Lazime uingie akaunti ili kubadilisha wasifu wako au kuona wasifu wa wengine

Umeshafungua akaunti? Ingia

Ingia
Umesahau nenosiri lako?
Sijapata barua pepe ya kuthibitisha

Fungua akaunti mpya

Taarifa
Majadiliano
Methali
Ili kupiga KURA kwa Methali ya Mwezi
Kura
0
Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by
"Maisha yakikupa limao, tengeneza juis" inamaanisha pale tunapokutana na changamoto, tunapaswa kujaribu kuzifanyia kazi  ili zibadilike kuwa fursa. Limao pekee ni chungu, lakini sukara na maji safi hugeuza limao chungu kuwa kinywaji kitamu cha kuburudisha. Maisha yanapoleta chungu na changamoto (limao), tunaweza kuwa wabunifu na wastahimilivu ili kubadilisha changamoto hizi kuwa fursa (juis).

Je, umewahi kubadilisha changamoto kuwa fursa?
Je! unajua misemo au mithani inayohusiana na kanuni hiyo hiyo?
Toeni maoni hapa chini!

Misemo inayohusiana kutoka kwa tamaduni mbalimbali:
Kizuizi cha hatua huendeleza hatua. Kinachosimama njiani kinakuwa njia.
- Tafakari za Marcus Aurelius (Roma ya Kale)

اِصْنَعْ شَرَابًا حَلُّوا مِنْ حَامِض لَيْمُون الْحَيَاةِ
Tengeneza kinywaji kitamu kutoka kwa asidi ya limau ya maisha.
-Methali ya Kiarabu 

जब भी जीवन में मुश्किलें आएँ तो उनका भी लाभ उठाएँ
Matatizo yanapotokea, tumia fursa hiyo pia. 
-Methali ya Kihindi

(Chanzo: Shukrani kwa Wiktionary)
...
Maelezo Picha hii iliundwa kwa kutumia Akili Bandia. Unafikiriaje? Je, picha gani ingefafanua methali hii vyema?
Ili kupiga KURA kwa Methali ya Mwezi
Kura
0
Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by

Maana

Mtu hawezi kuepuka hatima yake.

Matumizi

Methali hii hutumiwa nyakati za vita, au juu ya kiongozi pale ambapo wakati wa kuanguka umefika (mf. Macbeth). Tazama pia: Kile kinachozunguka huja karibu (What goes around comes around)

Utekelezaji

Hata ukijitahidi sana kufikiria, kuhangaika na kuepuka matatizo, bado yanaweza kujitokeza. Wakati mwingine, kujaribu kuzuia tatizo kunaweza kusababisha tatizo lilelile kutokea au kuifanya kuwa mbaya zaidi (mf. Oedipus). Nyani anaweza kuchagua tawi lingine ili kuepuka kuteleza, lakini tawi hilo pia linaweza kuteleza vile vile.

Katika hekaya za Kigiriki, hatima zilitajwa kama dada watatu: Clotho anayesuka uzi wa maisha (kuzaliwa), Lachesis anayechota uzi (akimpa kila mtu baraka na changamoto alizojaliwa maishani), na Atropos anayekata uzi (kifo).

Methali hii inatuhimiza kukubali ukomo wa nguvu yetu na kukiri kwamba mambo mengi muhimu yako nje ya udhibiti wetu.

Misemo inayohusiana


Kiswahili:
Ulichojaliwa hakipunguzi wala haiwezi kukuongezea
Siku za mwizi ni arobaini Siku za mwizi ni arobaini 

Kilatini (Stoic
Amor fati
Penda hatma 
 
Kichina (kutoka kwa Analects)
生死有命,富貴在天
Maisha na kifo vimepangwa, utajiri na heshima [hutoka] mbinguni.
...
Marejeleo
Ili kupiga KURA kwa Methali ya Mwezi
Kura
0
Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by
Methali ya leo, (Kiburi hutangulia anguko au kiburi huja kabla ya kuanguka) maana yake ni watu wenya kiburi sana wanaweza kufeli haraka. Mafanikio huleta kiburi, na kiburi hutupeleka kupuuza mambo muhimu. Pia ukijiamini sana, ni rahisi kukosa. Kiburi (au ego/ubinafsi) inaweza kutufanya tusione ukomo wa uwezo wetu wala uhalisia wa hali yetu.

