You are now browsing in English. Switch to Swahili
In Swahili: "Sasa unavinjari kwa Kiingereza. Rudi kwa Kiswahili"
You need to login to view profiles OR to update your profile

Create a new account

New announcements
Discussions
Proverbs

Majani huonekana ya kijani zaidi upande mwengine

Join
or login
to VOTE for Proverb of the Month
Votes
0
Updated 5mo ago
by
View this proverb in English
The grass is always greener on the other side
Methali hii inahusiana na tabia ya kufikiria kwamba watu wengine wana vitu vizuri zaidi, hali nzuri zaidi nk... Kwa mfano kufikiri jirani yako ana majani mazuri kuliko wewe.

Chanzo cha methali hii ni "Sanaa ya Upendo" na Ovid, kitabu cha mashairi yaliyotungwa ili kutoa shauri kwa wanaume na wanawake kuhusu kutafuta na kudumisha mahusiano ya kimapenzi. Kitabu hiki kiliandikwa zaidi ya miaka 2000 iliyopita, takribani 2 KK:
Watu hutaka furaha mpya. Huwa tunaona kuwa watu wengine wana bahati zaidi kuliko sisi wenyewe. Mazao daima ni bora katika shamba la jirani yetu; ng'ombe wake hutoa maziwa zaidi. 
 - Ovid Ars Amatoria (Sanaa ya Upendo), Ukurasa wa 24

Kwa upande mmoja, methali hii inamaanisha, bora kushika kile ulicho nacho, na kupuuza kile ambacho wengine wanacho, hata kama inaonekana ni bora zaidi. Lakini pia kwa mtazamo mwengine, inamaanisha bora kutumia akili yako katika kuboresha hali yako mwenyewe (kama kumwagilia shamba lako) badala ya kufikiria sana ukweli kwamba shamba lako, au hali kwa ujumla, ni duni. Methali nyingine ni "Majani huonekana ya kijani zaidi pale ambapo yalipomwagiliwa maji." 

Methali zinazofanana kikanuni:
Kihindi: 
दूर के ढोल सुहावने लगते हैं
Ngoma za mbali husikika vizuri
Kichina: 
隔籬飯香 
Wali wa jirani hunukia vizuri
Kijapani:
隣の芝生は青く見える
Majani ya jirani huonekana kijana zaidi
Kurusi:
соседняя очередь всегда движется быстрее
Foleni nyingine husogea kwa kasi zaidi
Sources
Ars Amatoria (Sanaa ya Upendo), Ukurasa wa 24
The grass is always greener on the other side (Wiktionary)
Japanese (Wiktionary)
Hindi (Wiktionary)
Chinese (Wiktionary)
Russian (Wiktionary)
Loading...
Loading...
Login to view and post comments
Maana yake, afadhali kuridhika na ulicho nacho, badala ya kuiweka hatarini kwa ajili ya kupata kitu kubwa zaidi.

 Methali hii ni ya zamani sana. Chanzo cha methali hii ni kitabu cha kale kiitwacho  "Hadithi ya Ahikar." (Kinajulikana pia kama "Methali za Ahiqar.")
Mwanangu, mguu wa kondoo katika mkono wako mwenyewe ni bora kuliko bega zima katika mkono wa mwengine; Afadhali kondoo mdogo aliye karibu na wee kuliko ng'ombe aliye mbali; Afadhali shomoro aliyeshikwa mkononi kuliko ndege elfu warukao angani; vazi ulilo nalo ni afadhali kuliko vazi la zambarau usiloliona.
- Hadithi ya Ahikar (ukurasa wa 110)
Kitabu hiki kinasimulia hadithi ya mshauri wa wafalme wa kale wa Ashuru na Misri. Inadhaniwa kuwa hadithi hii ilitungwa takribani 600 KK, na kuna nakala iliyochapishwa mwaka wa 500 KK. 

Methali karibu na hii kutoka nchi mbalimbali:
French:
Un tiens vaut mieux que deux tu l'auras
'Shika-hii-hapa" moja ina thamana kuliko 'nitakuletea-baadaye' mbili
Japanese
明日の百より今日の五十
Hamsini leo ni bora kuliko mia kesho
Italian
Meglio un uovo oggi che una gallina domani
Bora yai leo kuliko kuku kesho

Mnaonaje -- methali hii ni ushauri mzuri? Ni bora kuridhika na kitu kinachopatikana kwa hakika, ama kutafuta kitu bora zaidi kisicho na hakika?
...
Updated 5mo ago
by

Je, una ndoto kubwa?

Ndoto ambayo huwezi kuitimiza peke yako? Labda hata ambayo haiwezi kukamilika katika kizazi kimoja?

Kuna makanisa ya kigothi barani Ulaya ambayo yalichukua zaidi ya miaka 600 -- zaidi ya vizazi 20 -- ili kukamilisha ujenzi!

Ingawa Piramidi kubwa zaidi ya Giza imejengwa kwa kasi (ndani ya kizazi kimoja), ila pia ilichukua makumi ya maelfu ya watu.

Nchini Tanzania, Msikiti Mkuu wa Kilwa Kisiwani ulijengwa katika karne za 11-14, ukajengwa upya baada ya tetemeko la ardhi, na uliendelea kufanyiwa ukarabati hadi karne ya 18. Ulitajwa pia miaka ya 1300 na msafiri Ibn Battuta. (Je ulijua unaweza kuona Kilwa Kisiwani kupitia "ziara ya mtandaoni" yaani 3D Virtual Tour? Ona kiungo chini kwenye "Rasilimali")

Maajabu ya dunia, ya kisasa na ya kale, yalianza kama ndoto kubwa, ndoto ambazo zilichukua vizazi vingi kutimiza. Kila kizazi kiliendeleza kazi ya zamani na pia walitoa mchango wao kwa kubadilisha mipango ya siku zijazo. 

