View this book in English Preparing in Advance for Potential Investors
Maandalizi kabla wawekezaji watarajiwa hawajafika
Mwongozo kwa ajili ya mapatano na wawekezaji katika jamii: Kitabu cha 1
Mchapishaji Columbia Center on Sustainable Investment
sw
Kurasa 49
Pakua
4.0 MB

Mwekezaji anaweza kuifikia jamii wakati wowote akihitaji ardhi na rasilimali. Miongozo hii inatoa mapendekezo kuhusu namna ambavyo watetezi na viongozi wa jamii wanaweza kuzisaidia jamii kujiandaa, na endapo zikiamua basi ziingie katika majadiliano ya kina kuhusu mikataba na wawekezaji wanaotaka kutumia ardhi na rasilimali za jamii kwa ajili ya biashara zao.

Mwongozo huu (Mwongozo 1) unaeleza namna ambavyo jamii zinaweza kujiandaa kwa majadiliano na wawekezaji watarajiwa, ikiwemo kufanya maamuzi kuhusu kufikia makubaliano au la. Mwongozo unaweza kutumika kuisaidia jamii: (a) kujiandaa kabla mwekezaji hajafika (b) kuamua kuingia katika majadiliano au la na mwekezaji ambaye ameshafika. Mwongozo 1 unapaswa utumike kabla ya kuanza maafikiano yoyote.

...
Kituo cha Uwekezaji Endelevu cha Columbia ni kituo kinachoongoza kwa utafiti unaotumika, na jukwaa lililoundwa kwa ajili ya kujifunza na kujadili uwekezaji endelevu wa kimataifa. ccsi.columbia.edu Namati ni shirika la kimataifa lililoundwa kwa ajili ya kuendeleza nyanja ya uwezeshaji wa kisheria na kuimarisha uwezo wa watu wa kudai na kulinda haki zao.
...
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all

No Books Found

Based on the filters you selected, there are currently no books.