Mafunzo ya Kifedha
Kozi Fupi ya Wiki 5 - Kitabu cha Mwalimu
Publisher UNCDF & WFP
sw
Download 4.0 MB
Ujuzi wa kifedha ni nini? Ujuzi wa kifedha ni mkusanyiko wa mbinu na maarifa vinavyomwezesha mtu kufanya uamuzi mwafaka kuhusu namna ya kutumia pesa. Ujuzi wa kifedha huzingatia ujuzi, maar- ifa, mbinu, na tabia za kifedha vinavyo- hitajika ili kufanyia uamuzi mwafaka wa kifedha ili kufikia kilele cha usitawi wa kifedha kwa mtu binfsi. Kuwa Kuwa mtu mwenye ujuzi wa kifedha ni pale ambapo unafahamu kanuni za msingi za kifedha kama vile: • Kuhifadhi pesa zako • Wapi na namna ya lufungua akaunti • Kuweka kumbukumbu mwafaka za shughuli zako za kifedha • Namna ya kupata usaidizi wa kifedha Kwa nini ni muhimu kuwa na ujuzi wa kifedha? • Mtu mwenye ujuzi wa kifedha huwa anafanya uamuzi mzuri katika shughuli zake za kifedha • Ana pesa za kugharimia dharura na mambo muhimu (kutoka hifadhi yake) • Pia utaweza kukopa pesa kwa urahisi bila vikwazo • Kuna unwezekano mkubwa kwamba mtu huyu hatafanya uamuzi mbaya wa kifedha utakaodhuru familia yake na biashara yake • Kuwa na maarifa yanayoongeza nam- na mtu huyu anavyofahamu shughuli zake za kifedha • Kuwa na mbinu zinazomwezesha kutekeleza maarifa yake ya ujuzi wa kifedha ili kutawala pesa zake • Kupata ukakamavu na tabia chanya inayomwezesha mtu kuwa na uhakika kuwa atafanya uamuzi mzuri wakati akishughulikia pesa zake
...
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all

No Books Found

Based on the filters you selected, there are currently no books.