Publisher ZAFELA - Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar - Zanzibar Female Lawyers Association
Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar-ZAFELA imezindua kitabu cha haki za wanawake kwa mujibu wa quran na sunna za mtume Muhammad S.W.A. Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya doble tree mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na wanasheria mbali mbali wanawake pamoja na wajumbe kutoka taasisi ya Konrad Adnawa Stiftung. Akitoa ufafanuzi wa kitabu hicho chenye jumla ya kurasa 68 juu ya haki ya uongozi na ushirikishwaji wa mwanamke pamoja na masuala ya kiuchumi, Mkurugenzi wa ZAFELA Jamila Mahmoud amesema kitabu hicho kimeangazia vyema maeneo hayo kwa mujibu wa muongozo wa dini.
...