Kuelekea kwenye Vituo vya Kutolea Huduma za Afya Visivyo na Unyanyapaa
Toward Stigma-Free Health Facilities in Tanzania: A Guide for Trainers

Language: sw
Details: Mwongozo huu umeandaliwa na Dr. Laura Nyblade na Christin Stewart (RTI International), Pfiraeli Kiwia na Willbrord Manyama (Kimara Peer Educators), na Rebecca Mbuya-Brown na Sara Bowsky (Palladium) wa Health Policy Plus. Health Policy Plus (HP+) ni mradi wa miaka mitano unaofadhiliwa na U.S. Agency for International Development
Summary: Lengo kuu la mwongozo huu ni kutokomeza unyanyapaa na ubaguzi katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa kutoa mafunzo kwa watendaji wa ngazi zote katika vituo vya kutolea huduma za afya. Hatua katika Kubadilisha Mitazamo: Programu hii ya mafunzo inalenga katika kuibua vitendo – sio tu kuuelewa unyanyapaa na ubaguzi na namna ambavyo huathiri huduma za afya kwa njia iliyo hasi, bali vitendo halisia vya kutokomesha unyanyapaa na ubaguzi. Kila zoezi linadhamiria “kuibua” adhma ya ndani ya washiriki ili wabadili mitazamo yao, kujaribisha tabia mpya, na kuchukua hatua kukabiliana na unyanyapaa na ubaguzi katika vituo vyao vya kutolea huduma za afya.