You are now browsing in Swahili. Switch to English
In Swahili: "Sasa unavinjari kwa Kiswahili. Rudi kwa Kiingereza"
Lazime uingie akaunti ili kubadilisha wasifu wako au kuona wasifu wa wengine

Umeshafungua akaunti? Ingia

Ingia
Umesahau nenosiri lako?
Sijapata barua pepe ya kuthibitisha

Fungua akaunti mpya

Michango mipya
157
vitabu
24
Wachangiaji

Karibu kwenye Maktaba!

Jiunge au Ingie na jiungane na wasomi wa dunia!

Maktaba.org imeumbwa kuwawezesha watu kusoma vitabu vinavyoboresha maisha yao, vinavyokuza vipaji vyao, na vinavyowasaidia kutimiza makusudi yao.

Maswali Yanayoulizwa Mara kwa Mara

  • Soma mtandaoni na pakua vitabu
  • Azima vitabu Arusha mjini
  • Toa maoni na jadili vitabu

Karibuni sana wageni!
Kimandolu, Arusha, Tanzania


22 Tindigani Street, Kijenge Kaskazini, Kimandolu
PO Box 837, Arusha, Tanzania
www.elimuyetu.org
maktaba@elimuyetu.org
Kuhusu Elimu Yetu
Elimu Yetu ni muungano wa famlia wanaothamini elimu. Tunaelimishana kupitia vipaji, ufahamu, na mtazamo chanya, na tunakufikia popote ulipo. Pamoja na Maktaba, tunatoa elimu bila malipo kwa watoto, vijana na watu wazima kwenye kituo chetu, Kijenge, Arusha, Tanzania. Kwa kujifunza zaidi au kujiunga, karibuni sana tutembelee.

Kusoma kuna faida gani?

"Vitabu ni hazina ya akili na elimu. Hazina ya fedha, dhahabu na majohari hufunguliwa kwa funguo. Ufunguo wa kufungulia hazina za vitabu ni kusoma. Mtu yeyote awezaye kusoma huweza kuingia katika hazina hii akachukua akili na elimu nyingi kama awezavyo kuona."
  • - Shaaban Robert, katika "Vitabu," Insha na Mashairi (1967)
“Unadhani dhiki ya kuvunjika moyo na maumivu yako ni ya pekee, hayajawahi kutokea katika historia ya dunia. Baadaye unasoma. Ni vitabu ndivyo vilinifundisha kwamba mambo yalioyonitesa sana ni yaleyale yanayoniunganisha na watu wote wanaohai na waliowahi kuwa hai.”
  • - James Baldwin, imetafsiriwa kutoka "The Doom and Glory of Knowing Who You Are," Life Magazine (1963)
“Elimu si kitu cha prestige. Elimu ni kitu cha kumkuza binadamu tu. Kumuwezesha kupanua uwezo wake... Waswahili wanasema ‘Kanga hatagi ujani utumwani’... Ignorance inapinga huyu binadamu kuchanua na kukua akafikia uwezo wake wote kwa sababu huyu ni kiumbe mwenye akili. Hakamilika mpaka akili zake zimepata nafasi za kuulewa uliimwengu na kuutawala ulimwengu. Huyu si mbuzi huyu. Huyu ni binadamu. Hataki afya ya kawaida tu. Ataka vilevile na akili yake ielewe mambo yalivyo… Elimu kazi yake ya kwanza, na kubwa zaidi, ni hii ya kupambana na mazingira yanayomzuia bindamamu kuflower, kublossom, kutaka akafikia hali ya mwisho.”
  • - Julius K. Nyerere, "Maana ya Elimu," (1975)
“Unaweza kuwa mwanafunzi, mwalimu, mfanyabiashara, profesa, msanii, mkulima, fundi, mhadhiri, mwanariadha, mama wa nyumbani -chochote kile -neno ni moja tu kuwa: hapo ulipo hapatoshi! Unao uwezo wa kubadilisha maisha yako katika nyanja yoyote ile kama unataka na ukitaka utazitendea kazi kanuni, mbinu na maarifa yaliyomo ndani ya [v]itabu. Asili na hulka yako si kusota na kubaki hapo ulipo, bali kupambana na changamoto ya aina yoyote ile ili uweze kupata ushindi maishani. Usikubali mtu yeyote, mazingira yoyote au hali yoyote ile ikukandamize na kuuzika uwezo, vipaji na maarifa yaliyojificha ndani yako. Na kama tunakubaliana juu ya ukweli huu, basi napenda nikupe hoja nne muhimu: Hoja ya kwanza ni kuwa: nakutaka ukisome kitabu , kwa uchache, mara tatu. Hoja ya pili ni kuwa: uwe na kalamu. [Andika] kanuni ama mbinu yoyote unayoona kuwa imekuvutia… Hoja ya tatu: kibebe [kitabu]; utembee nacho kokote uendako na ukisome wakati wowote upatapo fursa. Na hoja ya mwisho ni kuwa: usiishie katika nadharia, bali chukua hatua na hatamu kutafsiri nadharia katika vitendo ... Kwani unao uwezo wa kufanya hivyo. -Mwandishi”
  • - Emmanuel Mbogo, “Siri Za Maisha,” (2010)