Utawala wa Sheria: Mwongozo kwa Wanasiasa

Faster download
Download 1.0 MB

Published Year: 2012

Book Thumbnail

Language: sw

Details: Tafsiri ya Kitabu hiki kutoka lugha ya Kiingereza kwenda Kiswahili imefanywa na Bw. Adam Shafi na Bodi na Wafanyakazi wa Kituo cha Huduma za Sheria cha Zanzibar (Zanzibar Legal Services Centre), S.L.P. 3360, Zanzibar, Tanzania kwa kujitolea (pro bono).

Summary: Madhumuni ya mwongozo huu ni kuwapatia wanasiasa uwelewa juu ya misingi muhimu ya utawala wa sheria. Maelekezo ya utayarishaji wa Mwongozo huu yalikuwa ni kuwa uwe mfupi kama inavyowezekana ili uweze kusomwa na wanasiasa wenye shughuli nyingi katika ngazi mbalimbali. Lakini vile vile uwe na faida kwa watoaji maamumuzi na watunga sera wengine, kwa wanahabari na wengineo wanaohitaji kujipatia uwelewa kuhusu mada hii. Kadhalika, Mwongozo huu lazima uwe ni rahisi kuutafsiri na kuchapishwa kwa lugha mbalimbali. Hii ndiyo maana hamna michoro ya majedwali na picha katika Mwongozo huu. Lugha halisi ya Mwongozo huu ni Kiingereza. Hata hivyo, Mwongozo unaweza kutafsiriwa katika lugha nyengine kwa ruhusa ya Taasisi husika, ilimradi tu Utangulizi huu unakuwemo na kuwa tafsiri hiyo ni tafsiri ya kweli ya makala hii. Nakala halisi ya Mwongozo huu inapatikana katika mitandao ya Taasisi simamizi, na tafsiri zitaingizwa humo vile vile.