa Shule Inayojali Mazingira an Elimu kwa Maendeleo Endelevu
Kwa Shule za Msingi Tanzania
Kimeandikwa na Elisa Pallangyo
Mchapishaji Tanzania Forest Conservation Group
Mwaka 2017
sw
Kurasa 44

Elimu ina uwezo wa kumpa binadamu maarifa na baadaye kumbadilisha mwelekeo na tabia yake kuendena na mabadiliko ya dunia.

Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania pamoja na serikali ya Tanzania wamejitahidi kufanya kazi ya kujenga uwezo na welewa wa mazingira kwa shule, jumuiya na wananchi kwa ujumla ili waweze kutoa michango yao ya kuhifadhi na kulinda mazingira na rasilimali zao kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Mojawapo wa mbinu za kupata maendeleo endelevu ni pamoja na kutumia na kuendeleza Elimu ya Mazingira shuleni na katika jamii. Serikali imekuwa inaingiza Elimu ya Mazingira katika mitaala ya shule za msingi, sekondari na vyuo. Uingizaji wa Elimu ya Mazingira katika mitaala itasaidia kwa kiasi kubwa kulinda na kuhifadhi mazingira yetu na hivyo kupata maendeleo endelevu.

Kiongozi hiki cha Mwalimu kinakusudia kuwapatia welewa, stadi na kuwajengea uwezo walimu wa kuingiza Elimu ya Mazingira na Elimu kwa Maendeleo Endelevu katika mtaala wa shule za msingi Tanzania. Kiongozi hiki pia kinamjengea mwalimu uwezo wa kutumia taratibu / mbinu za ufundishaji na ujifunzaji zinazounga mkono Uchunguzi, Maono, Matendo na Mabadiliko (UMMM), IVAC. Mfumo wa UMMM unasisitiza kutumia njia za ufundishaji na ujifunzaji wa vitendo, kufikiri kwa makini, uhuru wa kujieleza/kulezea mawazo yako na kutumia mazingira yako kama zana za kufundishia na kujifunzia. Mbinu zote hizi zinaendeleza haki za binadamu na elimu bora kwa mwanafunzi.

Ni matumaini kuwa Kiongozi hiki kitamwezesha mwalimu aweze kuingiza Elimu ya Mazingira /Elimu kwa Maendeleo Endelevu katika mtaala na wanafunzi waweze kupata maarifa, stadi za maisha na njia sahihi za kubadilisha mwelekeo na tabia zao katika kufikia Maendeleo Endelevu.

...
Shukrani kwa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili, Tanzania na Danish Outdoor Council
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all

No Books Found

Based on the filters you selected, there are currently no books.