Handbook on laws governing land, marriage, children's rights, inheritance, divorce and sexual offences.
Kiongozi hiki cha Sheria kimeandaliwa na wajumbe wa kujitolea wa Kituo cha Msaada wa Sheria kwa Wanawake, (WLAC) kwa ajili ya Wasaidizi wa Sheria ambao si wanasheria (Paralegals) ambao wana moyo wa kuwasaidia wanawake na watoto. Friedrich-Ebert-Stiftung wamefadhili uandishi na uchapaji wa Kiongozi hiki, kwa matarajio kuwa kitasaidia kuinua hali ya wanawake wa Tanzania kwa kuongeza ufahamu wa sheria na haki zao. Tunatumaini kuwa Kiongozi hiki kitaweza kufanikisha madhumuni hayo ambapo itasaidia katika nyanja zote za maendeleo.
Sura ya Kwanza ya Kiongozi hiki inahusu Sheria za Ardhi.
Sura ya Pili inaelezea kuhusu Sheria ya Ndoa. sura hii inachambua nini maana ya ndoa, ni mambo gani muhimu kuyatimiza kabla ya kufunga ndoa, aina za ndoa, namna ya kugeuza ndoa, dhana ya ndoa na masharti yake. Mwisho inafafanua haki na wajibu wa wanandoa.
Sura ya Tatu ya Kiongozi hiki inaelezea Sheria inayohusu Talaka. Ndani ya sura hii inaelezwa talaka ni nini, sababu ya kutoa talaka na sababu zinazosababisha ndoa kuvunjika kutolewa kwa talaka. Mwisho imefafanua taratibu za kufuata kisheria ili talaka iweze kutolewa.
Sura ya Nne ya Kiongozi hiki inachambua kwa kina Haki za Mtoto. Inafafanua mtoto ni nani, hadhi mbalimbali anazopewa mtoto kisheria, haki za mtoto kimataifa, Mkataba Kiongozi cha Sheria ix wosia umefafanuliwa – maana yake, aina za wosia na taratibu wa kimataifa wa Haki za mtoto. Pia inaelezea ni nani mwenye wajibu wa kumtunza mtoto. Ndani ya sura hii wajibu wa wazazi, jamii na taifa unafafanuliwa. za kuandika wosia. Pia taratibu za kufuata katika kufungua mirathi kama kuna wosia au hakuna wosia, zimefafanuliwa.
Sura ya Tano ya Kiongozi hiki inahusu Sheria ya Mirathi. Katika sehemu hii imefafanuliwa maana ya mirathi, Sheria zinazoshughulikia mirathi nchini Tanzania na namna sheria hizo zilivyoweka mgawanyo wa mali zilizoachwa na marehemu miongoni mwa warithi.
Vilevile Sura ya Sita na ya mwisho ya Kiongozi hiki inahusu Sheria ya Makosa ya Kujamiiana. Sura hii inaangalia mabadiliko katika sheria mbalimbali zinazogusa makosa ya kujamiiana.
Ni matumaini yetu kuwa wale wote watakaosoma kiongozi hiki watanufaika vya kutosha na elimu watakayoipata.
...