You need to login to view profiles OR to update your profile

Have an account? Login

Log in
Forgot your password?
Didn't receive your confirmation email?

Create a new account

Ufuatiliaji wa Fedha za Ruzuku kwa Shule za Msingi Nchini
Publisher Taasisi Ya Kuzuia Na Kupambana Na Rushwa
Published 2020
sw
Pages 25
Download 0.8 MB
Katika kutekeleza majukumu yake, kwa mujibu wa kifungu cha 7(a) na (c) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11/2007, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ilifuatilia fedha za ruzuku kwa shule za msingi 971 katika Halmashauri mbalimbali nchini katika kipindi cha mwezi Agosti na Septemba 2019. Lengo kuu la ufuatiliaji huu ni kutathmini usimamizi wa fedha za ruzuku zinazotolewa kwa shule za msingi (Capitation Grant, CG) ili kuhakikisha malengo ya Serikali ya kutoa elimu kwa watoto wote wenye umri wa kwenda shule yanafikiwa. Malengo mahususi ni: kufuatilia matumizi ya fedha za ruzuku kwenda katika shule za msingi; kutathmini ushiriki wa wadau katika usimamizi wa fedha za ruzuku; kubaini mianya ya rushwa; na kubaini changamoto katika matumizi ya fedha. Katika kufikia lengo la ufuatiliaji, maswali matano yalijibiwa - je kuna uvujaji/ubadhilifu wa fedha? Je kuna ucheleweshaji wa fedha? Je kuna thamani ya fedha? Je kuna uwazi katika matumizi? Je usimamizi wa Halmashauri ukoje? Je ipo mianya ya rushwa? Je shule zinakabiliwa na changamoto zipi katika matumizi ya fedha? Taarifa za ufuatiliaji huu zilipatikana kupitia hojaji (questionnaire), orodha ya ukaguzi (checklist), mahojiano na wadau, na kupitia nyaraka. Jumla ya shule 971 zilifuatiliwa nchi nzima ambazo ni sawa na 5.6% ya shule zote za msingi. Aidha, wakati wa ufuatiliaji, timu zilifanya majadiliano na wapokeaji na watumiaji wa fedha hizo, kuwaeleza kilichobainika na kutoa ushauri wa hatua za haraka za kuchukua ili kuboresha matumizi ya fedha hizi. Matokeo ya ufuatiliaji yanabainisha mapungufu na changamoto kama ifuatavyo: (a) kutokuwepo kwa kiwango sawia cha mgawanyo wa fedha za ruzuku kulingana na idadi ya wanafunzi waliosajiliwa; (b) fedha za ruzuku kutotosheleza mahitaji yote yanayowekwa; (c) kutozingatiwa kwa taratibu za manunuzi (Kutotumia hati msako, kutotangazwa kwa zabuni na baadhi ya wajumbe wa kamati kuwa wazabuni na kushiriki kwenye vikao vya maamuzi); (d) kutokuwepo kwa matumizi sahihi ya store-ledger kwa vifaa vinavyonunuliwa na kutolewa kwa ajili ya matumizi mbalimbali; (e) uwepo wa malipo mbalimbali ya vifaa yasiyo na risiti za kieletroniki (EFD Machine) hali inayotia shaka uhalali wa manunuzi hayo; (f) ukosefu wa mafunzo ya kitaalamu kwa Kamati za shule na waalimu kuhusu matumizi ya fedha za ruzuku; (g) kukosekana kwa uwazi katika matumizi ya fedha za ruzuku; na (h) uwepo wa maelekezo kutoka TAMISEMI yanayokinzana kuhusu fungu la michezo. Kufuatia matokeo hayo, TAKUKURU ilitoa mapendekezo ya kuziba mianya ya rushwa ili kuboresha usimamizi wa fedha za ruzuku hasa katika matumizi na ushiriki wa wadau.
...
Thank you to Taasisi Ya Kuzuia Na Kupambana Na Rushwa
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all