You need to login to view profiles OR to update your profile

Have an account? Login

Log in
Forgot your password?
Didn't receive your confirmation email?

Create a new account

Mirathi Nchini Tanzania
Mwongozo Kuhusu Mirathi, Wosia na Taratibu za Kimahakama Tanzania
Written by Simon Swai
Publisher Mahakama ya Tanzania
Published 2021
sw
Pages 65
Download 1.4 MB
"Maisha ni zawadi kutoka kwa Mungu Muumba wetu, zawadi hii ya maisha sio ya milele kuna siku nitakufa. Kifo kinapotokea pamoja na mambo mengine kuna maswali mawili ya msingi huzaliwa; (i) Wapi inakwenda roho yangu? na (ii) Mali na ndugu zangu wanabaki vipi? Kitabu hiki kinajikita kwenye kipengele cha pili tu kwa kuwa kipengele cha kwanza kina watu maalumu wa kukiongelea." - Simon O. Swai (Mwandishi) "Mirathi na taratibu zake ni eneo nyeti kwa sababu linawahusu wafu na walio hai. Licha ya kuwepo sheria zinazosimania eneo hili, ufafanuzi wa sheria hizo na maelekezo mahususi ya Majaji wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu kupitia hukumu mbalimbali, bado usimamizi wa mirathi ni changamoto kubwa katika jamii yetu. Wajane, na Watoto hasa waliozaliwa nje ya ndoa bado wanapitia changamoto nyingi kufikia haki zao kupitia mirathi. Kitabu hiki kinajaribu kuelezea kwa lugha nyepesi taratibu za kuzingatia ili kifo kisiwe chanzo cha migogoro katika jamii zetu. Kwa muktadha huo, mwandishi amesisitiza umuhimu wa kuandika wosia na utaratibu wa kufuata. Ameelezea pia, kwa ufasaha mkubwa, taratibu za kimahakama za usimamizi wa mirathi tangu Mahakama za Mwanzo hadi Mahakama ya Rufani. Ni matumaini yangu, kama yalivyo matumaini ya mwandishi, kwamba kitabu hiki ni kwa manufaa na kinaweza kusomwa na kueleweka kwa kila mwanajamii. Chafaa pia wa matumizi ya Wanasheria wanaosimamia mashauri ya mirathi, Mahakimu, Majaji na kufundishia vyuoni kama kitabu cha rejea." -Ilvin Claud Mugeta, Jaji, Mahakama Kuu Kigoma
...
Thank you to Tanzania Legal Information Institute
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all