Lakini kwa upande mwengine, katika dunia ya kisasa, watu wengi wanathamini zaidi fadhili za kujiamini na kujivunia. Ju kuna utofauti gani kati ya kujiamini (kitu kizuri) na kiburi (kitu kibaya). Toeni maoni, nawaomba!

Methali hii huhusishwa nna hadithi ya Ikarus, kutoka Ugiriki wa kale. (Someni kitabu chetu kipya chenye michoro, "Usiruke Karibu Sana na Jua").  Ikarus alipewa mabawa na baba yake, Daedalus. Mabawa hayo yalitengenezwa na manyoya na nta.  Daedalus akamwambia mwanake asiruke karibu sana na jua, lakini Ikarus alipuuza ushauri wa baba yake, akiruka juu sana, kwa kiburi. Jua liliyeyusha nta, na Ikarus akaanguka baharini na kuzama.

Titanic (Meli) ilijengwa kuanzia 1909. Kabla ya safari ya kwanza,  Phillip Franklin, mkuu wa kampuni aliandika:
There is no danger that Titanic will sink. The boat is unsinkable.
Hakuna hatari ya Titanic kuzama. Meli hii haizamiki.
Kwa sababu ya kiburi chao, hawakuwa na mashua (lifeboats) za kutosha kwa abiria wote, kwa ajili ya dharura. Mwaka wa 1912, Titanic ilizama, pamoja na watu zaidi ya 1500 waliofariki.

Katika fasihi, mashujaa wengi wa trajedy wanashushwa na majivuno na kiburi. Kwa mfano, katika kitabu cha Mflame Lear (na Shakespeare), kiburi cha mfalme kilimfanya awe katika hatari ya kubembelezwa, na uamuzi wake mbaya ukamgharimu kile alicho nacho. Kiburi cha Juliasi Kaizari kilimpeleka kusisitiza kwenda bungeni akipuuza maonyo mengi kwamba angeuawa. Vilevile, Oedipus (Mfalme Edipode) alijivunia sana, na hakusikiliza wengine waliomshauri, asitafute ukweli kuhusu wazazi wake.

Methali ya leo inatoka katika kitabu cha Mithali katika Biblia.
Kiburi hutangulia kabla ya uharibifu
na moyo wa kujivuna kabla ya maangamizi. 

Korani pia ina aya nyingi juu ya kiburi, kwa mfano:
ٱللَّهَ لَا يُحِبُّ مَن كَانَ مُخْتَالًا فَخُورًا 
Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi wenye kiburi wanao jifakhiri
Surah An-Nisa - 36

Hapa kuna baadhi ya mithali kutoka nchi mbalimbali juu ya kanuni hiyo hiyo.
Kifaransa:
Qui fait le malin tombe dans le ravin
Mwerevu huanguka kwenye bonde
Kirusi:
Сатана гордился, с неба свалился; фараон гордился, в море утопился; а мы гордимся - куда годимся?
Shetani alikuwa na kiburi, akaanguka kutoka mbinguni; Firauni alikuwa na kiburi, akazama baharini; na tunajivunia - tunafaa wapi?
Kiingereza:
The bigger they come, the harder they fall.
Kadiri wanavyokuwa wakubwa, ndivyo wanavyozidi kuanguka.
...
Maelezo Mchoro na Caspar David Friedrich, mwaka wa 1817, "Wanderer above the Sea of Fog / Der Wanderer über dem Nebelmeer / Msafiri Juu ya Bahari ya Ukungu"
Marejeleo
Ili kupiga KURA kwa Methali ya Mwezi
Kura
0
Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by
Methali hii ina maanisha hupaswi kutegemea matokeo mazuri kabla hayajatokea. Hupaswi kutegemea mayai yako yote yatakuwa vifaranga wenye afya nzuri. Je, una hadithi kuhusu methali hii? Toeni maoni!

Rekodi ya kwanza iliyoandikwa ya methali hii ya Kiingereza ni shairi iliyoandikwa mwaka wa 1570 na Thomas Howell:
Usiwahesabu kuku wako ambao hawajaanguliwa,
Pima maneno kama upepo, hadi upate uhakika

Lugha nyingi zina methali zinazofundisha kanuni karibu na hii. Mifano:

Kiswahili:
Tujivune hatimaye.