Hivyo bhasi, kama unajaribu kufanya jambo kubwa -- jambo ambalo hakika litabadilisha ulimwengu - usitarajie litafanyika kwa siku moja. Na usijaribu kuijenga peke yako. 

Methali Zinazohusiana:


 Kiswahili:
Ukitaka kwenda haraka, nenda peke yako, ukitaka kwenda mbali, nenda na wenzako

Kifaransa:
Rome ne fu[t] pas faite toute en un jour
Kutoka kitabu cha Li Proverbe au Vilain kilichochapishwa takriban mwaka wa 1190
Kifaransa cha kisasa: Rome ne s'est pas faite en un jour
Maana yake: Roma haikujengwa kwa siku moja

Kichina:
冰凍三尺,非一日之寒
Mita ya barafu sio kwa sababu ya siku moja ya baridi

Kigaelic
Chan ann leis a’ chiad bhuille a thuiteas a’ chraobh
Sio pigo la kwanza linaloangusha mti
...

Picha: Shukran kwa Zamani Project waliounda ziara ya mtandaoni ya Kilwa Kisiwani!

Updated 5mo ago
by

Ufafanuzi


Methali hii ya Kiingereza inatafsirika pia kama "Kalamu ina nguvu kuliko upanga au jambia" au " Kalamu ni kali kuliko upanga." Katika methali hii, jambia au upanga unaashiria nguvu na ukatili, na maana ya kalamu ni maneno. Ingawa upanga unaweza kushinda kwa nguvu, kalamu inaweza kuwashawishi, kuwahamasisha, na kuwaelimisha watu. Sio kila mtu ana silaha za kuwalazimisha watu wengine kufanya kile anachotaka, lakini kila mtu ana uwezo wa kubadilisha ulimwengu kupitia kile anachofikiria, kusema na kuandika kwa maneno. 

Silaha za siku hizi ni kalamu na karatasi.
 - Methali ya Kiswahili

Methali hii ni kweli kwa sababu mara nyingi maneno huchochea na kudhibiti jinsi watu wanavyotumia nguvu na silaha zao. Kwa mfano, kupitia sheria, maneno ya viongozi, mahakimu na majaji yana uwezo wa kuwafunga watu gerezani au hata kuwaua. Kutoa hotuba ya moto kwa umati wa watu wenye hasira kunaweza kuleta ghasia kali na madhara mengine (ona Juliasi Kaizari).

"Ukinipa picha, nitakupa vita."
- William Randolph Hearst
(Mwandishi wa habari na mchapishaji wa magazeti, Marekani)

Lakini pia, methali hiyo inatukumbusha nguvu ya upinzani usio na vurugu kwenye kuleta mabadiliko ya kudumu, kanuni iliyotetewa na kuonyeshwa na watu kama Mahatma Gandhi, Martin Luther King, na Nelson Mandela.  Angalia pia: Insha ya "Civil Disobedience"  na Henry David Thoreau, pamoja na Tamthilia mashuhuri ya "Antigone" na Sophocles.

Chimbuko


Nukuu hii ya "kalamu ina nguvu kuliko upanga" ilipata umaarufu kupitia tamthilia ya "Richelieu: au The Conspiracy"  na Edward Bulwer-Lytton (mwaka wa 1839, ukurasa wa 47). Lakini hakika wazo lilikuwepo kabla.

Wengine wanasema chimbuko halisi la methali hii ni Hadithi ya Ahikar. Kitabu hiki kiliandikwa takriban miaka 600 kabla ya kristu, na ni chimbuko la methali zingine kama "Ndege mkononi ana thamani ya wawili mtini"). Katika toleo letu, mfasiri hakuweza kusoma maandishi kutokana na hali ya karatasi, na maneno yalikatika. (Ukurasa 171/274
Dhibiti kinywa chako kwa uangalifu ...[ILIKATA]... na ufanye moyo wako kuwa mzito(?), kwa maana neno linalosemwa ni kama ndege, naye alitamkaye ni kama mtu asiye na  ...[ILIKATA]... ufundi wa maneno una nguvu zaidi kuliko ufundi wa  ...[ILIKATA]...
- Hadithi ya Ahikar, Ukurasa wa 171/274
Je, hili ndilo chimbuko halisi la methali hii, miaka zaidi ya 2,500 iliyopita? Muwe majaji...

Chanzo karibu na methali hii pia kinaonekana katika Agano la Kale:
Kwa maana neno la Mungu ni hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili.
Waebrania 4:12, Biblia

Na vilevile katika Shakespeare: 
Wengi wanaovaa panga huogopa kalamu.
-William Shakespeare
Tamthilia ya Hamlet, Sehemu ya 2, Onyesho la II (ukurasa wa 59)

 Je, unakubali kalamu hushinda jambia? Toa maoni yako hapo chini!
...

CC BY Unaruhusiwa kunakili & kusambaza mchoro huu na makala hii bila idhini, ukitaja tu chanzo (www.maktaba.org)

Updated 5mo ago
by
The winner of a competition or conflict receives the majority or entirety of the rewards, and possibly additional benefits beyond what was being fought over. 

In war, the spoils could refer to land, gained power or other sought after resources. In other pursuits the spoils typically refer to accolades, money or opportunities.

The proverb is typically used to explain unequal outcomes or to remind others that the stakes of many conflicts are winner take all, zero sum, or at the very least, disproportionately favorable to the few winners.

Check out the sources section for a description of the context and information about the US politician who was credited with the phrase (in the 1830s).
...
Updated 5mo ago
by