You are now browsing in Swahili. Switch to English
In Swahili: "Sasa unavinjari kwa Kiswahili. Rudi kwa Kiingereza"
Lazime uingie akaunti ili kubadilisha wasifu wako au kuona wasifu wa wengine

Umeshafungua akaunti? Ingia

Ingia
Umesahau nenosiri lako?
Sijapata barua pepe ya kuthibitisha

Fungua akaunti mpya

Kijitabu cha Maadili kuhusu Kufanya Kilicho Sahihi
Mchapishaji Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (Serikali ya Tanzania)
sw
Kurasa 31
Pakua
0.5 MB
Ili nchi iwe na maendeleo ni muhimu kwa kila mwananchi kudhamiria kufikia kiwango cha juu cha uadilifu. Hii inamaanisha kwamba tunahitaji kufanya kilicho sahihi daima ili kujenga imani ya watoto wetu, watumishi wenzetu na wananchi wengine. Kama Mtumishi wa Umma, ili kufanya kilicho sahihi hapana budi kutekeleza majukumu kwa kuzingatia taaluma, kuwa mwaminifu na kuwajibika. Kwa upande wake, Serikali ina jukumu la kuwajengea uwezo watumishi wake ili waweze kuzingatia utaalamu wao, wawe waaminifu na wawajibike. Ufafanuzi unaotolewa katika kitabu hiki una lengo la kusaidia uelewa wa Kanuni za Maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma na hapana budi kusomwa pamoja na Sera, Sheria na Kanuni za nchi. Kwa kutumia maadili yaliyoainishwa kwenye Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma ufafanuzi huu unachanganua maadili ya msingi ya kuzingatia utaalamu, kuwa mwaminifu na kuwajibika. Ufafanuzi huu una mifano itakayokusaidia kuelewa mitanziko ya kimaadili unayokabiliana nayo ili kukusaidia kufanya uamuzi kwa uadilifu. Vilevile, kama mtumishi wa umma, mwenye kuzingatia utaalamu, mwaminifu na mwenye kuwajibika ni jukumu lako daima kufanya kilicho sahihi. Ndio maana maadili haya ya msingi yanakuhusu na yanatumika kwetu sisi sote, bila ya kujali jinsia, kabila, rangi, cheo, dini au umri. Kama mtumishi wa umma wewe pia ni mlezi wa dhamana ya umma. Watu unaowahudumia wanakutegemea utekeleze majukumu yako kwa uadilifu na kwa kiwango cha juu cha uwezo wako. Hivyo una wajibu wa kuonyesha kuwa unastahili dhamana hiyo kwa kutekeleza kwa vitendo maadili ya utumishi wa umma. Hivyo ukimwona mwananchi au mtumishi anakiuka maadili ya utumishi wa umma unatakiwa utoe taarifa kwa Mamlaka husika. Serikali imekusudia kuweka utaratibu wa kupokea taarifa na malalamiko ulio dhabiti na salama kwa watoa taarifa au walalamikaji. Endapo unahitaji ushauri zaidi kuhusu Kanuni za Maadili ya Utumishi wa Umma au Ufafanuzi huu tafadhali wasiliana na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma. Kama mmoja wa wanaowajibika kuheshimu na kutekeleza Maadili ya Utumishi wa Umma, mimi binafsi nimedhamiria kuonyesha mfano wa kutekeleza majukumu kwa kuzingatia taaluma, kuwa mwaminifu na kuwa mwajibikaji. Kutokana na dhamana ya umma uliyopewa na wewe pia unatakiwa uwe mfano wa kuigwa. Ruth H. Mollel Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma
...
Shukrani kwa Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora (Serikali ya Tanzania)
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all