Kifaransa:
Il ne faut pas vendre la peau de l'ours avant de l'avoir tué.
Usiuze ngozi ya dubu kabla ya kumuua.

Kiarabu
لا تشتري السمك وهو في البحر بل انتظر حتى يصطاد
Usinunue samaki yumo baharini; subiri hadi itakapokamatwa.

Kijerumani:
Man soll den Tag nicht vor dem Abend loben.
Usisifu siku moja kabla ya jioni.

Kilatini:
Ante victoram ne canas triumphum
Usiimbe shangwe kabla ya ushindi.

Kireno:
Não conte com o ovo dentro da galinha.
Usihesabu yai ndani ya kuku.
...
Maelezo Picha hii ilichorwa kwa kutumia Akili Bandia (AI). Mnafikiriaje? Toeni maoni!
Marejeleo
 Wiktionary (Kamusi iliyo huru)
Ili kupiga KURA kwa Methali ya Mwezi
Kura
0
Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by
Methali ya leo inatoka katika hadithi ya Ugiriki ya Kale ya Ikarus ... na tuliwaandikia kitabu kifupi cha picha kuhusu hadithi ya Ikarus...

Soma sasa

Usiruke Karibu Sana na Jua


"Usiruke karibu sana na jua" ni onyo dhidi ya kiburi. Methali hii inatufundisha kwamba kiburi na tamaa vinaweza kuleta madhara mabaya ukipuuza  tahadhari, unyenyekevu na ushauri mzuri.

Kwa mfano, fikiria mjasiriamali mdogo. Anazindua bidhaa yake ya kwanza na anapata mafanikio ya haraka. Akiwa ametiwa moyo, anaanza kuweka mipango kabambe zaidi na zaidi. Anaamua kuomba mkopo mkubwa wa benki ili kuzindua bidhaa zaidi na kununua vifaa, mali na ardhi. Lakini ukuaji wa mauzo aliokuwa akitarajia haujitokezi, na anajikuta akichelewa na malipo ya mkopo. Hatimaye, biashara inazidi kuzama kwenye deni. Angeenda "njia ya kati," yaani kujenga mafanikio yake kwa hatua nyingi ndogo, na kusikiliza maonyo ya washauri wake, mambo yangeenda vizuri zaidi.

Tunaweza kutumia methali hii katika maisha yetu ya kila siku kwa kuelewa mipaka yetu, kwenda taratibu, kutafuta washauri na mamenta wenye hekima, na kuyasikiliza maonyo kutoka kwa wengine.

Je umewahi kuruka karibu sana na jua? Ilikuwaje? Pia, tafadhali tunaomba maoni yenu kuhusu kitabu cha Usiruke Karibu Sana na Jua!
...
Marejeleo
Ili kupiga KURA kwa Methali ya Mwezi
Kura
0
Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by
Nyakati za mafanikio, watu wanapenda kuhusishwa na kudai pongezi, hata kama mchango wao ulikuwa mdogo. Lakini mambo yanapoharibika, watu wanakimbia na hulaumiana. Hii ndo maana ya methali "Ushindi una baba wengi, kushindwa ni yatima." (Success has many fathers, failure is an orphan.)

Kwa mfano, fikiria kama umepokea pesa za wawekezaji ili kuanzisha biashara. Biashara ikifanikiwa, wawekezaji wataiona kama mafanikio yao, wataiita "biashara yetu", na itakuwa rahisi sana kutafuta wawekezaji wengi zaidi. Lakini ikiwa biashara imefeli, wawekezaji wako wataiita "biashara yako" na kuomba urudishe pesa zao.

Mara nyingi unaweza kutambua kiongozi halisi wa biashara, shirika au kikundi kwa kuona ni nani anayewajibika nyakati za changamoto na matatizo. Kiongozi bora ni yule ambaye anashiriki sifa na pongezi na wenzake nyakati za kufanikiwa, na anakubali kuwajibika na kulaumiwa nyakati za kushindwa.

