Maadhimisho ya Miaka 40 Tangu Kupitishwa kwa Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu 1981 - 2021
Written by
Publisher Pretoria University Law Press
Mwongozo huu unachukuliwa kama ni utangulizi unaopatikana na wenye taarifa nyingi za mfumo wa haki za binadamu ulioanzishwa na Umoja wa Afrika. Mwongozo huu unatoa muhtasari wa maendeleo yanayohusu Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu, chombo chake cha usimamizi, Tume ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu, na Mkataba wa Haki na Ustawi wa Mtoto na chombo chake cha usimamizi, Kamati ya Afrika ya Wataalam wa Hakina Ustawi wa Mtoto. Toleo hili la Mwongozo lilizinduliwa tarehe 27 Juni 1981, kwakuadhimisha miaka 40 iliyopita, ambapo Mkataba wa Afrika ulipitishwa. Pia, mwaka 2021 ni mwaka wa 15 tangu Mahakama ya Afrika ianze kufanya kazi.
Mwongozo unalenga kuonyesha matukio muhimu ya maendeleo ya kihistoria na kutoa utangulizi wa mfumo wa Afrika wa haki za binadamu, unaopatikana na unaoendelea kurejewa kila wakati. Mwongozo umeandaliwa na Kituo cha Haki za Binadamu, Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Pretoria kikishirikiana na Tume ya Afrika. Matoleo mawiliya Mwongozo yalitolewa mwaka 2011 na 2017.
Kituo cha Haki za Binadamu, ambacho mwaka 2021 kinasheherekea miaka 35 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1986, ni idara ya kitaaluma na pia ni Shirika Lisilo la Kiserikali. Kituo kina hadhi ya uangalizi katika Tume ya Afrika. Kituo kinatoa programu za kitaaluma na kinashiriki katika utafi ti, utetezi na mafunzo ya haki za binadamu, kikilenga zaidi Afrika. Progamu zake kuu ni Shahada ya Umahiri katika Haki za Binadamu na Demokrasia katika Afrika na Mashindano ya Mahakama ya Afrika Haki za Binadamu ya Mfano. Kwa taarifa zaidi kuhusu Kituo cha Haki za Binadamu, tembelea
tovuti ya Centre for Human Rights, Faculty of Law, University of Pretoria, South Africa.
...