View this book in English Fish handling, quality and processing : training and community trainers manual
Jiandikishe upate habari na vitabu bure!
Ubora na Uchakatji wa Samaki
Mwongozo wa Mafunzo kwa Wakufunzi wa Jamii
Mchapishaji SmartFish
Mwaka 2012
sw
Kurasa 124
Pakua 3.4 MB
Sekta ya Uvuvi hutoa chakula na ajira kwa mamilioni ya watu, na pia walaji wa samaki wana haki ya kula samaki waliovuliwa, kuhifadhiwa na kuandaliwa vizuri. Walaji wengine wana wasiwasi kuhusu jinsi chakula kinavyoandaliwa kabla hawajala chakula hicho. Wanajali sana ubora, na wanakuwa na wasiwasi kuhusu kilichotokea kwa samaki kabla hawajamla. Hivyo, inabidi wawaamini wavuvi, wachakataji na wafanyabiashara ya samaki kwamba watakuwa makini na samaki wanaowavua na kuwahudumia. Mwongozo huu wa wakufunzi umetolewa na kamisheni ya bahari ya Hindi, programu ya “Smart Fish" kama hitaji la biashara ya kikanda. Uvuvi ni moja ya raslimali muhimu inayoongezeka ambayo nchi za Mashariki na Kusini mwa Afrika zinayo kwa ajili ya usalama wa chakula, maisha ya watu na kukua kwa uchumi. Hata hivyo juhudi zinatakiwa kufanyika kuhakisha kuwa jinsi idadi ya watu inavyoongezeka katika nchi hizi ndivyo mahitaji ya chakula na ajira yanavyoongezeka, faida zinazotokana na raslimali ya uvuvi zitalindwa kupitia usimamizi endelevu na uongeza thamani. IOC iliongoza mpamgo wa utekelezaji wa malengo ya uvuvi Kikanda kwa ajili ya Kanda ya ESA - I0 (IRFS) {SMARTFISH} iliyozinduliwa February 2011 ikiwa na malengo ya kuongeza viwango vya Maendeleo ya jamii, uchumi, mazingira na mahusiano ya kikanda katika Ukanda huu kupitia uvunaji endelevu wa raslimali ya uvuvi. Kufanikisha mpango huu ni kuainisha mikakati ya kikanda na kuimarisha mahusiano ya kikanda hasa katika ubia na COMESA, EAC, and IGAD. Hatimaye watakaofaidika ni wavuvi na jamii ya watu wanaoishi katika ukanda wa pwani na wakazi wengi waliopo nchi za Burundi, Comoros, Djibouti, Democratic Republic of Congo, Eritrea, Ethiopia, Kenya, Madagascar, Malawi, Mauritius, Rwanda, Seychelles, Somalia, Sudan, Swaziland, Tanzania, Uganda, Zambia na Zimbabwe.
...
Ni lengo la Programu ya Smartfish kuhakikisha kuwa mwongozo huu wa wakufunzi unatumika Kama chombo cha kuongoza utekelezaji Kwa washika dau wate ili kuimarisha uhuduniaji, kanuni za usafi na usafishaji, sambamba na viwango vya COMESA na EAC Kwa manufaa ya biashara ya kikanda, ajira na usalama wa chakula.
...
Shukrani kwa Mkulima
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all

No Books Found

Based on the filters you selected, there are currently no books.