You are now browsing in Swahili. Switch to English
In Swahili: "Sasa unavinjari kwa Kiswahili. Rudi kwa Kiingereza"
Lazime uingie akaunti ili kubadilisha wasifu wako au kuona wasifu wa wengine

Umeshafungua akaunti? Ingia

Ingia
Umesahau nenosiri lako?
Sijapata barua pepe ya kuthibitisha

Fungua akaunti mpya

Jiandikishe upate habari na vitabu bure!

Enjoy thousands of free books, support non-profit programs or get tools to grow your non-profit

Falsafa

Mitazamo Bora kutoka Vitabu Tunavyopenda Zaidi

Maktaba ya Elimu Yetu tunaamini mitazamo bora huja kwa kusoma! Hivi ni vitabu vitatu vya msingi vilivyotushawishi na vilivyotuhamasisha kuunda tovuti hii. Visome sasa au vitafute bila malipo katika maktaba karibu na kwako, na jiunge na maktaba.org ili kushiriki katika mijadala ya jamii!

Siri za Maisha

Siri za maisha ni riwaya ya Kiswahili inayosimulia hadithi ya Pama, fundi wa kompyuta, aliyekatishwa tamaa na kazi yake ya kuchosha na maisha yake ya kawaida, akialikwa kuanza safari ya ajabu, kuingia kwa ulimwengu wa makuburi, na kugundua vipaji vyake vilivyofichwa na mtazamo mpya kuhusu maisha.
Kanuni:
  • Kila mtu ana uwezo mkubwa na vipaji vilivyofichwa ndani yake.
  • Wengi wanabaki walipo kwa sababu ya “Programu Tasa” au fikra potofu kwamba hawana uwezo.
  • Ili kutimiza uwezo wa ajabu uliozaliwa nao, lazimu tupange upya akili zetu kwa “Programu Zae "Programu Zae" zilizotuwezesha kujiamini.
  • Watoto wanapaswa kutiwa moyo na kuhamasishwa kugundua uwezo wao bila kusikia matusi.
  • Ili kutimiza ndoto zako, hupaswi kukata tamaa.
  • Usiishie vitabu katika nadharia “bali chukua hatua na amua kutafsiri nadharia katika vitendo katika maisha yako

Leadership Education

Elimu ya Uongozi ni njia ya kufundisha kwa kumpa mtu uhuru wa kujiongoza katika safari ya elimu yake. Mamenta huwawezesha wanafunzi kujiendeleza kupitia hatua za asili za kujifunza kuanzia misingi bora, kwenda upendo wa kujifunza, na kuwa wasomi ili kutimiza sudi zao.
Kanuni:
  • Kila mtu ana wito na uwezo wa kujiamua.
  • Kila mtu ana akili.
  • Elimu ni ile inayomwezesha mtu kuvigundua na kuvikuza vipaji vyake kwa juhudi zake za hiari.
  • Ukitaka kulea mfuasi, mpe kijana mazoezi ya kufuata, kutii na kunyenyekea. Ukitaka kulea kiongozi, mpe nafasi ya kujiongoza na kuwaongoza wenzake.
  • Viongozi bora wanataka walimu na mamenta wema wanaowapenda, wanaowajali kwa muda mrefu, na wanaowalea kwa ujumla.

Elimu Ya Kujitegemea

“Elimu ya Kujitegemea” ni hotuba iliyotolewa mwaka 1967 na Mwalimu Julius K. Nyerere, baba wa taifa la Tanzania. Mwaka 1948 Mwl. Nyerere alikuwa mkulima na mwalimu wa kawaida wa Secondary Tabora kijijini, lakini alisikia wito wa kusimamia haki za asili za Waafrika, na alijua elimu yake bora ilimtayarisha kutimiza kusudi hili. Baada ya kuteswa na kukamatawa na wakoloni kwa sababu ya uharakati wake, Mwl. Nyerere akaendelea kuongoza Tanzania kupata uhuru bila vita mwaka 1961. Elimu ya Kujitegemea ilichapishwa 1967 miaka michache baada ya uhuru kuelekea njia mpya ya elimu kwa taifa jipya, na leo bado insha yake ni waraka wa sera wa elimu taifa la Tanzania.
Insha ya “Elimu ya Kujitegemea” inaanza kwa kuuliza shabaha ya elimu ni nini? Kurithisha hekima na maarifa kutoka kizazi kimoja kwenda kingine ili kuwaanda vijana kuyaelewa na kuyabadilisha mazingira yanayowazunguka na kuchukua nafasi zao kwenye jamii. Halafu Mwl. Nyerere alitaja changamoto tatu zilizorithishwa na mfumo wa elimu ya ukoloni. Unapozisoma, fikiria na jiulize: je umeona changamoto hizi kwenye mfumo wa elimu wa taifa lako leo?
  • Kwanza, elimu ya kikoloni ulinfaisha wanafunzi wachache tu, walioweza kupata ajira kwa mashindano kama maafisa na karani serikalini.
  • Pili, shule za kikoloni zililea watoto mbali na familia, shamba na maisha halisi, na ziliwafundisha wanafunzi kudharau wazazi na utamaduni wao.
  • Tatu, mfumo wa elimu wa kikoloni uliwapa wanafunzi fikra potofu kwamba maarifa yote ya thamani hupimwa na mitihani na hupatikana kwa vitabu vilivyoandikwa na wataalamu.
Katika nusu ya pili ya hotuba yake, Mwl. Nyerere akaelezea suluhisho, Elimu ya Kujitegemea: Kuwaalika familia na majirani shuleni, kuwapa wanafunzi uhuru wa kujiamulia elimu yao, na kutumia miradi ya kilimo na ujasiramali katika mitaala ili kukuza ujuzi na fikra ya kujitegemea.
Principles:
  • Shabaha ya Elimu ni kurithisha maarifa na hekima kutoka kizazi kimoja kwenda kingine ili kuwawezesha vijana kuyaelewa na kuyabadilisha maazingira yanayowazunguka, na kuchukua nafasi zao katika jamii.
  • Elimu ni wajibu wa kila mtu, kila mlezi na kijiji kwa ujumla.
  • Kila mtu ni mwalimu na mwanafunzi, bila kujali umri wake au ngazi ya elimu, kwa sababu kila mtu ana kitu cha kujifunza na kitu cha kufundisha.
  • Vijana hujifunza bora kupitia miradi ya maana na kazi halisi

Soma kitabu chote
Elimu ya Kujitegemea

Kinapatikana kwa Kiswahili au kwa Kiingereza.