Mwongozo wa Kusoma kwa Ufahamu
Mchapishaji 21st Century Basic Education Program (TZ21)
Mwaka 2015
sw
Pakua 1.0 MB
Malengo ya mwongozo huu wa Kusoma kwa Ufahamu ni kuwapatia walimu msaada maalumu, mifano, na mikakati ya kuboresha uwezo wa usomaji kwa ujumla na ufahamu kwa wanafunzi. Mwongozo huu utatoa: 1. Historia fupi na maelezo ya usomaji, kufundisha kusoma na kusudi maalum la kufundisha ufahamu, 2. Misingi ya ufundishaji fanisi wa kusoma kwa ufahamu kwa wanafunzi wa madarasa ya chini kwa kutumia mazingira na zana za kawaida, 3. Jinsi ya kufundisha kusoma katika kundi kubwa, 4. Jinsi ya kufundisha kusoma katika vikundi vidogo, na 5. Jinsi ya kuwasaidia wanafunzi wanaosoma kwa shida. Walimu wanaweza kutumia taarifa zilizomo katika mwongozo huu kuboresha maarifa yao ya jumla ya kufundisha kusoma, kujifunza mambo yanayopaswa kuangaliwa katika ufundishaji bora wa kusoma na kuelewa jinsi ya kutumia matini waliyo nayo katika madarasa yao ili kubuni na kufundisha kwa ufanisi kusoma kwa ufahamu.
...
Mafunzo haya ya ziada ya Kusoma kwa Ufahamu na mwongozo huu kwa walimu wa darasa 1 na 2 ni matokeo ya msaada wa watu wa Amerika kupitia ufadhili wa Shirika la Misaada ya Kimataifa ya Mendeleo la Marekani (USAID) kwa Programu ya Elimu ya Msingi ya TZ21. Msaada huu wa watu wa Marekani unalenga kujenga uwezo wa watoto wa Tanzania kielimu.
...
Shukrani kwa 21st Century Basic Education Program (TZ21)
Una maoni juu ya kitabu hiki?
Toa maoni yako ili kuanzisha majadiliano!
Kabla ya kuona na kutoa maoni, lazima uingie kwenye akaunti. Kutengeneza akaunti ni rahisi na bure,na huchukua chini ya dakika 1!
Vitabu vinavyohusiana: Browse all

No Books Found

Based on the filters you selected, there are currently no books.