You need to login to view profiles OR to update your profile

Have an account? Login

Log in
Forgot your password?
Didn't receive your confirmation email?

Create a new account

Kushiriki kwa Wananchi katika Mchakato wa Bajeti Katika Kaunti Zao
Publisher Kituo cha Sheria, Kenya
sw
Pages 20
Download
3.0 MB
Kama mwananchi, umepewa mamlaka katika mfumo wa ugatuzi. Mamlaka haya pia yana majukumu. Unastahili kushiriki katika maamuzi yanayohusu maisha yako kama vile kuchangia katika kubuniwa kwa bajeti na mipangilio ya serikali. Jukumu lako ni kuelewa kinachofanywa na serikali na kuhakikisha kuwa umehusika kikamilifu katika maamuzi inavyowezekana. Ugatuzi ni kubadili namna uamuzi unavyofanywa na utoaji wa huduma nchini Kenya. Fikiria huduma unazozijali kama vile, afya, maji, masomo au makao. Ni nani anaye amua na kutahmini huduma itakayopewa kipaumbele kifedha? Katika mfumo mpya wa ugatuzi kuna sehemu mbili za utawala; ile ya Kaunti na ile ya Kitaifa. Kaunti zina majukumu ya baadhi za huduma. Serikali ya kitaifa vile vile. Lakini serikali zote mbili zinafaa kufanya kazi kwa pamoja zikishirikiana. Kaunti zina majukumu juu ya elimu ya kimsingi ya utotoni (kama vile ya chekechea), soko, vituo vya afya vya Kaunti, makao, maji, usafi, na zinginezo. Kaunti zinastahili kutunga fedha kwa ajili ya huduma hizi kila mwaka. LAZIMA wananchi wahusishwe katika michakato ya bajeti.
...
Thank you to Kituo cha Sheria, Kenya
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all