You need to login to view profiles OR to update your profile

Have an account? Login

Log in
Forgot your password?
Didn't receive your confirmation email?

Create a new account

Sign up for news and free books by email!
Jenga Maisha Yako
A Femina Hip Girl Power Programme
Publisher Femina Hip
Published 2017
sw
Wapendwa Wasichana, Sasa mko katika hatua muhimu sana ya safari ya mafanikio. Mnapata fursa ya kujifunza na kuandaa maisha yenu ya baadae. Mkiwa shule mtajifunza kuhusu masomo, na kujipanga kuhusu aina za kazi mnazotaka kuzifanya mkimaliza masomo. Wengi mna ndoto mbalimbali za maisha, lakini kuna changamoto nyingi sana katika jamii zetu, mojawapo ni fursa za ajira. Changamoto hizi mnaweza kuzishinda endapo mtafanya maamuzi yanayoongozwa na taarifa sahihi. Kupitia mafunzo haya ya Femina ya “Jenga Maisha Yako” mtajifunza kuhusu kujitegemea, thamani ya kuanzisha biashara yako, aina mbalimbali za biashara, usimamizi wa fedha, namna ya kushinda changamoto na kufanya uamuzi bora. Katika mafunzo haya ya Femina Hip ya “Jenga Maisha Yako” mtaweza: b KUWA JASIRI, na kujua kwamba mnaweza kufanikiwa kama wasichana wafanyabiashara. b KUPATA TAARIFA kuhusu misingi ya kufanya biashara. b Kutumia maarifa hayo KUWA MAKINI na kutafuta masoko na fursa mpya. Mafunzo haya yanawahusu NINYI tu. Yameandaliwa kuwa shirikishi na tunategemea mtafurahia sana! Kutakuwa na fursa nyingi kwenu kushiriki katika majadiliano na shughuli nyingine. Zungumza bila kuogopa, acha wengine wote darasani wajue una nini cha kusema. Sauti yako ni muhimu.
...
Kitabu hiki kimetayarishwa na Timu ya Femina Hip. Femina ni shirika la kiraia linalotumia vyombo mbalimbali vya habari kuwafikia vijana, likifanya kazi na vijana hao, jamii zao pamoja na wadau mbalimbali kote nchini Tanzania. Elimu kupitia burudani ndiyo njia tunayoitumia – tunaburudisha na humo humo tunaelimisha walengwa wetu kwa kutumia visa vya maisha ya kila siku na shuhuda za watu mbalimbali. Tunatoa nafasi kwa sauti za vijana kusikika kwa kupitia kazi zetu tofauti – majarida ambayo kutoka mara kwa mara, luninga, redio, mitandao ya kijamii, ujumbe mfupi wa simu pamoja na shughuli za nje ambazo hufanywa uso kwa uso kama vile matamasha.
...
Have thoughts on this book?
Add a comment to get the conversation started!
Before viewing or adding comments, you must create an account. It takes just seconds!
Related books: Browse all