You are now browsing in Swahili. Switch to English
In Swahili: "Sasa unavinjari kwa Kiswahili. Rudi kwa Kiingereza"
Lazime uingie akaunti ili kubadilisha wasifu wako au kuona wasifu wa wengine

Umeshafungua akaunti? Ingia

Ingia
Umesahau nenosiri lako?
Sijapata barua pepe ya kuthibitisha

Fungua akaunti mpya

Jiandikishe upate habari na vitabu bure!
Mwongozo wa Mfumo wa Haki za Binadamu wa Afrika
Maadhimisho ya Miaka 40 Tangu Kupitishwa kwa Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu 1981 - 2021
Kimeandikwa na
Mchapishaji Pretoria University Law Press
Mwaka 2022
sw
Kurasa 106
Pakua
4.1 MB
Mwongozo huu unachukuliwa kama ni utangulizi unaopatikana na wenye taarifa nyingi za mfumo wa haki za binadamu ulioanzishwa na Umoja wa Afrika. Mwongozo huu unatoa muhtasari wa maendeleo yanayohusu Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu, chombo chake cha usimamizi, Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, na Mkataba wa Haki na Ustawi wa Mtoto na chombo chake cha usimamizi, Kamati ya Afrika ya Wataalam wa Hakina Ustawi wa Mtoto. Toleo hili la Mwongozo lilizinduliwa tarehe 27 Juni 1981, kwakuadhimisha miaka 40 iliyopita, ambapo Mkataba wa Afrika ulipitishwa. Pia, mwaka 2021 ni mwaka wa 15 tangu Mahakama ya Afrika ianze kufanya kazi. Mwongozo unalenga kuonyesha matukio muhimu ya maendeleo ya kihistoria na kutoa utangulizi wa mfumo wa Afrika wa haki za binadamu, unaopatikana na unaoendelea kurejewa kila wakati. Mwongozo umeandaliwa na Kituo cha Haki za Binadamu, Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Pretoria kikishirikiana na Tume ya Afrika. Matoleo mawiliya Mwongozo yalitolewa mwaka 2011 na 2017. Kituo cha Haki za Binadamu, ambacho mwaka 2021 kinasheherekea miaka 35 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1986, ni idara ya kitaaluma na pia ni Shirika Lisilo la Kiserikali. Kituo kina hadhi ya uangalizi katika Tume ya Afrika. Kituo kinatoa programu za kitaaluma na kinashiriki katika utafi ti, utetezi na mafunzo ya haki za binadamu, kikilenga zaidi Afrika. Progamu zake kuu ni Shahada ya Umahiri katika Haki za Binadamu na Demokrasia katika Afrika na Mashindano ya Mahakama ya Afrika Haki za Binadamu ya Mfano. Kwa taarifa zaidi kuhusu Kituo cha Haki za Binadamu, tembelea tovuti ya Centre for Human Rights, Faculty of Law, University of Pretoria, South Africa.
...
ISBN: 978-1-991213-04-4
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all