Methali hii ilitumika na Rais wa Marekani, John F. Kennedy, mwaka wa 1961, akiongea na waandishi wa habari baada ya mgogoro wa "Bay of Pigs". Lakini inaonekana kwamba chanzo halisi cha methali hii ni cha kale zaidi... inatoka Mwanahistoria wa Roma ya Kale aliyeitwa Tasitus, katika biografia ya jenerali Agrikola kilichoandikwa miaka 98 baada ya kuzaliwa Kristo, akieleza changamoto ambazo jeshi la Roma lilikabiliana nazo katika ukoloni wa Uingereza. 
[Katika vita] sifa ya mafanikio hudaiwa na wote, wakati maafa yanahusishwa na mtu mmoja peke yake.
- Tacitus, Agricola

Je umewahi kuona mfano wa methali hii katika maisha yako? Tunaomba mawazo yako!
...
Marejeleo
Dr. Makirita Amani - Kisima cha Maarifa
Roma ya Kale

Kiingereza:
John F. Kennedy - Transcript of Press Conference, April 21, 1961
JFK never claimed to be the originator of this proverb and preceded it with "There's an old saying..."
He did popularize the phrase, as you can see from this Ngram chart from Google books, which shows the explosion in usage of the phrase after 1961.

Tacitus

Daily Stoic (from email archives):
It is precisely when things are good that we should be considering the possibility that someday they might not be so good. We should be acquiring allies. We should be doing favors and good for other people—because someday, we’ll need them to do the same for us. 

Portions of the image were made using AI, CC BY
Ili kupiga KURA kwa Methali ya Mwezi
Kura
1
Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by
Msemo huu unajulikana kama "Sheria ya Mashimo:" mtu ambaye yuko katika hali ngumu, hapaswi kuifanya kuwa mbaya zaidi.
Msemo huu husemwa wakati mtu amejiweka katika hali ngumu na anaendelea kufanya kosa lilelile. Kwa mfano, ukijikuta kwenye mahusiano mabaya, deni au uraibu, huwezi kutatua tatizo kwa kurudia kosa lilelile lililokufanya kuwa pale ulipo.

Mara nyingi nukuu ya "Sheria ya Mashimo" huhusishwa na Will Rogers, Bill Brock au Denis Healy, ila misemo karibu na huo inaonekana katika vyanzo kadhaa vilivyoandikwa kabla: 
[M]wenye hekima, akiona kwamba yumo shimoni [hata]chimba zaidi. (1911)

Kuna fursa nyingi zaidi leo kuliko zamani, lakini mtu ambaye amechimba shimo na bado anakataa kulitoka, anaweza kutarajia tu kujichimbia kwenye giza zaidi kadiri anavyochimba chini zaidi. Jibu la "Nyakati Ngumu" ni "Ukiwa shimoni, acha kuchimba -- inua kichwa chako -- fungua macho yako -- fikiria -- soma -- panda. Kupanda ni rahisi na kuchimba ni vigumu, na kadiri unavyopanda zaidi, ndivyo utakavyojikuta katika nchi yenye faida na furaha zaidi.” (1920)

Je, umewahi kufanya changamoto kuwa mbaya zaidi kwa kurudia kosa lililokuweka pale?
...
Marejeleo
Blog ya Jacob Mushi - Ukijikuta kwenye shimo
Law of Holes (Wikipedia)
1911 (Washington Post article)
1920 (Google Books)
Ili kupiga KURA kwa Methali ya Mwezi
Kura
0
Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by
Kazi kubwa ni rahisi kubeba kama watu wengi wanashirikana.

Methali hii inatofautiana na methali nyingine ya Kiingereza inayosema "Wapishi wengi huharibu mchuzi." Kama Baba yangu alivyosema, "Msemo ni 'mikono mingi kazi haba'... si 'mikono mingi kazi bora!'"

Ingawa chimbuko cha methali hiyo haijulikani kwa hakika, inaonekana katika mkusanyo wa Methali za Kiingereza za John Heywood (kitabu kilichapishwa Uingereza mwaka wa 1546). Ananukisha shairi "Jinsi Mke Mwema Alivyomfundisha Binti Yake" (karne la 14), shairi linalonikumbusha kuhusu Utendi wa Mwana Kupona.

Methali zinazofanana: 

Kichina: 
人多好辦事
Watu wengi, kazi nzuri

Kirusi:
берись дружно, не будет грузно 
Ishike pamoja, haitakuwa nzito
...
Marejeleo
Ili kupiga KURA kwa Methali ya Mwezi
Kura
1
Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by
Hapo zamani za kale kulikuwa na kijana aliyetafuta kipaji chake. Siku moja, alishauriwa na babu yake “Kila mtu ana kipaji, utafute chako.” Kwa hivyo, alianza safari ya kukitafuta.

Barabarani aliwakuta vijana wenzake wakicheza mpira wa miguu. Walimkaribisha na akaanza kucheza nao. “Labda hiki ndicho kipaji changu!” alijisemea moyoni.  Hata hivyo, mpira ulipomkaribia, aliogopa. "Sijui kupiga mpira!" akaasema. Wengine wakamkimbiza wakimchekea.

Mtaani, alikutana na mmachinga. “Labda hiki ndicho kipaji changu.” alifikiria. Mmachinga alimkubali, akamwagiza “Msalimie huyu mteja.” Lakini mteja alipomkaribia, kijana aliogopa, “Sijui jinsi ya kumsalimia mteja!” alisema kijana. Mmachinga alikasirika, na kijana akafukuzwa tena.

Akiendelea kutemebea alifikiria “Najuta kutoka leo, sina kipaji chochote.” Alipofika ufukweni, alikutana na mvuvi. Mvuvi alimkaribisha na akaingia mashuani. Mvuvi akampa kamba na kusema “Funga hii.” “Sijui kufunga kamba!” kijana alimjibu mara moja. Mvuvi akamjibu “Kama hujui kufunga kamba, funga nyingi.”

Baada ya siku hiyo, kijana alijifunza mengi kutoka kwa mvuvi, na alifunga maelfu ya kamba. Hatimaye, alikuwa mvuvi stadi aliyeheshimiwa na jamii.

Kipaji chako hakipo tu katika asili yako, bali kinaundwa na juhudi unazozitoa. Ukubali kufundishwa na wengine, na usiogope kujaribu vipya. Fundo la kwanza utakalofunga, hulifungwi vizuri sana. Lakini kadri unavyoendelea kufunga kamba nyingi, ndivyo utakavyojifunza mbinu na mikakati bora.

Yule anayesema "siwezi" hujizuia nafasi za kujifunza. Kama hujui jinsi ya kufanya kitu fulani, ujifunze kwa vitendo na mazoezi. Kama hujui kupiga mpira, piga mipira mingi. Kama hujui kusalimia wateja, wasalimie wengi. Kama hujui kufunga kamba, funga nyingi.
...
Marejeleo
Shukrani kwa Jan M anayetoka jimbo la Connecticut, Marekani, kwa kupendekeza methali hii kwetu!
Hadithi ni ya kwangu; inaruhusiwa kunakili / kuchapisha bila idhini ukitaja tu chanzo. CC BY
Ili kupiga KURA kwa Methali ya Mwezi
Kura
0
Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by
Hakika methali hii inaonyesha kanuni muhimu kuhusu mahusiano: Kutoa ahadi hujenga matarajio katika watu wengine. Tunapokosa kutimiza ahadi zetu, tunaharibu mahusiano yetu na jina letu. Ukitoa ahadi, jiulize, "Je, tungeandika mkataba wa maandishi unaosema hivyo, ningekuwa tayari kutia saini?" 

Kifaransa:
Chose promise, chose due.
Lililoahadiwa litadaiwa
Kirusi:
Долг платежом красен, а займы отдачею.
Deni ni nzuri linapolipwa, na mikopo inaporudishwa.
Kilatini:
Pacta sunt servanda
Makubaliano lazima yaheshimiwe. (Kanuni muhimu ya sheria ya kimataifa)
Kichina
口說無憑
Maneno yaliyosemwa hayana uthibitisho.
Kiingereza
Your word is your bond.
Neno lako ni dhamana yako.

Mnaonaje? Ahadi ina nguvu kama mkataba?
...
Marejeleo
Kirusi: attested to here and in this 1941 USSR propaganda poster
Kichina: 口說無憑 Spoken words are no guarantee.
Kiingereza: Word is bond
Ili kupiga KURA kwa Methali ya Mwezi
Kura
0
Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by
Kiingereza: Dress for the job you want, not the job you have.

Watu huona uwezo wako kupitia tabia zako na uhodari wako, lakini pia kupitia nguo zako. Ukitaka kuwa meneja, vaa nguo za heshima ili wafanyakazi wenzako waweze kutambua uwezo wako haraka zaidi. Ukitaka kuwa msanii, valia kama msanii. 

Methali haisemi watu wanapaswa kufanana, bali inatuhimiza tuanze leo kuishi maisha tunayotaka kuishi katika siku zijazo.
...
Maelezo Mchoro huu ulitengenezwa kwa kutumia Akili Bandia (AI). Mnafikiriaje?
Marejeleo
Sources

“You have to dress for the job you want, not the job you have, and you have to start doing the work you want to be doing.”

Ili kupiga KURA kwa Methali ya Mwezi
Kura
0
Iliharirishwa miezi 5 iliyopita
by
Methali ya leo ni "Haraka haraka haina baraka." Tafsiri yake kwa Kiingereza ni "Haste makes waste" au "Hurry hurry has no blessing" Mnaonaje - tafsiri ipi bora? Toeni maoni chini... 

Kwa upande wangu naona kwa mitazamo miwili. Methali hii inaweza kutufundisha:
  1. Subira: Haraka husababisha makosa, na makosa hutuzuia baraka. (Nenda taratibu)
  2. Mindfulness (yaani uwepo kiakili na utulivu): Tunapopoenda kwa haraka, hakuna muda wa kutambua, kutumia au kufurahia baraka tulizo nazo. 

Kuna misemo karibu na "haraka haraka haina baraka" katika nchi nyingi. Mifano: 
Kihispania: 
No por mucho madrugar amanece más temprano
(Kuamka mapema hakufanyi jua kuchomoza mapema)
Kifaransa: 
Tout vient a point a qui sait attendre
(Everything comes to those who wait)
Kiswahili:
 Pole pole ndio mwendo 
Kichina: 
欲速则不达
Methali hii ya Kichina ni karibu na "Haraka haraka haina baraka". Inatoka kitabu cha Misemo ya Konfusio (Analects, 13:17, ona ukurasa wa 92):
Tsz-hiá alipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Kü-fu, aliomba ushauri wa Konfusio juu ya serikali,  Konfusio akajibu "Usitamani matokeo ya haraka. Usiangalie faida ndogo. Ukitaka matokeo ya haraka, hayatakuwa ya mbali; na ukizingatia faida ndogo huwezi kukabiliana vizuri na mambo muhimu."

Katika kitabu cha  "Methali za Kiswahili Zaidi kutoka Afrika Mashariki" waandishi Kalugila na Lodhi walitaja methali hii kama mfano mzuri wa mtindo wa ushauri katika methali:
Kwa mujibu wa tarehe/historia, yaelekea kuwa mithali zilitangulia tungo za ushairi, na watungaji wa Kiswahili walikuwa na fursa ya kutumia hazina kubwa ya mithali zilizohifadhiwa na wakuzaji wa masimulizi na mapokeo ambao wengi wao walikuwa wanawake. Mithali za hapo mwanzoni bila shaka zilitungwa kwa mitindo ya ushairi ambayo polepole ikatakata na kuweka imara miundo ya arudhi/prozodi zilizokubaliwa kuwa za kawaida. Mithali za Kiswahili za kawaida mno, na zilizo fupi pia, ni zenye mizani 6, 8, 12 au 16. Nyingi zao hutumika katika tunga kama mistari, vipande au mikarara/vipokeo. Kuna mifano ming i ya mashairi yanayoanzia na mithali fulani na pia ni maelezo marefu ya mithali yenyewe.Katika mifano ifuatayo kutoka mashairi mbalimbali kuna ikaa (mwendo wa ulinganiful ya 3 + 3, yaani mizani 6 parnoja na kituo cha kati na mkazo kwenye mizani ya mwisho ila moja: [Mifano:] Akili ni mali. Mahaba ni haba. Mapenzi majonzi.
Kituo katika mithali na fumbo kisababishacho vipande 2, 3 au 4 ni sawa na kituo chenye ikaa/mwendo katika mashairi ya vina yenye mizani kamiIi zinazolingana. Vina vyenyewe vinaweza kuelezwa kama ifuatavyo. [Mifano]:
Haraka haraka / haina baraka (aaba, 3+3/3+3)
(Kwa) haba na haba / hujaza kibaba. (aaba, 3+3/3+3)
 
Niliuliza Akili Bandia "Nifanye nini ili kutekeleza methali ya "haraka haraka haina baraka katika maisha yangu ya kila siku?" Hapa ni shauri zake: (Nilihariri nukuu)
Kuweka Mipango: Kabla ya kuanza kazi/mradi, chukua muda wa kuweka mipango. Gawanya kazi kubwa katika hatua ndogo zinazoweza kudhibitiwa, na ujipe muda wa kutosha kukamilisha kila hatua vizuri.
Kufanya Maamuzi: Usifanye maamuzi kwa haraka na ya haraka, hasa kuhusu mambo muhimu. Orodhesha chaguzi zako zote, pima faida na hasara, tafuta ushauri, kisha ufanye chaguo sahihi.
Kujifunza: Badala ya kujaribu kusoma kitabu, darasa au zoezi la nyumbani kwa haraka, nenda polepole, jiulize maswali, soma tena na tena hadi uelewe nyenzo kikamilifu. Kwa njia hii utajifunza kweli na kukumbuka habari, badala ya kuisahau haraka. Pia utafurahia kujifunza mengi zaidi!
Mahusiano: Kujenga mahusiano imara huchukua muda. Iwe na marafiki, familia, au mapenzi, usikimbilie. Wekeza muda katika kumfahamu mtu, kumwelewa, na kujenga msingi imara.
Kazi: Zingatia ubora kuliko kasi, na uchukue muda wako wa mapumziko ili kuepuka uchovu. Epuka kuharakisha kazi zako ili kuzimaliza haraka. Ukienda haraka hautafanya kazi yenye ubora wa juu, lakini pia kufanya kazi kwa makini hukusaidia kujifunza na kukua.
Afya: Usitafute suluhisho la haraka wala njia za mkato katika masuala ya afya yako. Mazoezi, chakula safi, na mapumziko ni muhimu, na yote yanahitaji muda.
Kujiboresha: Ukuaji na maendeleo ya kibinafsi ni mchakato wa muda mrefu. Usiharakishe. Weka malengo yanayoweza kufikiwa, yafanyie kazi hatua kwa hatua, na uthamini ushindi mdogo unaoendelea.
Mindfulness (uwepo wa kiakili): Kuwa makini na mahali ulipo na kile unachokifanya. Wakati wa kula, furahia ladha kile unapotafuna. Unapozungumza na mtu, mzikilize kwa makini. "Haraka haraka haina baraka" inatufundisha maisha ni safari. 
Naona Akili Bandia alinipa ushauri mzuri wa busara... Ningependa kujua maoni yenu :)

Vitabu Vinavyohusiana:
More Swahili Proverbs from East Africa: Methali zaidi za kiswahili toka Afrika Mashariki by Leonidas Kalugila and Abdulaziz Y. Lodhi, ukurasa wa 77
Methali za Kiswahili - Swahili Proverbs ukurasa wa 202
Misemo ya Konfusio - Analects, 13:17, ukurasa wa 92 (Kiingereza kutoka Kichina)
Interpersonal Communication - A Mindful Approach to Relationships 

...
Marejeleo
Rasilimali:
Mindfulness (Jamii forums)
Wiktionary - "Haraka haraka haina baraka"
Swahili Proverbs about Hurry and Patience collected by Albert Scheven, Center for African Studies, University of Illinois, Urbana-Champaign
Google translate inaonyesha "Haste makes waste" tafsiri yake ni "Haraka haraka haina baraka" na inasema "reviewed by contributors." Lakini ukibadilisha nafasi (back translate) utaona "Haste has no blessing." Hm... Ipi bora?

Vyanzo vya methali za lugha nyingine:
Kichina: (Wiktionary)  (BBC)
Kihispania: (Wiktionary)
Kifaransa (le dictionnaire Orthodidacte)
Proverbial Leaders
# 1
56 proverbs added
37 comments
# 2
15 proverbs added
68 comments
# 3
0 proverbs added
16 comments
# 4
0 proverbs added
9 comments
# 5
0 proverbs added
0 comments
# 6
0 proverbs added
0 comments
# 7
0 proverbs added
0 comments
# 8
0 proverbs added
0 comments
# 9
0 proverbs added
0 comments
# 10
0 proverbs added
0 comments